Nikimtosa wanangu je?

danmwitta

New Member
Jun 6, 2011
3
0
Nimezaa nae watoto wawili,tumeishi miaka 12,nampenda sana ila alishanihakikishia katu hatobadili dini,iwapo nataka mke mkristo nioe,wanangu bado wadogo mmoja miaka 7,wa pili miaka 4. Kiimani sipo popote pia wanangu muda wote wana mama yao na mimi nafanya kazi mkoani.nifanyeje? Nioe mwanamke mkristo mwenzangu au je? Nishauri jamani!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mwita ndugu yangu unanishangaza kweli
tangu lini mura akajali dini?(jokes)

enewei,
unless otherwise convinced,dini haiwezi kuwa sababu ya wewe kuoa mwanamke mwingine tofauti na huyo unayedai 'Nimezaa nae watoto wawili,tumeishi miaka 12,nampenda sana'
oooh please give me a break! ni mapenzi gani hayo unayoongelea?kama umeweza kuishi naye bila tatizo for 12 good years,kimetokea nini cha kukufanya ubadilike sasa hivi?
 
unataka nini tena mkuu..........kuishi miaka 12 mmepitia machungu/matamu zaidi ya hapo mnajuana ndani nje...........kunamafanikio mengi mmeyapata mkiwa pamoja......unapokwenda kuoa mwingine kwa ajili ya dini ni kujitakia matatizo...........swala hapa ni upo nje ya kundi inakuwa umetengwa kikanisa unaweza kuwaona watumishi wa kanisa wakusaidia mawazo...........nasikia kuna kufunga ndoa ya mseto
 
hebu acha utani Mura...umekaa na dada wa watu miaka yote hiyo na mmezaa watoto wawili...hukuona dini yake? au hujui kama kulikuwa na wakaka wa dini yake walikuwa wanampigia misele enzi hizo na akawakataa kisa wewe?
nakushauri ukae na mkeo mleee watoto.
 
Miaka yote mmeishi hadi mkafikia hatua ya kuzaa na sasa mnao watoto 2,
Je ulikuwa wapi kujiuliza swala la dini au imani?
Kwenu hapo mlipofikia sion kama dini ni sbb ya kuwatenganisha kama mmeishi wote
12yrs na sasa ndo mnajiuliza haisaidia kama ni ndoa nenda bomani mkafunge ndoa ya
bomani na siku zote huma nina imani kuwa dini zote tumnamuabudu mungu mmoja
watoto wakikua wataamua wenyewe ni dhehebu gani waende
 
Ndugu,jikague kile ambacho unaona ni bora kwako kifanye!Mambo ya imani yana umuhimu wake,but inategemea na wewe unavyoyachukulia mambo,ila kila jambo lina jambo!
 
Nimezaa nae watoto wawili,tumeishi miaka 12,nampenda sana ila alishanihakikishia katu hatobadili dini,iwapo nataka mke mkristo nioe,wanangu bado wadogo mmoja miaka 7,wa pili miaka 4. Kiimani sipo popote pia wanangu muda wote wana mama yao na mimi nafanya kazi mkoani.nifanyeje? Nioe mwanamke mkristo mwenzangu au je? Nishauri jamani!!!!!!!!!!!!!!!!
Hapo kwenye ekundu: uoe mkristu ili iweje na wewe unasema kiimani hupo popote. Hii yaonesha au huko mkristu, au kama uko mkristu basi huiishi imani yako. Sasa mke mkristu, ili iweje? We sema tu: "nioe mke mwingine"?
Nakushauri kama unaishi naye vizuri huna sababu ya kumwacha na kuoa mke mwingine (mkristu). Baki naye huyohuyo, mtunze akutunze na kwa pamoja mtunze watoto wenu. Waleeni watoto katika imani pia: au imani yako (ambayo naona huiishi) au katika imani ya mke. Itawasaidia watoto kumjua Mungu na kujua yote mema yanayomsaidia mtu kuishi vizuri na wengine.
 
boc huoi dini unaoa mke na tayari mke unaye so sahau hizo longolongo. after all kisheria baada ya miaka 2 huyo ni presumed wife wako. relax wajengee maisha wanao na usianzishe vurugu za kuoa mke mwingine utaacha vita huku nyuma
 
Muoe tu kwa serikalini, mapenzi hayaangalii dini, mambo yenu ya dini yasiwaumize watoto ambao bado ni wadogo na wanahitaji upendo wa wazazi wao wote wawili, kama unampenda kama ulivojielezea, usimwache oaneni serikalini kila mtu abaki n dini yako, watoto inajulikana huwa wanafata kwa baba mengine ni maelewano tu
 
Nimezaa nae watoto wawili,tumeishi miaka 12,nampenda sana ila alishanihakikishia katu hatobadili dini,iwapo nataka mke mkristo nioe,wanangu bado wadogo mmoja miaka 7,wa pili miaka 4. Kiimani sipo popote pia wanangu muda wote wana mama yao na mimi nafanya kazi mkoani.nifanyeje? Nioe mwanamke mkristo mwenzangu au je? Nishauri jamani!!!!!!!!!!!!!!!!

Kama suala la dini lingekuwa muhimu kwako ungelitatua kabla hata ya kuanza kuishi wote. Sio kusubiri baada ya miaka 12. After all umesha sema kiimani haupo popote. Sasa kwa nini unataka mama watoto abadilishe dini, wakati wewe mwenyewe kiimani haupo popote? Nilidhani wewe ni fundamentalist fulani hivi, lakini sivyo. Kwanza, umeishi nae miaka 12 wakati ukijua kabisa kuwa yeye sio mkristu. Pili, umezaa nae watoto wawili wakati unajua kabisa kuwa yeye sio mkritu. Tatu, wewe mwenyewe kiimani haupo popote. Kwa sababu hizo tatu, nakupotezea.
 
Umuache mkeo uoe mke mkristo wakati we mwenyewe kiimani hauko popote....it doesn't make sense!!
Kuna watu wengine hata hawajui wanataka nini, you want to destroy uhusiano thabiti wa miaka 12 sababu ya dini? wewe ni wa karne hii ya sasa au, dini sio kigezo siku hizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom