Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
Kulikuwa na simulizi fulani ya Mkata mti mmoja ambaye alipokuwa anakata mti,pembeni palikuwepo na kijana aliyekuwa amelala.Yule mkata mti akamwambia yule kijana 'ondoka hapo utaangukiwa mti' Yule kijana alibisha akasema 'niko macho,naona vizuri hauwezi kuniangukia' Lakini mwisho wa simulizi hiyo,Mti ulimwangukia na akafa pale pale.
....
Nimekumbuka usemi huo baada ya jirani yangu kumuona ameanza ulevi ghafla,kawa mkali kwa mkewe kuliko tulivyomzoea! Juma lililopita nikiwa natoka kwenye kusaka riziki, akaniona na kusema nimpe pesa kidogo akashitue..Nikampa Mnamo usiku wa saa mbili akaja kwangu akiwa pombe imemkaa vema na kunisimulia mengi ambayo hakika yanaumiza
....
Pale kwake alimleta kijana mmoja wa kuhudumia mifugo yake,Kijana huyo alipofika katika familia hiyo akaanza mazoea na mama mwenye mji,ambayo hayakuwa mazuri kimaadili.Hata hivyo kijana huyo ambaye ni 'Handsome' kama wasemavyo vijana wa mjini,alijifanya mtii
....
Watu hawana dogo walianza kumtonya mwenye nyumba kuwa mazoea yale si mazuri lakini akawajibu anamwamini mkewe na alikuwa makini kuwa hakuna litakalotokea
....
Baada ya muda amebaini mama wa ile nyumba ana ujauzito.Akamuuliza mkewe akakiri.Mumewe akabaki anajiuliza ilikuwaje kwani walipanga kutopata mtoto mwingine ili wapate nafasi ya kulea watoto wao wawili ! Mwanamke anabaki analia.Kibaya zaidi yule kijana amekimbia hajulikani alipo pasipo kugombezwa au kuaga.Mambo yote hayo yanamjengea picha kuwa tayari ile mimba si yake
.....
Jirani rafiki huyu anajilaumu sana ni kwa nini alipuuza aliyoambiwa? Ni heri angewasikiliza.Nimemshauri asubiri matokeo.
Hapa ndipo nilipojua kweli,ukiambiwa na watu wengi juu ya jambo moja linalofanana kuhusu mpenzi wako au kazini kwako,,Chunguza Si kila mmoja hakupendi au anakutakia mabaya.Using'ang'anie tu 'Niko Macho Niko Macho' utaangukiwa mti.
^^
 
Ndoa siku hizi zimekuwa kama Serikali, zimekuwa na taasisi za usalama wa Ndoa, taasisi ya usalama ya ndoa yako ikiwa legelege kama TISS lazima mkeo agegedwe.
 
Mh! Kweli mwaya!! Lakini maneno ya watu sometimes yanavunja ndoa za watu sana ni vema kupata muda wa kuchunguza.yaelekea jamaa aliambiwa lakini hakutaka kuchunguza at the end ndo hvyo tena..wakat mwngne siye wanawake sijui tupewe nini?? Kulea mtoto si wako yataka moyo!!
 
Ndoa siku hizi zimekuwa kama Serikali, zimekuwa na taasisi za usalama wa Ndoa, taasisi ya usalama ya ndoa yako ikiwa legelege kama TISS lazima mkeo agegedwe.

hivi mkeo hadi agegedwe nje ni kwamba mume ameshndwa majukumu yake ama vipi? Sijawah kuelewa.
 
hili nalo ni neno ,,,,,,

japo uchunguzi zaidi wahitajika kuupata ukweli , ila kama mambo yenyewe ni ya kinga ni bora kuliko tiba ni bora ufanye maamuzi mapema.
 
na akimfukuza kesho utasikia jamaa ameshikiwa bango na sijui TGNP, sijui LHRC kwa kosa la kumtelekeza mkewe akiwa mjamzito! kweli wanaume tuna kazi aisee!!
 
Adhabu aliyopata huyo mwanaume sio sawa yake!!
Haya mambo tuyaache tu kwa style hiyo Bado mnanishauri KUOA?
Ngoja nizeeke zeeke kwanza
 
Mh! Kweli mwaya!! Lakini maneno ya watu sometimes yanavunja ndoa za watu sana ni vema kupata muda wa kuchunguza.yaelekea jamaa aliambiwa lakini hakutaka kuchunguza at the end ndo hvyo tena..wakat mwngne siye wanawake sijui tupewe nini?? Kulea mtoto si wako yataka moyo!!
Utaleaje mamy?where do you get the guts?labda ulogwe
 
Halafu ndo maana nyie wenye familia mkiambiwa na wake zenu tutoe hii mimba mume wangu...usimbishie utalea mtoto sio wako!!
 
Huyo mume kiwango kimeshuka nini?,na pengine wife ndo kasisitiza anataka houseboy na siyo housegirl,ili asaidie majukumu,vidume tutunze viwango tusije pelekwa timu zingize kwa mkopo.
 
Halafu ndo maana nyie wenye familia mkiambiwa na wake zenu tutoe hii mimba mume wangu...usimbishie utalea mtoto sio wako!!


Teh teh wanawake wasikie tu ila ndilo jukumu lililotuleta duniani,kuishi nao
 
Huyo mume kiwango kimeshuka nini?,na pengine wife ndo kasisitiza anataka houseboy na siyo housegirl,ili asaidie majukumu,vidume tutunze viwango tusije pelekwa timu zingize kwa mkopo.

Lolote laweza kuwa sahihi
 
Ndoa siku hizi zimekuwa kama Serikali, zimekuwa na taasisi za usalama wa Ndoa, taasisi ya usalama ya ndoa yako ikiwa legelege kama TISS lazima mkeo agegedwe.

Kweli kabisa inabidi ukiona jambo kama hulielewi unda tume mapema kabla mambo hayajaenda mrama .
 
na akimfukuza kesho utasikia jamaa ameshikiwa bango na sijui TGNP, sijui LHRC kwa kosa la kumtelekeza mkewe akiwa mjamzito! kweli wanaume tuna kazi aisee!!

Hakuna nisiowapenda kama hizo taasisi.
 
Ndoa nyingi zina matatizo, utawaona wanandoa wakitabasamu nje lakini ndani wana majeraha.
 
a word is enough for the wise! aache pombe kwani hilo ni suluhisho la muda mfupi. adumishe upendo kwa mkewe ili mkewe aumie zaidi. forgiveness is the best revenge.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom