Habarin za jioni wana MMU.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,nina kazi ambayo inaniingizia kipato changu kinachonikimu ktk maisha nipo kwenye mahusiano na binti mmoja kwa takribani mwaka mmoja sasa, ambaye pia ana kipato chake kizuri tu,tumekuwa tukisaidiana katika shida na raha, wiki moja iliyopita huyu binti, aliniambia kuwa amepatwa na shida ambayo inagharimu kiasi cha shiling laki nne na akaniahidi atanirudishia mwezi wa kwanza, hivo akaomba nimuazime.
Huyu binti namshirikisha kwenye mambo mengi sana, ikumbukwe nilishawahi kumshirikisha malengo yangu,na pia nikamjulisha kiaisi ambacho kinahitajika ili hayo malengo yaweze kutimia na pia isitoshe nikawa nmemjulisha kiasi ambacho nimefanikiwa kukikusanya na kukihifadhi katika account yangu ya akiba.Maana nlipanga kufikia 2016 mwezi wa 7 niweze kuanza kutekeleza hayo malengo yangu,vyote hvo nilimshirikisha.
Hivo alivyonifuata kuomba nimuazime hyo hela alijua kabisa siwezi kumnyima kiukweli kutoka moyoni sikupanga kabisa kuigusa hyo hela maana nafahamu madhara yake,nlikuwa nathubutu hata kujinyima mwenyewe kipindi nmekosa hela, niko tayari nitafute hela sehemu nyingine ili mrad tu saving account yang ibaki salama.
Baada ya yeye kuniahidi kuwa hyo hela itarudi mwezi wa kwanza kama ilivyo nkawa nmeamua kumkabidhi hyo laki nne.Juzi kati tar 20 siku ya ijumaa ya mwezi huu tukiwa tunachat akaniambia kuwa anashukuru kwa kumkabidhi hiyo pesa, mimi nkamuambia asijali ila nkamuomba anirudishie hyo pesa mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.Hapo ndo ugomvi ulipoanzia, akaniambia kuwa mimi sina utu wala ubinadamu na nina roho ya kinyama,maana haiwezekani nimuazimishe pesa hata wiki mbili hazijapita naanza kumdai hivi wadau iko sawa kweli hii? Akawa amekasirika sana, siku ya jana usiku akanipigia tena akaongea tena maneno yaleyale kwa hasira sana, akasema kuwa amemuomba mtu amuazime hela ili anirudishie na hatothubutu tena kuniomba ama kuazma chochote kutoka kwangu.
Nimejaribu kumuomba sana na kumsihi kuwa mimi sikumaanisha anipe saivi ila nichosema ni kwamba anipe mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.anasema kuwa lazima anirudishie ndani ya wiki hii maana mtu aliye muomba hawezi kumzuia asitume kwa madai ya kuwa anaogopa siku atakapo muomba tena ataonekana anamtania nipo njia kuu wadau yaani sijui nifanyaje,je nmemkosea nini? Maana tangu hiyo jana usiku hatujaongea wala hajanitafuta mpaka saivi simu hapokei, najiuliza je,ana mpango gani na mimi? Mbona ananifanyia vitimbwi vya ajabu hvi? Pia nafikia mahali najuta kumshirikisha huyu mtu mambo yangu,wenda asingefahamu nina kias gani cha pesa pia najiuliza kwa hayo yanayotokea nini hatima yake?
Samahani kwa thread ndefu wadau ila nna huzuni sana, maana sijui hatima ya huu uhusiano na pia sijui hatima ya pesa yangu maana simu hapokei, naomba mnishauri ndugu zangu, maana naiona dunia chungu.
Natanguliza shukurani kwenu nyote