Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Himidini wala silazimishi ndoa, soma uzi wangu vizuri. Ndoa nilishaipata. Nilikaa 8 years kwenye ndoa. Raha na karaha za ndoa nazijua hivyo sina cha kulazimisha mpendwa wangu. All I need is a company lakini si dizaini ya Mariooo (kula kulala) kama wewe...

Hakyamungu, sasa wewe hujajuwa huyo uliyenaye pia ni Marioo kula kulala?

Hivi tuwe wakweli kama upo over 40 unadhani is possible kumpata single Man?

Wakandie hao Marioo lakini fainal utarudi kwao ili wakupige mikito ya uhakika, tena umri wako ndio wa nyege zinazohitaji mtu wa kuacha kazi afanye kazi.

Mwanaume presentable mwenye cash yake wa umri huo anataka vibinti vibichi kama Smile na lara 1
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mdada above 40 niliolewa nikaachana na mwenzangu some years ago. Kwa vile nilikua busy kusomesha watoto zangu watatu ambao sasa wameweza kujitegemea, sikutaka kua na uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote maana elimu ya watoto wangu na kuwasimamia was my priority.

The time has now come that I need a companion wa kumalizia nae hii n’ngwe ya maisha niliyobakiza kuliko kua mwenyewe. Watoto pia wameshasambaratika kuhangaika na maisha. Wawili wako nje ya nchi wanafanya masters na mmoja ambaye ndio mkubwa ameshaolewa ana degree ya BSc electronics aliyopata UDSM.

Nimekutana na kaka mmoja above 40 nae japo nimemzidi 3 years, hii hainipi tatizo kwani umri kwangu sio shida, most important kwangu is how we feel for each other. Nae aliwahi kuoa akazaa watoto wanne lakini pia akaachana na mkewe. Mtoto mmoja katika hao wanne alizaa wakati wa ujana na mwanamke mwingine ambaye hawakubahatika kuoana. Aliyemuoa ndio walizaa watoto watatu.
Ni miezi kama 5 – 6 hivi tangu nifahimiane na huyu kaka. Sote ni waajiriwa japo mimi kipato changu kinamzidi mwenzangu. Hili pia si tatizo kwangu, kama nilivyosema mwanzo najali tunavyojisikia tukiwa pamoja.

Tatizo kubwa ni kwamba, huyu bwana amekua kama limbukeni wa mapenzi tangu tufahamiane. Kama ni kupendwa kwa style hii mwenzenu nahisi nashindwa. Amekua king’ang’anizi kupita maelezo na wakati mwingine kulazimisha yasioyowezekana.

Analazimisha anataka kuhamia kwangu na atanioa. Sio tatizo kwangu lakini kwa maisha niliyoishi for years nikiwa mwenyewe sio kitu naweza kuamua in a night. Hataki kuelewa kwa namna yoyote ile. Juzi juzi hapa tulikwaruzana, actually niliamua kuachana nae kabisa! Lakini alinipa vitisho sana, kwamba siwezi kumuacha na hayuko tayari kuniacha hata iweje. Mpaka alitaka kuja kuleta fujo nyumbani baada ya kumwambia sitafungua gate akija.

Naomba mfahamu kwamba huyu anayejifanya ananipenda kupita kiasi, hana msaada hata mmoja katika maisha yangu. Nahangaika na maisha yangu mwenyewe kama nilivyozoea, ninachokula au ninachovaa nakijua mimi. Yeye kutwa ni kujitetea kua kipato chake ni kidogo kuliko cha kwangu japo sioni kama ni kigezo cha kutotoa msaada kama baba mtarajiwa. Sihitaji msaada 100%, hata 20% kwangu nitashukuru maana sijashindwa kuendesha maisha yangu. Ila msaada wake kidogo kwangu will mean so much ili kudumisha uhusiano wetu. Sasa hivi nina wasiwasi maana ananisumbua kupita kiasi kua lazima tuishi pamoja. Siwezi kuamua hili mara moja hasa kutokana na maisha niliyoishi ya muda mrefu nikiwa mwenyewe na pia nina watoto, I have to make them understand, na siwezi kuwafanya waelewe kwa mara moja. Watoto ni wakubwa na wana akili hivyo ni lazima niwapeleke polepole waelewe kua nili sacrifice my love life kwa sababu yao na sasa nahitaji mwenza. Sijui watalielewaje hili maana ni process. Hapa napo mkinishauri jinsi ya kulileta kwa watoto nitashukuru, maana naamini hapa jamvini wapo waliopitia mtihani kama huu.

Kikubwa ambacho ndio mtachoka, mtu huyu mwenye mapenzi mazito kwangu, sijui anaishi wapi..... japo yeye anajua kwangu na watoto wangu wawili anawafahamu. Huyo mmoja anayeishi nje ya nchi alikuja likizo wakaonana alipokuja nyumbani. Wanamjua as Mama’s friend, japo nahisi vile ni wakubwa they might have smelt something, japo hainipi shida maana mwisho wa siku its my happiness. Simfahamu mtoto wake hata mmoja maana anasema watoto wake hawawezi ku support yeye kua kwenye mahusiano, sina hakika na hili, sasa sijui akiamua kutelekeza watoto watatu ambao anaishi nao itakuaje, maana mmoja huyo mdogo anaishi na mama yao, nashindwa kupata hesabu inayojumlishika kwa hili. Niko katika harakati za kumalizia nyumba yangu nje ya mji ambayo nahamia soon, ana insist kua tuhamie pamoja, nisiende kuishi mwenyewe maana ni sehemu ya ugenini na nyumba ni kubwa. He’s got a point in a way, lakini haiwezi kua rahisi kiasi hiki anavyofikiria yeye. Kwangu mimi bado niko njia panda. Pia hatujawahi kujadili kua anakuja kuishi na mimi kwa namtiki gani na watoto wake atawaacha wapi. Vile ni kitu ambacho sijakiunga mkono 100% hata nguvu ya kuuliza haya sijawa nayo.

Naomba ushauri wenu wapendwa, hivi unaweza kweli kumpenda mtu kwa moyo wako wote, lakini mwenzio asijue unakoishi zaidi ya kazini kwako na usitoe msaada hata mmoja kwake, ilhali ukienda kwake unataka ukarimiwe kwa chakula na mapenzi? Hii mimi hainiingii akilini.

Tulipokwaruzana juzi niligundua nilifanya makosa kumfanya awe free nyumbani kwangu, as he used to come any time. Japo alikua anaingia chumbani kwangu only kama tuko wawili tu ndani ya nyumba, maana nina msichana wa kazi ambaye weekends mara nyingi anaenda kwao kusalimia na binti wa mdogo wangu ambaye namsomesha. Naye pia weekends anaenda kwa mama yake. Baada ya kugundua hilo kosa na mkwaruzano uliokuwepo, nilimwambia kuanzia sasa hatakuja tena nyumbani kwangu. Tutaonana nje ya nyumbani kwangu, in a hotel, for drinks, dinner etc... lakini kwangu sio sasa mpaka niweke mambo sawa na watoto. Hili tunalumbana nalo kwa karibu wiki mbili sasa hataki kunielewa. Anadai yuko more comfortable kama tutaonana nyumbani kwangu. Mimi nahisi anapenda kuja kwangu kwa vile he gets everything for free. Samahani kama nitawakwaza wanaume lakini ndivyo nidhaniavyo, maybe am wrong, mtaniambia. Tangu kumetokea kutoelewana hajaja tena nyumbani maana nimekataa kata kata ila tunaongea kwenye simu na kubishana ndio kwingi zaidi maana hataki kunielewa. Naomba mnijuze kama nina kosa hapa.

Niliamua kumueleza kua, kama yeye ameona haiwezekani mimi kujua kwake na kufahamu watoto wake vile anawaheshimu, kwanini mimi pia hataki ku consider hili? Kama ni makosa nilishayafanya, na nimegundua, sitaki kurudia tena! Hataki kuelewa, maana ameshikilia kwa vile mimi nina kipato namnyanyasa vile hana uwezo wa kulipia hotels, drinks and maybe meals if we decide to sit somewhere kuongea.

Kwa kweli sijui nielezeje maana mimi sio mwandishi mzuri but niko njia panda! Nawagetemea nyinyi mnipe ushauri maana huyu baba si muelewa. Kutwa anajitetea kua mimi namnyanyasa kwa vile hana kipato kizuri kama mimi. Ni mtu wa kulalamika kutwa hana pesa! Kwa kweli nachoka maana hata mimi nina shida zangu na majukumu ya ndugu lakini silalamiki kwa mtu yoyote kuhusu matatizo yangu, sana sana natafuta ufumbuzi mwenyewe. Mwanamme mzima kutwa kulalamika hana pesa kwa mwanamke, mimi sioni kama ni sawa.

Naomba msinihukumu kwa lolote, ninachotaka ni msaada wa ushauri maana nimekamatwa na huyu baba ambaye nashindwa kujua ananitafuta nini kusema kweli na nitamtoka vipi maana hataki kusikia kitu kinaitwa kuachana.

Samahani pia kwa kuwachosha, mimi sio mwandishi mzuri hivyo uandishi wangu ni wa kuzunguka zunguka ila naamini mtanielewa.

Kwa kuangalia story na accomplisments zako inaonyesha una life style ambayo kila kijana wa mjini mvivu anaitaka sasa bas ni vigumu sana kwa ww kukutana na wenye mapenzi ya kweli mie nadhani tafuta kibabu kimoja ambacho na chenyewe kimeridhika kiwe kinakupa company kipindi ambacho unahitaji na kama unataka ukimiliki basi uhamie kwake! Vinginevyo haya unayoyakataa yatakuwa mengi na pengine ukaibiwa na kuletewa magonjwa!
By the way pole ila kwa nn usivumilie kama ulivyovumilia wakati unalea wanao!
 
Da Asia pole naona uko tena njia panda kwa mara ya pili.

Huyu anayelazimishia kuhamia kwako ni John au Peter?

Nakumbuka John alikuwa yuko sawa lakini hamkuwa "compatible".

Pia nakukumbuka Peter alikuwa mtu wa mission town lakini mlikuwa "compatible".

Sasa hebu "clarify" hapa ili tujue kama "what went round came back".
 
Hakyamungu, sasa wewe hujajuwa huyo uliyenaye pia ni Marioo kula kulala?

Hivi tuwe wakweli kama upo over 40 unadhani is possible kumpata single Man?

Wakandie hao Marioo lakini fainal utarudi kwao ili wakupige mikito ya uhakika, tena umri wako ndio wa nyege zinazohitaji mtu wa kuacha kazi afanye kazi.

Mwanaume presentable mwenye cash yake wa umri huo anataka vibinti vibichi kama Smile na lara 1
mi mbichi eeeh ? nichukue basi
 
hebu kuwa mtu mzima kama umri wako! Kama unaamua kusimamia kitu amua moja kwa moja si kuatafuta sababu et watoto,cjui nyumbani kwangu,cjui cfahamu anapoishi! whaaaat? Kwanza nimejaribu kusoma post yako cjaona neno kuwa unampenda! kama humpendi mtu lazima utamtafutia tu misababu kibaoooo! umeona hakufai potezea
 
EMT, sio lazima kila story iletwayo hapa iwe ni yako, unaweza ku personalise story lakini ki ukweli ni kwa niaba ya mtu.

Da Asia pole naona uko tena njia panda kwa mara ya pili.

Huyu anayelazimishia kuhamia kwako ni John au Peter?

Nakumbuka John alikuwa yuko sawa lakini hamkuwa "compatible".

Pia nakukumbuka Peter alikuwa mtu wa mission town lakini mlikuwa "compatible".

Sasa hebu "clarify" hapa ili tujue kama "what went round came back".
 
Inshaa Allah, Ameen....

Kwanza napenda nikupongeze dada yangu ni wanawake wachache sana wenye ujasiri na uthubutu kama wa kwako kwa kuweza kuwasimamia wanao despite of da rough road!Big up indeed!

Kuhusu huyo mwanaume achana nae ucje ukajutia muda wako mwingi ulio spent mwenyewe na wanao!Wengine huwa ni waharibifu in nature!Keep distance na atambue msimamo wako!
Ukiona vitusho vyake vinazidi mreport polisi mapema!
M
Allah akufanyie wepec In shaa Allah!
 
EMT, sio lazima kila story iletwayo hapa iwe ni yako, unaweza ku personalise story lakini ki ukweli ni kwa niaba ya mtu.

It would have been much better kama ungesema from the very beginning kuwa the story is hypothetical au ni ya mtu mwingine.

Kwa sababu ni useless kumpa mtu ushauri in an hypothetical case wakati kuna watu wana real cases na wanatafuta ushauri lakini hawaupati kwa kudhaniwa kuwa stories zao ni za kutengeneza.

Kama story ni kwa niaba ya mtu there was no need to personalise it. Maana siku yakikukuta na wewe sijui nani ata-personalise story yako.

Sometimes, we need to get real.
 
Kaka siku hz umekuwa harsh my dear sijui una nini story lakini
 
pole sana mama yangu, huyo siyo mkweli na usipokuwa makini atakuingiza katika matatizo makubwa, inawezekana kabisa anayofamilia na mke na ndiyo maana pesa haionekani, anakung'ang'ania sana kwa sababu alishagundua kwako anaweza kupata chochote, ni kweli kabisa wasiwasi wako kuwa anatakakuja kwako kwasababu ya huduma ya chakula na mengineyo maana hayupo tayari umtie gharama yoyote hotelini siyo matarajio yake "yeye ni mvunaji" mwanaume anayependa kweli angekusumbua kama ungemnyima penzi tu, mengine angeyaona ni ziada kama uaminifu siyo shida, kwanini hata hicho kidogo alichonacho huwa hakionekani ana mke na si mmoja .Hataki ujue kwake, akipatwa na matatizo akiwa kwako utakwenda wapi? utaishia korokoroni mama yangu. Anataka kuhalaisha uhusiano wenu ili hataakikudhuru abahatishe baadhi ya mali zako. TAKE CARE.
 
Jamaa ameshapigwa chini
 
Umemkawiza sana........fukuzia kule mwanaume marioo huyo.........huyo ana mke na watoto anaishi nao vizuri tu........wanaume wengine kwa kupenda bwerere mpaka wanakera.........Stuka maa.......haina haja ya kununua likitimoto lote kwa ajili ya sausage........kuna sausages brand nyingi sana madukani........kila aina wewe tu kuamua utakula ipi......

Hahahahahahahahah,

Huyo jamaa ni zaidi ya "chuma ulete"

Akimwendekeza mshikaji atabeba hata hati ya nyumba na kadi za magari......

Chezea wanaume kama mabinti....

Babu DC!!
 
Kwanza chunguza kama anamiliki bastola (te te te)

Pili huyo si mume ni gume gume; kama hana mke basi ana wanawake wengine wengi ndio maana amechagua nyumba yako kama maficho salama kwake.
 
@DaAsia
kwanza nikupe hongera kwa hatua uliyofikia katika malezi ya wano ukiwa peke yako.

Ishu yako ya mahusiano.. sidhani kama huyo mwanaume anakupenda kama unavyoeleza. Na m_dought sana; bado anaficha mambo mengi sana kwako kitu kinachotia mashaka. Nahisi ana malengo fulani (''''''), just be very carefull, kama unajisikia unampenda sana, weka mipaka na jipe muda wa kutosha kumsoma na kumwelewa. Hili ni pamoja na kuweka misingi/makubaliano thabiti ya jinsi gani mahusiano yenu yatakavyokuwa, nani atahamia kwa mwenzie, watoto itakuwaje n.k

"Kutwa anajitetea kua mimi namnyanyasa kwa vile hana kipato kizuri kama mimi. Ni mtu wa kulalamika kutwa hana pesa!" hii kitu hii ni hatari sana.

Mwanaume akijisikia dhaifu ni dhaifu kweli kweli ..magomvi na matatizo yasioisha huibuka kutokana na inferiority.

He can ruin ya life totally na ukajuta. Mie ndukiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kwanza chunguza kama anamiliki bastola (te te te)

Pili huyo si mume ni gume gume; kama hana mke basi ana wanawake wengine wengi ndio maana amechagua nyumba yako kama maficho salama kwake.

Ila kweli dada zangu kazi mnayo,

Unawezaje kumpa mtu kama huyo hazina zako zote bila kustuka??

Babu DC!!
 
Kwanza chunguza kama anamiliki bastola (te te te)

Pili huyo si mume ni gume gume; kama hana mke basi ana wanawake wengine wengi ndio maana amechagua nyumba yako kama maficho salama kwake.

Ahaaa anamfanya nyumba kubwa
 
Back
Top Bottom