Nikiwa nimelala nikisimama nasikia maumivu makali upande wa shingo kulia kwenda kwenye bega. Na kugeuza shingo inakua inauma

Yote mema

New Member
Jan 7, 2024
3
1
Wakuu nina shida, mwanzoni nilienda kwenye polyclinic nikaambiwa nina UTI kali, so nikachoma sindano tano nimezimaliza juzi.

Shida ni kua nikiwa nimelala, nikisimama ghafla nasikia maumivu makali yanayotoka kwenye upande wa sikioni kushuka kwenye bega upande wa kulia.

Na kitu kingine nikiwa nafungua mdomo unakua unalia kacha, kacha
Hii shida ni nini wakuu msaada tafadhali.
Danielmwasi stephot
 
Maelezo hayajatosheleza sana, pia ukaguzi wa mwili hasa sehemu husika ni muhimu. Kuna haja ya kujua kama: kuna ganzi, kusikia kama shoti ya umeme, nguvu ya umezo wa kung'ata.

Ingawa maeneo muhimu yaliyohitaji kufatiliwa:
1: Sikio lenyewe(kama kuna madhira yoyote)

2: Trigerminal nerve(mshipa wa fahamu unaochomoza mbele ya sikio).

3: Temporal mandibular jointi (jointi iliyopo usawa au chini.kidogo ya sikio).
 
Back
Top Bottom