Niko njia panda

Niko njia panda

Sawa Boss..

Mkuu FisadiKuu kwa ripoti za wanasaikolojia wewe ni mtu mwenye busara maana pamoja na kurushiwa maneno makali wewe unajibu kistaarabu. Big up ila next time waache watu na uhuru wao wa kuongea kwa lugha yoyote ile isipokua matusi tu!
 
Last edited by a moderator:
Retired mzima mie poa........hahahaha atasingizia alisinzia kwenye basi unajua mwendo mrefu iringa Dar.......kweli inakera unapomtafuta mtu yeye hana habari baadae analeta habari hazieleweki.

Poa dada, xmas wapi mwaka huu?

Haya mambo yanakera sana. Uzuri ni kwamba maisha baada ya hapo ni matamu sana.
 
Aise kwanza kweli kabisa awana bima wakiamua kitu hatauwabembeleze vip atakuja tu lakini a takuwa anamuwaza yule Yule kimsingi achana nae atakuletea magonjwa bule
 
Habarini za wekend wadau,

Naombeni mnisaidie kimawazo.umri wang ni miaka 24 ni muajiriwa serikalin huku Dodoma, wilaya ya Mpwapwa,lakini home ni Iringa nina girlfriend wangu ambaye yupo chuo cha RUCO kilichopo iringa, nmedumu naye takribani mwaka mmoja na nusu, ingawa tumepitia changamoto nyingi sana lakini tumeweza kudumu pamoja na hatimaye kusonga mbele.

Siku ya tar 17 alinipigia simu kunijulisha kuwa tarehe 18 ambapo ni siku ya ijumaa ana TEST,,hvo akimaliza hyo test ataangalia utaratibu wa kusafiri ingawa chuo kinafungwa tar 23, aliniambia kuwa atafanya hivo kwa sababu hakutakuwa na mishe yoyote, hivo akiendelea kubaki hapo ataboreka.

Mimi nikaridhia, siku ya jana jioni akanijuza kuwa kesho ambapo ni leo kuwa atasafiri kama alivonijuza mwanzoni na aliniambia kuwa ataondoka na gari ya sa 12, akaniambia kuwa anaenda Dar es salaam kusalimia ndugu ila kwao ni MOSHI mimi nikaridhia, nikamtakia safari njema mida ya saa nne tulifanikiwa kuongea zaidi na kutakiana usiku mwema. PICHA NDO IKAANZA KULIVO KUCHA.

Nlipanga niwah kumuamsha ili awahi hyo gar ya sa 12,lakini nkajikuta nmepitiwa na usingizi.nmekuja kuamka baada ya sa 12 asubuh,ambapo nlishangaa kutokukuta sms wala call ya kunijulisha kama kaondoka ama la.nliamua kumtumia text, kumuomba samahan nanukuu SAMAHANI NMECHELEWA KUAMKA, NLIPITIWA NA USINGIZI HVO KUSHNDWA KUKUAMSHA KWA WAKATI ILI UWAHI GAR, ikapokelewa lakini haikujibiwa nikaamua nitume tena text ya kumtakia safari njema, nayo ikapokelewa lakini haikujibiwa nkaendelea kuvuta subira mpaka mida ya sa tano,lakini bado alikuwa kimya.

Nikaamua nimpigie simu, nimejaribu kama mara 20 kwa kutumia namba yangu ya voda, naambiwa namba busy nikahisi kuwa AMENIBLOCK lakini nikapuuza hilo wazo,nikaamua nitumie tena namba yangu ya Tigo lakini nlipata matokeo yaleyale nliamua kujipa moyo na kuamini kuwa wenda anaongea na simu nyingine nikawa natuma tu sms zinaonyesha deliverd lakini hazijibiwi.

Nimekaa saa moja na nusu nimemtafuta tena lakini matokeo ni yaleyale nikaamua kuingia WHATSAPP nikaangalia namba yake anayotumia humo wasap ambapo mara ya kwanza ilikuwa inaonyesha last seen,status pamoja na profile picture lakini vyote hivo havionekani saivi nikawa bado siamini kuwa AMENIBLOCK ghafla likanijia wazo,la kutaka kufanya confirmation,binafsi wasap natumia namba ya tigo sijawahi badili namba na yeye anafahamu hivo, niliamua kwenda kwenye account yangu ya wasap na kubadili namba, nikaweka namba ya voda halafu nikarefresh nikarudi tena kuangalia ileile namba yake anayotumia wasap maajabu ndugu zangu, nikakuta profile picture ipo kama kawaida na last seen inaonyesha ni saa nane na dkka 50 mchana huu hakika nmejikuta natetemeka,na sijataka kuliamin hili tukio nmekuja kuhakiki kuwa hata namba yangu ya wasap ameiblock pia.

Nisaidieni kimawazo ndugu zanguni, nifanye nini maana kiukweli nashndwa kuamin sijagombana naye zaidi ya changamoto za kawaida katika mahusiano pia sijaelewa kama kasafiri ama laa.

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE


mwache akuache kwa mbwembwe..... we piga kimya tuu atarud analia mwenyew tuu.... hzo ndo tabia za wasichana wa chuo
 
Back
Top Bottom