Duh umenikumbusha miezi kama nane iliyopita, mwenzio niliblokiwa kuanzia instagram, facebook,na kote unakokujua ila nilipiga moyo konde nikamove on na yeye anaenjoy maisha na mtu wake, huku akiniacha njia panda bila ya kujua la kufanya
Naomba Mungu anivushe salama mwaka huu,ila nikushauri kitu
Kumuacha mwanamke unayempenda ni ngumu kuliko kitu chochote hapa dunian yani ni rahisi zaidi ya jakaya kuamia ukawa kwa sasa, ila inaitaji courage kufanya hivyo na itafika muda utasahau tu
Pole sana mkuu BILGERT kwa yaliyokufika ila naomba usihuzunike sana na kusikitika. If it wasnt meant to be it wasnt meant to be. Mshukuru Mungu kwa kukufunukia na kukuonyesha tabia halisi ya mwanamke uliye naye. Huwezi jua pengine angeweza kukufanyia makubwa zaidi huko mbele ya safari endapo mngeendelea na uhusiano wenu ambayo yangeuumiza sana moyo wako.
Najua jinsi gani na unaumia kutokana na uliyofanyiwa na uliyempenda, lakini maumivu yote hayo yatakwisha tu kadiri siku zinavyozidi kwenda maana hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Kidonda ulicho nacho kitapona haraka endapo utajitahidi kukitibia ili kipone. Kumkosa huyo mwanamke sio mwisho wa maisha yako kwani yupo mwanamke bora kwa ajili yako ambaye Mungu alikuandalia tangu kuumbwa kwako, she is out there looking for you. So usikate tamaa cuz ukikata tamaa utamkosa huyo mwanamke ambaye Mungu ameakuandalia. Piga moyo konde kaka, inuka, pull up your socks and move on with your life.
Wewe kwa sasa mwachilie atakapokuja na sababu zake mpe ukweli wa moyoni,hapa hata tukikupa ushauri gani lakini wewe ndie muamuzi wa mwisho. kuna mshkaji wangu namkumbuka tulikuwa tunampa ushauri mwisho wa siku humwambia demu wake ushauri wote tuliompa, na demu wake anatuona kama wanga wake. Nakupa ushauri huu ikiwa umemkuta kishafanya sex(hayupo bikira) basi usiwe na wivu. Aliejenga nyumba ni mtu mmoja ila wakaazi ni wengi. nategemea umenifahamu
shukrani kwa ushauri mkuu....nmekusoma.ila inauma saana
Nakushukuru sana Mkuu kwa ushauri wako Murua,Mungu akubariki sana.hakika,ntaufanyia kazi huu ushauri,na nina amini utanisaidia
Boom lenyewe la mawazo akae na kiboifrend afe njaa, we unamuamsha alfajiri akapande sijui sabena teh tulia bana mtoto yupo ndani ya private car, kavaa kigauni kifupi, anakula kiyoyozi dereva anachange gia huku mkono pajani....maisha ni matamu haki a mama