Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 4,124
- 6,141
Nikiwa Rais moja ya mambo ntakayoyafanya ni kuhakikisha makazi ya watanzania yanakuwa mazuri na katika ubora unaotakiwa
Nchi nzima itapimwa na kutengenezwa master plan itakayokuwa kwenye 3D
MAMBO YA KUZINGATIA
Kwa nyumba za watanzania walio wengi
GHARAMA ZA NYUMBA
Hizi gharama zitajumuisha nyumba nzima mpaka kupaua, rangi ya nje na mazingira ya nje, madirisha tiles za ndani, na rangi ya kwaida ya ndani- nje unaweza badilisha ubora wa rangi ila color ni ilele inatakiwa uniform kwa eneo husika
Apartment
Kwenye kila mji kutatengwa maeneo ya kujenga Apartment Mfano kwa dsm maeneo ya kimkakati ya mjini mfano kwa dsm kigogo, magomeni, manzese, kigogo, sinza, ubungo huku asilimia 100 ya nyumba zitakuwa ni Apartment na magorofa marefu wenye maeneo wataingia mkataba na developer namna ya kufikia muafaka
Hapa kutakua na partnership kati ya mwenye eneo na developer
MAENEO YA KIFAHARI
Hakutakuwa na subsidy kwenye maeneo yaliyotengwa kwa makazi ya watu wenye fedha, watu wanaoishi wa kipato cha chini watakubaliana na developer namna ya kutafutiwa eneo lingine na kuyaachia maeneo ambayo yapo kwenye maeneo yaliyotengwa ya kifahari
MENGINEYO
- Barabara zote zitakuwa kubwa na zitapigwa lami
- Kukiwa na mipango miji kutakuwa ni rahisi kupigwa paving
- Kutakuwa na mfumo wa Sewage watu hawatachimba tena mashimo
- Nyumba zote zitakuwa na access ya bomba la maji, fiber kwa ajili ya Internet hata mtu asipotaka kuunganisha miundombinu itakuwa ipo
- Kutakuwa na maeneo ya wazi kwa ajili ya kuchezea watoto
- Kutakuwa na public garden kwa ajili ya watu kupumzikia
Nchi nzima itapimwa na kutengenezwa master plan itakayokuwa kwenye 3D
MAMBO YA KUZINGATIA
- Serikali itahakikisha gharama za kujenga nyumba zinakuwa ndogo sanaaa ili kuhakikisha zoezi la kureplace nyumba ambazo zipo kwenye squatter linafanikiwa
Kwa nyumba za watanzania walio wengi
- Serikali itatoa mda kwa wenye nyumba wa mtaa husika waweze kubadilisha nyumba zao na kuzijenga kulingana na masterplan
- Mwenye nyumba atajengewa nyumba inaypendana na standard inayotakiwa na atalipa deni kwa mda wa miaka 15
GHARAMA ZA NYUMBA
Hizi gharama zitajumuisha nyumba nzima mpaka kupaua, rangi ya nje na mazingira ya nje, madirisha tiles za ndani, na rangi ya kwaida ya ndani- nje unaweza badilisha ubora wa rangi ila color ni ilele inatakiwa uniform kwa eneo husika
- Nyumba ya hali ya chini kabisa laki 3 haya ni yale maeneo kwa ajili ya watu maskini, miji ya Tanzania lazima iwe inclusive na zitakuwa zinampangilia- sio lazima ulipe mara moja mtu anaweza lipa hata kwa miaka 3
- Chumba kimoja master na store million 3
- Chumba kimoja cha kulala, sebule, jiko, store million 5
- Vyuma viwili vya kulala, sebule, jiko, dinning, store million 8
- Vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko, dinning, store na sebule million 8
- Vyumba vinne vya kulala, sebule, dinning, store, na sebule million 12
- Vyumba vitano vya kulala, sebule, dinning, store kubwa, million 18
Apartment
Kwenye kila mji kutatengwa maeneo ya kujenga Apartment Mfano kwa dsm maeneo ya kimkakati ya mjini mfano kwa dsm kigogo, magomeni, manzese, kigogo, sinza, ubungo huku asilimia 100 ya nyumba zitakuwa ni Apartment na magorofa marefu wenye maeneo wataingia mkataba na developer namna ya kufikia muafaka
Hapa kutakua na partnership kati ya mwenye eneo na developer
- Mwenye eneo anaweza muuzia developer eneo na likawa mali ya developer
- Mwenye eneo anaweza ingia mkataba na developer kwamba atapewa apartment mbili na zilizobaki zitakuwa za developer
MAENEO YA KIFAHARI
Hakutakuwa na subsidy kwenye maeneo yaliyotengwa kwa makazi ya watu wenye fedha, watu wanaoishi wa kipato cha chini watakubaliana na developer namna ya kutafutiwa eneo lingine na kuyaachia maeneo ambayo yapo kwenye maeneo yaliyotengwa ya kifahari
MENGINEYO
- Mabanda ya chips yatakuwa na namna ya kuyajenga hayatajengwa kiholela holela kama ilivyo sahivi
- Mama ntilie watakuwa na sehemu zao maalumu na sio kupika vichochoroni
- Guest watakuwa na maeneo yao
- Bar watakuwa na maeneo yao hawatajijengea tu watakuwa na namna ya kujenga
- Maduka ya kuuza vitu vya rejareja yatakuwa na standard yao
- Saloon za kiume zitakuwa na standard zao
- Saloon za kike zitakuwa na standard
- Massage centre lazima watakuwa ni professional na watakuwa na namna yao ya kujenga
- Open space zitakuwepo wale ambao maeneo yao yametengwa kama open space watalipwa fidia
- Public garden zitakuwepo wale maeneo yao ambayo yatakuwa ni public garden watalipwa fidia
- Kila mtaa utakuwa na kituo cha bodaboda ambacho kitakuwa cha kisasa sio na itakuwa ni marufuku bodaboda kujenga kiholela holela
- Garage za magari na pikipiki hazitajengwa kiholela
- Car washing zitakuwa na namna ya kujenga
- Ofisi za carpenter, welding nazo zitakuwa na namna ya kuzijenga hazitajengwa kiholela
- Gym hazitajengwa kiholela