Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi

Shida yako ni uhuru wa kupata wanawake wengi ndo unakusumbua. Hakuna dini sahihi bali kuna IMANI SAHIHI.
Hicho ndicho kitu pekee unakiwaza ahh

Kwani hujawai sikia pdre ako na mke na sio mke tuu Ana wake.

Mkuu mungu ni zaidi ya hicho unachokiwaza na dini ni sehem bora kumtazamia mungu.
 
Pole sana ndugu. Lakini bado kuna tumaini la kupata maisha mapya katika Yesu Kristo alie ile kweli. Makanisa mengi yaleo yamekosa ile nguvu ya roho mtakatifu tuliyoahidiwa sisi tulio watoto wa Mungu. Napenda nikushauri mambo mawili yafuatayo especially kwa kuwa umetoka katika background ya Roman Catholic na inaonekana baada ya kutoka huko ukaangukia kwa matapeli wa imani:-

1. Soma maandiko/Chimba ukweli kutoka katika maandiko (usiamini maneno matupu ya wanadamu)
Yohana 5:39
[39]Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Search the scriptures; for in them ye think ye have eternal life: and they are they which testify of me.

Matendo ya Mitume 17:11
[11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
These were more noble than those in Thessalonica, in that they received the word with all readiness of mind, and searched the scriptures daily, whether those things were so.

Ukweli wa Bwana Yesu utaupata katika maandiko maana kwayo yeye anashuhudiwa na wala sio kwa maneno ya wanadamu.

2. Ishi kama yasemavyo maandiko
Misingi na kanuni za maisha yako ikiwa kama maandiko yanavyoelekeza basi utaanza kuuishi ule utakatifu aliouhubiri Yesu Kristo na utaingia rasmi katika lile kundi la watakatifu ambao ndio Yesu Kristo atarudi tena kwa ajili ya hao, maana ndio walioahidiwa kuurithi ufalme wa mbinguni.

Achana na mambo ya itikadi za kidini, sijui Usabato, mara Upentecoste, sijui Uprotestant au Ukatoliki, wala Uislam. Hizi itikadi haziwezi kukufikisha mbinguni. Maana tangu mwanzo Mungu alitutaka tuwe watakatifu na kuuishi utakatifu (sio Ukatoliki, Upentekoste, Uprotestant wala Uislam)

Mambo ya Walawi 20:7-8
[7]Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Sanctify yourselves therefore, and be ye holy: for I am the LORD your God.
[8]Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
And ye shall keep my statutes, and do them: I am the LORD which sanctify you.

1 Petro 1:15-16
[15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
But as he which hath called you is holy, so be ye holy in all manner of conversation;
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Because it is written, Be ye holy; for I am holy.

Ni vyema ukajua pia hata kanisa aliloliasisi Yesu Kristo halikuwa na itikadi yeyote ile, ila imani ya utakatifu. Hivyo unatakiwa kuwa mtakatifu na kuondokana fikra za itikadi za kidini ili uwe sawa na Yesu Kristo.

1 Wakorintho 1:2
[2]kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
Unto the church of God which is at Corinth, to them that are sanctified in Christ Jesus, called to be saints, with all that in every place call upon the name of Jesus Christ our Lord, both theirs and ours:

1 Wakorintho 16:1
[1]Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
Now concerning the collection for the saints, as I have given order to the churches of Galatia, even so do ye.

Watakaotawala na Mungu kule mbinguni ni wale walio watakatifu tu.

Ufunuo wa Yohana 20:6
[6]Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Blessed and holy is he that hath part in the first resurrection: on such the second death hath no power, but they shall be priests of God and of Christ, and shall reign with him a thousand years.

Naamini utachagua lililo fungu jema. Mungu wangu wa mbinguni na akusaidie kufanya uamuzi ulio sahihi.
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
Karibu judaism
 
Nenda dini zote ila sio dini ya Kiyahudi ama Muslim. Hizi Imani zimejaa ukatili mkubwa sana. Angalia jinsi Mayahudi yanavyoua watu huko Gaza. Muislam nae anukuua huku anasema Allah Akbar. Angalia juzikati walivyoa wakristo huko Kongo na kule syria.Yaani anamuhusisha Mungu kwenye uovu wake.!. Ukitaka kuwa mkatili na kuchukia binadamu wengine jiunge na hizo Iman. Bora ubaki kwa Yesu maana alitutaka tuwapende watu wote. Yesu hakubagua.
Kwenye hii dunia namuogopa Sana Myahudi na Muislam.
Hicho ndicho shetani anataka yaani kumuona mwenzio hafai wakati mungu katuweka wote tuwe sawa.

Hamna aliye bora zaidi ya mwenzie mbele ya mungu wote tuko sawa
 
Jifunze maneno ya Mungu lakini usiwe mfuasi wa Dini yeyote kabisa!

Itakusaidia Sana na kukuweka huru!
 
Karibu sana katika Uislam. Uislam ndio Dini yako ya asili. Unaposilimu unakuwa unarudi katika asili. Uislam ndio Dini ya maumbile yako. Rudi katika maumbile yako halisi. Moyo wako hauna utulivu deep down kwa sababu haupo katika maumbile yako halisi. Ulizaliwa katika Fitrah (maumbile ya asili) ya Uislam, ila wazazi/walezi wakakubadilisha. Tumeumbwa sisi kumuabudu Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote kile (kuwa Waislam).

Mitume (Amani iwe yao) walikuja kuwaongoza watu na kuwarekebisha pale ambapo Fitrah yao ilipochafuliwa, Mitume wakaletwa kuwasafisha na kuwaongoza watu kurudi katika Fitrah yao, warudi kumuabudu Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote.

Yule Aliyeumba kila kitu na ni Muweza juu ya kila kitu Ndiye Anayestahiki Kuabudiwa na Anaabudiwa vile anavyotaka Yeye kwa sababu Yeye Ndio Mjuzi juu ya kila kitu. Ndio maana kaleta Mitume ili wawalinganie watu wao warudi katika Fitrah (maumbile ya asili) yao ya kumuabudu Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote kile na Allah Akawafunulia Mitume hao namna ya kumuabudu Yeye wakawafundisha jamaa zao.

Mitume wote walikuja kuwalingania na kuwaongoza watu wao kurudi katika maumbile ya asili na lengo la kuumbwa kwao wamuabudu Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote.

Kila watu walipopotoka katika maumbile yao halisi na wakaacha mafundisho ya Mitume, Allah Alileta Mtume mwengine mpaka alipokuja Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Mitume wote ikiwemo Nuh, Ibrahim, Musa, 'Iysa/Yesu na Mtume wa Mwisho Muhammad ambaye alitumwa kwa watu wote kwa zama zote mpaka Qiyama na akawa ni Mtume wa Mwisho na hakuna Mtume wala Nabii baada yake (Swala na Salamu ziwe juu yake na juu ya Mitume wote) walikuja kuwarudisha watu katika lengo la kuumbwa kwao.

Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) ndio Mtume wa mwisho na ndio alikuja na Sheria ya mwisho kutoka kwa Allah, na Sheria hiyo itabaki mpaka Qiyama, na wafuasi wa manabii waliopita wanawajibiwa kumfuata Mtume wa Mwisho pamoja na Sheria aliyokuja nayo kutoka kwa Mola wake.

Hivyo mkuu nodetz Uislam ndio Haqq na ndio njia ya sawa na ndio ndio Dini ya Manabii na Mitume wote wa Allah (Amani iwe juu yao Manabii na Mitume wote) na ndio Dini yako ya asili.

ayat 64 from Surah Al Imran
﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ﴾
[ آل عمران: 64]

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.
Mtoa mada Kama kweli unatafuta dini ya kweli hii Comment ndo imemaliza kila kitu,jamaa amejitahidi kuelezea na Huu ndiyo ukweli.
Cha kukujazia,ni kwamba nadhani Unaona ht humu watu wanavyohangaika kukupa majibu/uelekeo sahihi ndo Unaona kila mtu anaongea lake anavyoona yeye,yan ni fujo....hii fujo inaletwa kwasbb watu hawataki ukweli,watu hawataki hii DINI ya kweli ya kiislam,kama alivyosema Mkuu Hapa ni kwamba ile FITRAH haipo tena Kuna vitu/watu wanaowaamini wao wamewaaminisha na kuwadanganya kwamb UISLAM ni DINI kma DINI nyingine,hii siyo kweli mkuu.
Hebu jiulize hivi:
MUNGU MKUU ALIYEUMBA MBINGU NA DUNIA NA ALIYETUUMBA SISI WOTE HIVI MUNGU HUYU AUMBE KISHA ARUHUSU TU KUABUDIWA KAMA FUJO ETI KILA MTU AMUABUDU INAVYITAKA AKILI YAKE,YAN ASHINDWE KUTOA MUONGOZO MMOJA NAMNA GANI WATU WAMUABUDU?
Yan hata wewe tu Kwenye nyumba yako umeweka MUONGOZO kila aliyechini yako Lazima afuate Hiyo sheria,na Huwezi kuruhusu mtotO Au mke alete sheria/MUONGOZO wake humo ndani,huwez kukubali hiyo,

Sasa wewe inakuingia akilini eti Mungu aweze kuumba Afu ashindwe kuleta Muongozo?
Hao watu unaowaona wanatapatapa na hta Huko nadhani umewaona,hao wanahangaika kwasbb ukweli hawaujui na hawahangaiki Kama wewe kuujua na kuutafuta,washaharibiwa na wazazi wao,wameshatolewa ile fitrah/asili ambayo ni Uislam.nakusihi rudia tena kusoma Comment ya Mkuu hapo juu ili uelewe vzr lkn pendelea kuusoma uislam,utapata kweli yote na utagundua Kwanini watu wanahangaika.
Njoo Kweny UISLAM,dini iliyonyooka,dini ambayo inaeleza kila kitu kiuwazi,inakuelezea vzr namna gani umuabudu Mungu mmoja,namna gani uisha Hapa Duniani,lakini pia imeelezea vzr maisha baada ya kufa,kwamb Ukifuata ukiamini na kuufuata UISLAM kiukweli nini utapata baada ya kufa,hapa DINI inakueleza kinaga ubaga,yan Hapa huambiwi kimafumbo mafumbo Eti Ooh Utaenda mbinguni ukamuimbie bwana....uislam Hapa umeeleza vzr mnoo.
Pia ukifa kafiri yan umekufa hukuwa muislam kwamba ulifuata DINI zingne ambazo Sio mpango wa Mungu pia inakwambia nini utapata baada ya kufa.
Acha kufuata miluzi ya watu waliopotea na kukata tamaa,njoo Kwenye DINI yako ya asili ndugu.
 
Mwanzon nilikuwa nna mawazo kama yako.
Nkajua atheism iko nje ya hiyo nyumba, kumbe nayo ni chumba tu ndani ya hiyo nyumba.
Spirituality nacho ni chumba tu,
Scientology nacho ni chumba tu.

Kitu kilicho karibu na kutoka Kwenye hiko chumba ni Buddhism, tena particularly zen Buddhism
Sijafuatilia hiyo Zen Buddhism lakini nakuhakikishia ideology yeyote iliyopo hapa duniani ni wale wale.

Kwasababu hata bila ya hizo ideology (dini) mambo yanasonga tu kama kawaida, chochote utakachokigeukia na kujenga imani juu yake mambo yanajipa, uwezo upo nao ndani, ili udhihilike unahitaji nia juu ya kitu flani(chochote kile).

Hapa utangundua kuwa wewe ndio mwenye nguvu, wala sio kwasababu ya dini flani(Nguvu iko ndani yako).

Kitakachotofautiana ni matumizi (dhamira yako ni ipi njema au mbaya)
Unaielekeza wapi hiyo nguvu yako.
 
Duniani kuna Freedom of worship, chagua dini yeyote ambayo unaipenda.
Ila kama nia yako ni kuingia Mbinguni njia ni moja tu, YESU KRISTO. Vitabu vyote vimeandika habari za Mwokozi YESU KRISTO. Na huyu ndiye HAKIMU atakaye uhukumu ulimwengu.
Waulize swali hilo viongozi wako wa dini ni nani atakaye uhukumu ulimwengu?
Atakaye hukumu ndiye wa kumfwata. JINA LA YESU KRISTO LITUKUZWE.
 
Ukiangalia Kwa umakini utagundua watu wanasali/kuswali Ili wazikwe Kwa heshima ,Mungu haangalii dini anaangalia umeishije duniani(matendo).
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
Amka usiku kuanzia Saa Sita. Muombe Nwenyezi Mungu akupe ishara ya kile unacho kifikiria kama ni sahihi au si sahihi.
In Shaa Allah, Kwa uwezo wake atakuonyesha njia ilio nyooka.
 
Mkuu kuna watu hata sio waislam wana wake zaidi ya hao 4 na bado hawajihisi kuwa na hatia yoyote na labda nikwambie mm sijaoa na sina hata hilo wazo kwasasa.
Alaf kwanin wengi mnaangalia vitu vinavyo ahidiwa kwa wahisilamu kama ndo msukumo unaowafanya watu kuingia kwenye hiyo dini.

Kiufupi naaangalia sehemu salama ambayo naweza kuwa na malezi bora kwangu na kwa watoto na kizazi changu kijacho sababu dini nyingi zihalibiwa na huu utandawazi yaani dunia yasasa nikawaida kukuta watu wakilitumia kanisa kwa mambo ya hovyo.

Kwaiyo sina chochote ninachotegemea kupata kwenye iyo dini unayoisema zaidi ya kumjua mungu na kupata. maadili na malezi bora kwangu na kwa familia yangu ijayo
Kwa haya maelezo tu uisilamu unaoufikiria kwasasa kam kimbilio panakufaa. Uisilamu kwa asilimia kubwa unahusiana mema na kukatazana mabaya. Katika jamii familia yoyote yenye malezi ya kiislam na wameyashikilia na kuyafuata wanaheshimika kwa kiasi kikubwa mno.
 
Tatizo unataka kutumia LOGIC kwenye dini/imani. Logic na imani haviendi pamoja, chagua kimoja uende nacho.
Labda sisi binadamu tuna tabia ya kuukwepa ukweli.

Umeliwaza hilo
 
Habari wana jf leo ninaswala gumu linanitatiza naitaji maoni yenu.

Kama binadamu wengine namuamini mungu.

Ila napata wakati mugumu kuchagua dini ya kuabudia. Nikisema hivyo namaanisha mini ni mtu ambaye napenda kujifunza sana.

Na kijifunza kwanga kumefanya nibadili jinsi ninavyo itizama dini yangu iliyonelea (ukristo)

Nimekulia katika familia inayo abudua kupitia roman Catholic ila miaka mitano nyuma baada ya kujifunza na kuelewa vitu fulani mimi kama binadamu ninahaki ya kuchagua wapi nikaabudu ivyo nikaamua kubadili na kuwa katika makanisa ya kilokole.

Now nimwaka wa pili sasa huwa najiuliza kama uamuzi niliofanya ni sahihi make najikuta naitaji kubadili tena na safari hii naonelea zaidi kuwa mwisilam (dini ninayoipenda zaidi).

Kinacho nisukuma kufanya hivi sio nafata mkumbo hapana ila kunavitu vingi uwa vinanipa mwaswali na hayo maswali yakikosa majibu basi huwa naitaji kubadilisha msimamo wangu.

Nitaepuka kuweka maswali hayo hapa ili nisianzishe mjadala wa kinidi.

Kiukweli kabisa niko njia panda na ukizingatia naelewa pia sio rahisi kumwamini mungu kwa kuto shiriki katika dini yoyote maana utakosa malezi ya kidini japo wengine ufikili kuingia kwenye dini ni kama kujiingiza kwenye jela yako mwenyewe.

Ntashukulu kwa maoni yako mwana jf.
usichague dini, mchague Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Sijafuatilia hiyo Zen Buddhism lakini nakuhakikishia ideology yeyote iliyopo hapa duniani ni wale wale.

Kwasababu hata bila ya hizo ideology (dini) mambo yanasonga tu kama kawaida, chochote utakachokigeukia na kujenga imani juu yake mambo yanajipa, uwezo upo nao ndani, ili udhihilike unahitaji nia juu ya kitu flani(chochote kile).

Hapa utangundua kuwa wewe ndio mwenye nguvu, wala sio kwasababu ya dini flani(Nguvu iko ndani yako).

Kitakachotofautiana ni matumizi (dhamira yako ni ipi njema au mbaya)
Unaielekeza wapi hiyo nguvu yako.
Sasa haya maelezo uliyoweka hapa ndio zen Buddhism yenyewe.
Zen sio ideology.
Zen ni way of life.
Ambayo ukiifuatilia kiundani zaidi utagundua Kila mtu ni zen Buddhist.
 
Ukiangalia Kwa umakini utagundua watu wanasali/kuswali Ili wazikwe Kwa heshima ,Mungu haangalii dini anaangalia umeishije duniani(matendo).
Kweli na hayo matendo unayatenda katika msingi gani je unaiishi tuu unavyojua ww au kuna labda mwongozo uufate.
 
Kwa haya maelezo tu uisilamu unaoufikiria kwasasa kam kimbilio panakufaa. Uisilamu kwa asilimia kubwa unahusiana mema na kukatazana mabaya. Katika jamii familia yoyote yenye malezi ya kiislam na wameyashikilia na kuyafuata wanaheshimika kwa kiasi kikubwa mno.
Nakubaliana na hilo mkuu
 
Back
Top Bottom