Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Niko Macho,, Niko Macho...aliangukiwa na mti !!

Mh! Kweli mwaya!! Lakini maneno ya watu sometimes yanavunja ndoa za watu sana ni vema kupata muda wa kuchunguza.yaelekea jamaa aliambiwa lakini hakutaka kuchunguza at the end ndo hvyo tena..wakat mwngne siye wanawake sijui tupewe nini?? Kulea mtoto si wako yataka moyo!!

Mi sitafuga ng'ombe kwangu...
 
Huyo mume kiwango kimeshuka nini?,na pengine wife ndo kasisitiza anataka houseboy na siyo housegirl,ili asaidie majukumu,vidume tutunze viwango tusije pelekwa timu zingize kwa mkopo.

Hapa kuna umuhimu wa ile kitu inaitwa brantachi...
 
Adhabu aliyopata huyo mwanaume sio sawa yake!!
Haya mambo tuyaache tu kwa style hiyo Bado mnanishauri KUOA?
Ngoja nizeeke zeeke kwanza

Ahahaha hauko peke yako (hapa asipaone shemeji yako)

Halafu Mavoko Rich anasema, "haya maneno walisema wazee wa zamani, ukiwa mjanja kuchapiwa ni siri ya ndani."

Mi nauaaaaaaaaaaaa....roho yangu niachie ila yako pia halali yangu!!!

#badoniponiposana cc: Mbu
 
Last edited by a moderator:
Mchangiaji moja kasema heri mapenzi ya wazazi wetu.haya zamani yalikuwepo ila ilikuwa siri ya ndani.kuna jamaa mmoja walikuwa wanapenda kucheza na watoto wa mama jirani ambao walikuwa wanafanana nao sana.walipo kuwa wakubwa ndio wamekuja kujua kumbe ni ndugu zao
 
panapofuka moshi ujue kuna moto
sio kila habari au maneno yanayomhusu mwenzi wako ni ya kudharau
mengine hua kweli ati..pole yake
 
Kulikuwa na simulizi fulani ya Mkata mti mmoja ambaye alipokuwa anakata mti,pembeni palikuwepo na kijana aliyekuwa amelala.Yule mkata mti akamwambia yule kijana 'ondoka hapo utaangukiwa mti' Yule kijana alibisha akasema 'niko macho,naona vizuri hauwezi kuniangukia' Lakini mwisho wa simulizi hiyo,Mti ulimwangukia na akafa pale pale.
....
Nimekumbuka usemi huo baada ya jirani yangu kumuona ameanza ulevi ghafla,kawa mkali kwa mkewe kuliko tulivyomzoea! Juma lililopita nikiwa natoka kwenye kusaka riziki, akaniona na kusema nimpe pesa kidogo akashitue..Nikampa Mnamo usiku wa saa mbili akaja kwangu akiwa pombe imemkaa vema na kunisimulia mengi ambayo hakika yanaumiza
....
Pale kwake alimleta kijana mmoja wa kuhudumia mifugo yake,Kijana huyo alipofika katika familia hiyo akaanza mazoea na mama mwenye mji,ambayo hayakuwa mazuri kimaadili.Hata hivyo kijana huyo ambaye ni 'Handsome' kama wasemavyo vijana wa mjini,alijifanya mtii
....
Watu hawana dogo walianza kumtonya mwenye nyumba kuwa mazoea yale si mazuri lakini akawajibu anamwamini mkewe na alikuwa makini kuwa hakuna litakalotokea
....
Baada ya muda amebaini mama wa ile nyumba ana ujauzito.Akamuuliza mkewe akakiri.Mumewe akabaki anajiuliza ilikuwaje kwani walipanga kutopata mtoto mwingine ili wapate nafasi ya kulea watoto wao wawili ! Mwanamke anabaki analia.Kibaya zaidi yule kijana amekimbia hajulikani alipo pasipo kugombezwa au kuaga.Mambo yote hayo yanamjengea picha kuwa tayari ile mimba si yake
.....
Jirani rafiki huyu anajilaumu sana ni kwa nini alipuuza aliyoambiwa? Ni heri angewasikiliza.Nimemshauri asubiri matokeo.
Hapa ndipo nilipojua kweli,ukiambiwa na watu wengi juu ya jambo moja linalofanana kuhusu mpenzi wako au kazini kwako,,Chunguza Si kila mmoja hakupendi au anakutakia mabaya.Using'ang'anie tu 'Niko Macho Niko Macho' utaangukiwa mti.
^^



naomba kuuliza swali....
hivi watu wakiingia kwenye ndoa/wakishaoana, abortion hairuhusiwi?
(watu naona hawalizungumzii hili, as if hawalifikirii hili, nidhamu za uoga tuu)
 
naomba kuuliza swali....
hivi watu wakiingia kwenye ndoa/wakishaoana, abortion hairuhusiwi?
(watu naona hawalizungumzii hili, as if hawalifikirii hili, nidhamu za uoga tuu)

^^
Sina majibu ya kisheria au ya kidaktari (Kama kuna anaefahamu atatusaidia)
Lakini kwa upande wa majibu ya kiutu na kihisia kutoa mimba ni kudhulumu haki ya uhai kwa mtoto asie na hatia Kama daktari ataruhusu abortion ifanyike ili kunusuru uhai wa mama basi inaweza kufanyika.
Vinginevyo suala la kulea watoto wasio wetu kwa kujua au kutojua ni pigo jingine aliloongezewa mwanaume
^^
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom