Niki wa Pili: Magufuli anawanyima watoto haki ya kikatiba

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
32,882
2,000
Akihojiwa na kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv amepingana na msimamo wa rais Magufuli kuhusu kupiga marufuku wanafunzi waliopata mimba mashuleni

Msanii Msomi Niki amesema Magufuli anawanyima watoto haki ya kupata elimu ambayo ni haki ya kikatiba. Niki anasema wanafunzi wa kike waliopata mimba wanatakiwa wachukuliwe kama watu wenye mahitaji maalumu,wanahitaji faraja na kutokutengwa na jamii. "Fikiria baba wa mtoto yupo jela miaka 30,mama ametengwa na jamii" anasema Niki

Niki anasisitiza kuwa jamii isiwe na watu waliojaa hofu ya kusema wanachoona kinafaa zaidi na sio kunyamaza huku wakiumia.

Niki pia amesisitiza vijana kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu na maandiko kwani kumejaa maarifa
 
kipanta

JF-Expert Member
Sep 2, 2014
576
1,000
naona NIKI ana point nzuri sana hapo...mi pia kwa swala hili naona mheshimiwa katumia mbinu ya kutisha wakati naisi kuna njia mbadala ya kueza tokomeza hili swala sugu la mimba mashuleni....vitisho sio mbinu sahihi kwa watoto wadogo hapa ni sawa na kurudi enzi za ukoloni when wazazi walikuwa hawataki hata kuongea maswala ya sex mashuleni
 
Maxmizer

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
4,820
2,000
Akihojiwa na kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv amepingana na msimamo wa rais Magufuli kuhusu kupiga marufuku wanafunzi waliopata mimba mashuleni

Msanii Msomi Niki amesema Magufuli anawanyima watoto haki ya kupata elimu ambayo ni haki ya kikatiba. Niki anasema wanafunzi wa kike waliopata mimba wanatakiwa wachukuliwe kama watu wenye mahitaji maalumu,wanahitaji faraja na kutokutengwa na jamii. "Fikiria baba wa mtoto yupo jela miaka 30,mama ametengwa na jamii" anasema Niki

Niki anasisitiza kuwa jamii isiwe na watu waliojaa hofu ya kusema wanachoona kinafaa zaidi na sio kunyamaza huku wakiumia.

Niki pia amesisitiza vijana kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu na maandiko kwani kumejaa maarifa
nimegundua kumbe mkulu hasomi vitabu
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
1,945
2,000
wazazi timizeni wajibu wenu wa kuwalea watoto wenu ktk maadili mema, tusitoe visingizio, alicho kisema mkuu wetu wa nchi ni kwa maslahi ya familia zetu na taifa kwa ujumla!!

kila mzazi akitimiza wajibu wake, mimba za utotoni zitaepukika na watoto wa kike watafikia ndoto zao!!

wazazi acheni kuwa dekeza watoto wenu kama mayai!!! wakanyeni wapelekeni makanisani na misikitini wapate kubadilika kiroho.

kauli ya JPM itapunguza kama si kukomesha vitendo vya mimba kwa watoto, hivyo wapenda maadili tuunge mkono kwa vitendo kauli ya Rais badala ya kubeza!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom