Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Ndoa siku hizi zimekuwa kama Serikali, zimekuwa na taasisi za usalama wa Ndoa, taasisi ya usalama ya ndoa yako ikiwa legelege kama TISS lazima mkeo agegedwe.

mama yangu weeee,wewe umesema TISS uogopi kupelekwa msitu wa pande chachachacha!
 
Last edited by a moderator:
Kulikuwa na simulizi fulani ya Mkata mti mmoja ambaye alipokuwa anakata mti,pembeni palikuwepo na kijana aliyekuwa amelala.Yule mkata mti akamwambia yule kijana 'ondoka hapo utaangukiwa mti' Yule kijana alibisha akasema 'niko macho,naona vizuri hauwezi kuniangukia' Lakini mwisho wa simulizi hiyo,Mti ulimwangukia na akafa pale pale.
....
Nimekumbuka usemi huo baada ya jirani yangu kumuona ameanza ulevi ghafla,kawa mkali kwa mkewe kuliko tulivyomzoea! Juma lililopita nikiwa natoka kwenye kusaka riziki, akaniona na kusema nimpe pesa kidogo akashitue..Nikampa Mnamo usiku wa saa mbili akaja kwangu akiwa pombe imemkaa vema na kunisimulia mengi ambayo hakika yanaumiza
....
Pale kwake alimleta kijana mmoja wa kuhudumia mifugo yake,Kijana huyo alipofika katika familia hiyo akaanza mazoea na mama mwenye mji,ambayo hayakuwa mazuri kimaadili.Hata hivyo kijana huyo ambaye ni 'Handsome' kama wasemavyo vijana wa mjini,alijifanya mtii
....
Watu hawana dogo walianza kumtonya mwenye nyumba kuwa mazoea yale si mazuri lakini akawajibu anamwamini mkewe na alikuwa makini kuwa hakuna litakalotokea
....
Baada ya muda amebaini mama wa ile nyumba ana ujauzito.Akamuuliza mkewe akakiri.Mumewe akabaki anajiuliza ilikuwaje kwani walipanga kutopata mtoto mwingine ili wapate nafasi ya kulea watoto wao wawili ! Mwanamke anabaki analia.Kibaya zaidi yule kijana amekimbia hajulikani alipo pasipo kugombezwa au kuaga.Mambo yote hayo yanamjengea picha kuwa tayari ile mimba si yake
.....
Jirani rafiki huyu anajilaumu sana ni kwa nini alipuuza aliyoambiwa? Ni heri angewasikiliza.Nimemshauri asubiri matokeo.
Hapa ndipo nilipojua kweli,ukiambiwa na watu wengi juu ya jambo moja linalofanana kuhusu mpenzi wako au kazini kwako,,Chunguza Si kila mmoja hakupendi au anakutakia mabaya.Using'ang'anie tu 'Niko Macho Niko Macho' utaangukiwa mti.
^^

wanawake wanautumia vizuri udhaifu wao.
 
Kuna wauza nyanya,mangi wa dukani,mzaire wa salon,dereva wa boda boda,konda,mzoa taka the list goes on.
Akiamua kugawa atagawa tu

Bora agawe kwa hao wapita njia... Sio anakula na kujisaidia kwangu...
 
daah, mizunguko mingine!!! heri ya lile la riziki likufikie kuliko hili la usaliti, utaona umeibebea dunia,
 
Nakuunga mkono ila ni kuwa makini kwenye kuchuja ya ukweli na yasiyo ya ukweli.
Sina last long life lolly my firstly mliman million in a llmwllqll and more likely that you llmwllqll lqmlwlwlllmwllm llmwllql and thlwlw
 
Jirani rafiki huyu anajilaumu sana ni kwa nini alipuuza aliyoambiwa? Ni heri angewasikiliza.
Hapa ndipo nilipojua kweli,ukiambiwa na watu wengi juu ya jambo moja linalofanana kuhusu mpenzi wako au kazini kwako^^

'Mtu mmoja akikwambia jambo ana matatizo.., wawili,watatu au zaidi wakikufuata kukwambia jambo ujue una matatizo' - Askofu Basonga
 
Huyo mwanamke bado yupo hai? na huyo jamaa yupo uraiani au jela?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom