Niko kigoma

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wakuu
Sijaonekana jf kwa siku kama 7 hivi.
Niko Kigoma.
Shida hapa ni umeme na cafe inanilazimu nilipe bei tofauti tofauti.
Kama kuna umeme wa Tanesco 1,500/= kama ni Generator 2,000/=.
Umeme ni mgao wakuu.
Zaidi baadaye.
 
pole sana kule hakuna grid ya taifa!hata tanesco wanatumia generator!Kigoma ni otherland hiyo upo burundi mkuu!
 
Pole sana! Huko hata time zone inapaswa iwe ki burundi burundi! Maana utashangaa saa inasema vingine na hali halisi inakupa picha tofauti! Inabidi tu utese mawese!
 
pole sana kule hakuna grid ya taifa!hata tanesco wanatumia generator!Kigoma ni otherland hiyo upo burundi mkuu!

First Lady,
Ni vema ukachunga lugha unayoitumia ni kweli 'Kigoma iko Burundi?' Hali ya kigoma inawakilisha na inaonyesha hali halisi ya mgawanyiko uliopo katika nchi yetu. Inakuwaje, Kigoma ambayo ni sehemu ya Tanzania kuwa kama ilivyo kwa sasa? kweli imesahaulika kabisa. Sijawahi kusikia kigoma inapewa kipaumbele katika miradi ya maendeleo, mara utasikia, mradi fulani unakwenda kilimanjaro, Dsm, Mbeya au Mwanza kigoma sio rahisi. Hali kama hiyo imesababisha wananchi wa kigoma kuwa wapinzani wakubwa wa chama tawala. Wewe uliyeko huko endelea kutuletea habari kuhusu mkoa huo
 
Jibu unalo halafu unauliza uliza hapa!
 
Wakuu
Sijaonekana jf kwa siku kama 7 hivi.
Niko Kigoma.
Shida hapa ni umeme na cafe inanilazimu nilipe bei tofauti tofauti.
Kama kuna umeme wa Tanesco 1,500/= kama ni Generator 2,000/=.
Umeme ni mgao wakuu.
Zaidi baadaye.

Mchukia Fisadi,
Tafadhali usiishie hapo mjini, toka kidogo tu kuna daladala zinaelekea Mwandiga kwa Mhe. Zitto Kabwe, kaone mwenyewe na uendelee kutupasha habari. Tunaposema ufisadi umeitafuna nchi ni pamoja na kudumaza mikoa ambayo ni tajiri sana kwa mali asili. Mchukia fisadi tunakutegemea sana utuletee unachokiona.
 
uniletee migebuka usisahau kwenda kibirizi kununua dagaa!I LOVE KIGOMA my kids homeland
 
Wana JF,
Mkoa wa Kigoma unawakilisha jamii ya WTZ ambao wameathirika sana na tawala zilizopita. Kama wanaJF, hakuna haja ya kuanza kubeza mkoa wa kigoma bali tueleze ukweli ili tawala zilizopo zielekeze nguvu za ziada katika mkoa wa kigoma na mikoa mingine inayofanana nayo. Mhe. Jk, alipoingia madarakani, yeye aliahidi kuinua mikoa ambayo aliita mikoa ya 'PEMBEZONI', maana yake mikoa iliyosahaulika kimaendeleo. Sasa sijui kama kweli Jk anafanya kama alivyoahidi.

Kwa wanaobeza kwamba kigoma iko nyuma kimaendeleo, isingepaswa kuwa nyuma. kigoma inautajiri wa kutisha: ni mkoa unaolima michikichi, wote mnajua products za michikichi ikiwemo korie tunayolingia hapa Dsm ambayo tunaagiza kutoka Malaysia badala ya kuhimiza viwanda kujengwa kigoma. Kigoma nyanda za juu wanalima Kahawa, migomba na ni wafugaji wakubwa wa mifugo kama ng'ombe n.k. Kigoma wanalima mpunga kiasi kwamba nchi jirani zinaitegemea chakula kutoka kigoma. Kigoma ina mbuga za wanyama adimu kama sokwe, jambo la ajabu mbuga zinazoongelewa ni nyinigne sio 'gombe wala Mahale. Kuna samaki wa kipekee migebuka na dagaa na pia kuna samaki wa mapambo ambaye duniani anapatikana kigoma na Brazil (watalaam mtanisaidia hapa). kuna utafiti unaoendelea kufanyika na inasemekana bonde la ziwa tanganyika kuna reserve kubwa ya mafuta.

Kijiografia, kigoma imependelewa, ni njia ya kufika Burundi, Congo DRC, Zambia, Rwanda pia ni rahisi kufika. Sasa opportunities zote hizo hazikutumika na hazitumiwi na tawala zote zilizopita na ile iliyopo. Sasa kwa nini kigoma isiwe nyuma? is like a sleeping giant, but, as we go on, Kigoma deserves a lot interms of socio-economical development.
 
Mwakeye first lady hahhaaaaaaaaaaaaaaaa!

wewe nilijua tu maana nimetania kuisema KG vibaya nusu unirukie nahisi tungekuwa hatutenganishwi na skrini sijui ingekuwaje!mimi Kigoma naipenda sana
maana ni mkoa wa wanangu pia ubavu niliowekewa ndo ulitoka huko!I thank MY GOD MY LORD FOR THIS!
Ila usijali ipo siku KIGOMA itakuwa juu kimaendeleo
 
Wakuu
Sijaonekana jf kwa siku kama 7 hivi.
Niko Kigoma.
Shida hapa ni umeme na cafe inanilazimu nilipe bei tofauti tofauti.
Kama kuna umeme wa Tanesco 1,500/= kama ni Generator 2,000/=.
Umeme ni mgao wakuu.
Zaidi baadaye.

Du pole mkuu. Hizo ndiyo tofauti za mikoa ya Tanzania. Swala la uneven development and distribution of income are issues to be addressed. But puuh who is responsible wakati kila mwenye uwezo wa kuamua katika serikali zetu kwanza anafikiri kwa namna gani atafaidika yeye na mipango bila kuangalia majority.

Na ijulikane wazi kuwa baada ya kuonekana upinzani ni mkubwa Kigoma then serikali ya ssm inakomoa mikoa kama hiyo pia. Japo katika campaign JK aliahidi kushughulikia mikoa ya pembezoni ambayo iko nyuma kimaendeleo, basi nakuuhakikishia atashughulikia yote lakini si Kigoma kwa Chadema na CUF.

Vinginevyo mkuu naomba uniletee zile sabuni zinazotengenezwa na mafuta ya mawese, sijui wanaziita nini vile.,zina mabaka ya blue na white All the best with your plans there, safari njema ya kurudi home.
 
Sio Kigoma tu, kuna mikoa iko katikati lakini hakuna maendeleo kabisa mfano Singida huwezi fikria hakuna hata mtu anaoungelea. Kwa mimi angalau Kigoma yupo ZITO na wengine lkn Singida hata wabunge wake siyo machachari huko INHOUSE. Huu ndio wakati tuanze kuzungumzia maendeleo ya maeneo husika, hii itawakumbusha wahusika.
 
kibaya zaidi mikoa yote hiyo(Kigoma,Singida,Lindi) ina utajiri na location za nguvu sana kushinda mikoa mingi.Ipo siku kitaeleweka.
 
Dhana iliyopo TZ ni kwamba mpaka mpate waziri muhimu kama wa miundo mbinu au mtoe Rais ndio mtakumbukwa. Rukwa (Mpanda) si mnaona sasa angalau hata magazeti yanaandika waziri mkuu akitembelea. Wacha Tarime watake kuwa autonomous.
 
Dhana iliyopo TZ ni kwamba mpaka mpate waziri muhimu kama wa miundo mbinu au mtoe Rais ndio mtakumbukwa. Rukwa (Mpanda) si mnaona sasa angalau hata magazeti yanaandika waziri mkuu akitembelea. Wacha Tarime wadai autonomy.
 
Wakuu
Sijaonekana jf kwa siku kama 7 hivi.
Niko Kigoma.
Shida hapa ni umeme na cafe inanilazimu nilipe bei tofauti tofauti.
Kama kuna umeme wa Tanesco 1,500/= kama ni Generator 2,000/=.
Umeme ni mgao wakuu.
Zaidi baadaye.
...Ukiweza sogea sogea hadi kasulu na kibondo nasikia watz wa huko wanawekewa lami 2kms only around hivyo vimiji....sijui ndio kanya boya ya 2010!!!!! Bara bara ya Zito nadhani kazi full swing nilikuta wachina wameweka kambi yao na vifaa viko pale.. Mtu mzima kashikwa pabaya amekubali yaishe..
 
Back
Top Bottom