Nikasema nilikuwa na Jini mahaba…..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikasema nilikuwa na Jini mahaba…..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 20, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa ndio nimemaliza kidato cha nne na kuja jijini Dar na kufikia kwa mjomba wangu aliyekuwa akiishi maeneo ya Tandale kwa Mkunduge ili aweze kunifanyia mpango wa kupata vibarua huko viwandani. Pamoja na kusomea huko vijijini na kuwa ndio mara yangu ya kwanza kuja mjini lakini nilikuwa ni kijana machachari sana pale mtaani kutokana na ubitozi wangu wa kijijini. Nilikuwa nimejijengea marafiki wengi pale mtaani na walikuwa wanapenda sana stori zangu za bushi, wakati huo mimi nilikuwa najua nawakoga kwa stori zangu, lakini kumbe walikuwa wananisanifu kwa lafudhi yangu ya kilugaluga.


  Miongoni mwa watu waliokuwa wakivutiwa na stori zangu alikuwepo dada mmoja wa Kingoni ambaye alifahamika kwa jina la Marceline. Tulikuwa tukiishi naye nyumba moja akiwa ndio ana miezi miwili tangu ahamie nyumba hiyo, sisi tukiwa tumepanga nyumba kubwa na yeye akiwa amepanga banda la uani. Huyu dada alikuwa ni mzuri kwa kiasi chake hasa wa umbo maana alijaaliwa kuwa na kalio kubwa la mviringo mwenyewe nilikuwa napenda kuita kijungu na sura pia haikumuangusha. Alikuwa ni muuguzi na alikuwa anafanya kazi hospitali ya Magomeni wakati huo. Hakuwa ameolewa ila aliwahi kunidokeza kwamba anaye mchumba ambaye anasoma nje ya nchi. Alikuwa anapenda sana kupiga stori na mimi na alikuwa ananipenda sana, maana hata vijizawadi alikuwa anapenda kuniletea kila anaporudi kutoka kazini. Mimi kama kijana ambaye sikuzoea upendo wa aina nyingine isipokuwa ule wa kingono nilianza kuutafsiri vibaya upendo ule. Ingawa alikuwa ananizidi umri labda kama miaka kumi hivi, lakini nilijua dhahiri kwamba dada Marceline ananitaka, na nilijua anataka vijana shababi kama mimi ambao damu inachemka. Niliamini hivyo kwa sababu tangu ahamie katika nyumba tuliyokuwa tukiishi alikuwa anapenda sana kuongea na mimi na ni mimi pekee kati ya vijana tuliokuwa tukiishi katika nyumba ile ambaye nilikuwa naingia chumbani kwake, kupiga naye stori.

  Kutokana na ukaribu ule, nilijikuta nikiingiwa na ibilisi na kutamani kumtongoza, maana nilikuwa najua tu kwamba ananitaka lakini nilijua hawezi kuniambia kwa sababu kwa kawaida wanawake huwa hawasemi bali husubiri watongozwe. Nilianza mikakati yangu ya kumtongoza kwa kumchomekea vijineneno vya mapenzi nikiwa napiga naye stori, lakini akawa anageuza yale mazungmzo yangu kuwa utani, mie kwa ujinga wangu nikajua hiyo ndiyo kawaida ya wanawake ya sitaki nataka. Basi siku moja kulikuwa na msiba pale mtaani ikatokea watu wote tumetoka kwenda msibani. na pale nyumbani walikuwa wamebaki watoto pekee. Mida ya saa moja usiku shangazi alinitaka nirudi nyumbani nikakae na watoto kwa sababu kulikuwa hakuna mtu mzima. Nilipofika nyumbani nilipitiliza moja kwa kwa moja hadi uani ambapo nilikuta taa ikiwaka chumbani kwa dada Marceline. Nikajua atakuwa amerudi kutoka kazini, nikajiseme moyoni kwamba huo ndio wakati muafaka wa kuomba utukufu, na nilijua kwa sababu tuko peke yetu asingeweza kukataa, nilibisha hodi nikiwa na shauku, na hakuchukua muda akafungua mlango, aliponiona alinikaribisha ndani na moja kwa mojan nikaenda kukaa kwenye kitanda.

  Alionekana kushtuka kidogo, kisha akaniambia, ‘lakini mbona kochi liko wazi kwa nini ukae kitandani' mimi kwa kutojua amekereka, nikamuuliza, ‘kwani ni nani mwenye mamlaka ya kukalia kitanda hiki zaidi yangu?' hakunijibu bali aliguna tu, alikaa kwenye kochi na kisha akaendelea na kazi yake ya kufuma vitambaa vyake, nilinyanyuka na kuhamia kwenye kochi, na kumwambia, ‘haya nimekuja kukaa karibu yako mpenzi usije ukaninunia bure……….' Alinitazama usoni kisha akatabasamu. Mimi kuona lile tabasamu nguvu zikaniishia kabisa nikaona nisicheleweshe mambo, nikajikakamua na kumwambia, ‘unajua Marcelina nakupenda sana na nimeshindwa kuvumilia nimeona leo nikwambie ukweli' Alishtuka kidogo kabla hajaniambia, ‘ahsante kwa kunipenda, mbona hata mie nakupenda sana tu, kwani hata katika amri kumi za Mungu tumeambiwa tuwapende majirani zetu kama tunavyojipenda.' Nikajua amechomekea tu neno la Mungu ili kuzuga, lakini alitaka ujumbe ufike. Sikulaza damu, nikamsogelea na kumuwekea mkono begani huku nikimwambia, ‘kwa kuwa mjomba na shangazi watalala msibani, basi mie nitalala hapa kwako ili tupeane mahaba mimi na wewe, au unasemaje?'

  ‘Huo siyo utani mzuri, najua kama binadamu unaweza kunipenda kwa njia hiyo lakini hujui hiyo ni hatari mchumba angu akijua na isitoshe wewe ni kijana mdogo sana kwangu na jinsi unavyonichukulia sivyo kabisa.' Aliniambia kwa upole kisha akautoa mkono wangu begani kwake akanyanyuka na kwenda kukaa kitandani, kisha akashusha pumzi huku akiniangalia, nadhani alikuwa haamini kile kinachotokea mbele yake, lakini kwa kuwa ibilisi wa ngono alishanipanda na damu ilikuwa ikinichemka, wala sikusoma uso wake, mimi nikajua ndio kawaida ya wanawake lazima waweke vikwazo kidogo. Nilinyanyuka na kumfuata pale kitandani, alikuwa ametulia akisubiri kitakachofuata, nilipofika kitandani nilikaa pembeni yake kuanza kubwabwanya. ‘Najua ni kweli lakini kwa jinsi ninavyokupenda yaani huwezi kuniambia kitu nikakuelewa, naomba unihurumie, nakuomba…………………………' Wakati nasema maneno hayo alikuwa ametulia, huku akiniangalia, nikaona atakuwa amekubali, nikaupeleka mkono wangu shavuni mwake kisha nikaushusha hadi shingoni, yeye ametulia tu akiniangalia. Mpaka hapo nikajithibitishia kwamba alikuwa akinipenda sana, na Ibilisi wangu akazidi kunipa ujasiri wa kwenda mbali zaidi, nikaushusha mkono wangu taratibu hadi kwenye titi la kulia.

  Kuona hivyo alisimama ghafla akitaka kutoka, nilimdaka kama chui anavyomkamata swala, na katika kuvutana gauni lake likachanika mgongoni pale inapoishia zipu mpaka chini, alimudu kunichomoka na kutimua mbio kutoka nje. Nilibaki pale ndani kwake kwa nukta kadhaa nikijiuliza imekuwaje, maana niliona kila kitu kilikuwa shwari. Hata hivyo niliamua kutoka nje ili kumuangalia kama ameenda wapi lakini sikumuona pale uani, niliamua kwenda kumfuata chooni lakini sikukuta mtu, niliamua kuingia ndani kwetu nikawa natafakari tukio zima jinsi lilivyokwenda, na kujilaumu kwa kumchelewesha. Mpaka hapo bado akili yangu ilikuwa inaniambia kwamba Marceline alikubali ila alikuwa ananionea aibu kwa sababu tumezoeana.

  baada kama ya nusu saa hivi mtoto wa mjumbe wa shina alikuja kuniita, akiniambia kwamba naitwa na mjumbe, akili yangu haikufanya kazi sawasawa, nilijua labda ni mambo ya msiba kwani kukiwa na msiba mjumbe huwaita vijana ili kutoa maelekezo ya shughuli za kuchimba kaburi. Nilipofika nilimkuta mjomba, shangazi, Marceline na wazee wawili maarufu pale mtaani pamoja na wamama wengine wawili wa pale mtaani. Akili yangu bado ilikuwa ni ya Kifisi Maji kwani iliniambia kuwa itakuwa ni maswala ya msiba kwa kuwa nilimuona Marcelina kajitanda kanga moyo wangu wala haukushtuka.

  Niliwasalimia wote niliowakuta pale lakini hakuna aliyeniitikia. Nilijaribu kuulizia agenda za kikao hicho, lakini mjumbe akanikata kalma na kuniambia kwamba siku hiyo kulikuwa hakuna agenda bali wanamsubiri Polisi kutoka ofisi za CCM (Kipindi hicho polisi Post zilikuwa ziko kwenye ofisi za CCM kabla ya ujio wa vyama vingi wenyewe tulikuwa tunaita Polisi zone). Haukupita muda nilimuona Polisi akifika pale akiwa ameshika Pingu, na ndipo yule mjumbe akafungua kikao kwa kusema………., ‘Ndugu zanguni samahani sana, ni jambo la kusikitisha kwamba pamoja na kuwa tumepata msiba mkubwa hapa mtaani kwa kufiwa na sheikh wa mtaani kwetu, lakini kuna mwenzetu mmoja ambaye tulikuwa tunamuheshimu sana, tukidhani nimuadilifu, lakini kumbe ni chui ndani ya ngozi ya kondoo, na kwa kukosa haya na adabu amejaribu kumbaka mwenetu Marcelina ambaye ni muuguzi anayetusaidia hapa mtaani kutuchoma sindano za masaa tukiugua.'

  Wajumbe wote waliokuwa kwenye kile kikao waliguna na kuanza kunong'ona. Nilimuona Mjomba na shangazi wakiwa wamenikazia macho kwa hasira, nilihisi mapigo yangu ya moyo yakiongeza kasi na mwili ulianza kunitetemeka huku jasho likinitoka, kwani yule Polisi alikuwa amekaa kimya huku akiwa anazichezea pingu zake akisubiri nikabidhiwe kwake. Nikaiona jela ikiwa mbele yangu dhahiri. Kisha mjumbe akaendelea, 'Huyu kijana mnayemuona hapa mbele yenu ndiye mtuhumiwa (akinionyesha mimi) na ushahidi wenyewe ni gauni alilolivaa huyu binti, limechanwa chanwa vibaya sana utadhani binti wa watu alivamiwa na kundi la mbwa mwitu.' Yule mjumbe alisema maneno hayo huku akionyesha lile gauni la Marceline ambalo nadhani alilivulia hapo hapo kwa mjumbe na kupewa Kanga ajifunge, lengo lilikuwa ni ushahidi ukabidhiwe Polisi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

  ‘Kutokana na maelezo yako muheshimiwa Mjumbe naona kama umeshanihukumu tayari, lakini naomba nikiri kwamba niliingiwa na Jini mahaba na ndio chanzo cha tukio hilo, naomba kwa heshima ya kikao hiki nimuombe radhi dada Marceline tuyamalize….' Nilishikwa na ujasiri na kujitetea.

  Mama mmoja mwenye Kiherehere kati ya wale waliokuwepo kwenye kikao alidakia nakusema, ‘We mwana we ishia hapo hapo, iwe umekumbwa na Jini Mahaba au Jini Kipwepwere sijui, hayo yote utayaelezea Polisi, mtoto hayawani mkubwa wewe kutaka kuchungulia tupu za wakubwa zako bila aibu…………. khaaa' yule mama alikuwa akiongea kwa hisia, utadhani huyo niliyemtendea jambo hilo ni mwanae.

  Najua mnataka kujua kilichotokea baada ya hapo………………………………Jamani sikufungwa na mambo yalimalizwa kifamilia na huyo Marceline ameolewa na ameendelea kuwa dada yangu wa hiyari.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,114
  Likes Received: 2,214
  Trophy Points: 280
  Mtafute shigongo ukalambe ajira story zako kama zake nzuri kweli.
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Yaani wewe....mi najua mwisho wa story unalamba mzigo kumbe umelambwa!! Lol
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 8,923
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  da! Umenichekesha..eti imekuaje wakati mambo yalikua shwali tu...ila huyo mtoto alikuwa na roho ngumu da!
  Siku hizi ukimshika tu begani...ha ha ha analegea anatepeta ndembendembe..unapiga pasi ya mwisho fasta.
   
 5. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du! mkuu nimecheka peke yangu huyu jini kipwepwere aaaaaaaaah!
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180

  Naendelea kuunganisha dots na matukio ya Polisi....!!
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,505
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Inafaa kwenye magazeti ya udaku sehemu ya chombezo.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Mkuu unataka waniweke kwenye Most Wanted yao nini?
  Mbona naona unanichulia bana.......................Mikasa yangu niliimaliza kimya kimya
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Acha unoko wewe..................Hii sio maneno mbofu mbofu, bali ni tukio la kweli kabisaaa,........ Mama yangu mzazi vile nakuampia!
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180

  Hapana bana....najua tu one day utajisahau ukasema ulilala selo, we unataka kubaka halafu umalize kimyakimya....Lol haiwezekani!!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,103
  Likes Received: 3,866
  Trophy Points: 280
  umeamkaje mkku,
  nitarudi kusoma hii vizuri zaidi.
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Kumbe wewe hujui, kwa taarifa yako katika kesi ambazo humalizwa kimya kimya, basi ni kesi za kubaka..............Hakuna mwanamke anayeweza kusimama kizimbani akaanza kusimulia u.p.u.u.z.i aliofanyiwa....................LOL
   
 13. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa unajua kulikoroga na kulinywa pia wajua, hapo ndipo napokuaminia mkuu.
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu chonde chonde! usifanye vijana wa sasa wakaiga mkumbo!, alafu wakajajutia nafsi zao.
  Hayo yalikuwa zamani mtu anaona haya kulitamka tusi kama lilivyo, Hawa wasikuhizi neno mapenzi hawalivalishi nguo anatamka tu "Twende tukat**bane". bila wasiwasi huku anakutazama usoni.
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Haa!! kuna maelfu ya kesi za kubaka polisi na mahakani..au we unazungumzia dunia gani??
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Ulileta kisa chako kimoja humu uliandika umefikia Kariakoo. Leo unatuambia umefikia Tandale.

  Kama ni hadithi za kutunga si ueleze mwanzo kuwa hii ni paukwa pakawa.
   
 17. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  Mkuu hadithi zako nzuri kweli! ila leta muendelezo wa ile ya mwanamke wa ziwani!
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi bwana na ile hadithi nyingine ulipigwa club kwa kung'ang'ania mwanamke ukidhani ni wanaojiuza duuu!
  mkuu unaonekana ulikuwa unapenda sana ngono!
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Na wewe kumbe huna kumbukumbu...........Nilikuja kwa mara ya kwanza nikafikia kwa kaka yangu Kariakoo, baada ya mkasa wa kipondo pale Avalon Cinema niikarudishwa kijijini, baabae nikarudi na kufikia kwa mjomba mkubwa huko Temeka kata ya 14, na baada ya ule mkasa wa dogo kuja mikono mitupu nikapona kwenda jela lakini sikukaa sana nikarudi kijijini tena, mkasa huu, nilirudi tena Town na kufikia kwa mjomba mdogo maeneo ya Tandale kwa Mkunduge..........
  Haya ni kitu gani huelewi sasa?
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Haya nimekuelewa, sasa tunangoja ukija tena tuone utafikia wapi, maana hapo umeshamaliza wilaya zote tatu.
   
Loading...