Nikaribisheni Msema hovyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikaribisheni Msema hovyo

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by Msema hovyo, Jul 3, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wandugu imenilazimu kuingia humu, maana nimekuwa kimya kwa muda mrefu lakini sasa nimeamua. Na imenipasa kufanya hivyo kutakana na hasira ya kukosa umeme. Kwa kuwa kazi za ofisi haziendi wala nyumbani hakukaliki, nafikiri nitakuwa busy na simu yangu kushare mawazo na great thinkers humu ndani. Kwa kuanza napendekeza tuandamane kumshinikiza Ngeleja ajiuzulu.
   
 2. Pruner

  Pruner Content Manager Staff Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
 3. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu ila tu USIPITILIZE kwa kusema hovyo..
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Karibu sana.

  Unai recharge kwa solar?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,842
  Trophy Points: 280
  unamjua ngeleja?
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Karibu..
   
 7. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwakweli simjui ila namsikia. Maana madhara yake kwa taifa ni makubwa. Na hapo ndo nashawishika kumuandama kwa maslahi ya nchi
   
 8. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Eeeh, Mama!! Nimelazimika kununua solar charge baada ya hizi kadhia za umeme kukatika kila kuchwapo
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  karibu sana ila zingatia vigezo na masharti ya kusema ovyo.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Sasa unalalamika nini na unao umeme wako mwenyewe wa solar? hapo inabidi ufurahi kuwezeshwa kuwa na umeme wako mwenyewe, hakuingilii mtu wala hakukatii mtu, au hilo nalo waona si jema?
   
 11. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huu sasa ni utata tu FaizaFoxy. Kwa hiyo unataka kusema kule kununua nguzo ya umeme kwa milioni, kufanya wiring kwa malaki, na kuingiza umeme kwa mamilioni, ilikuwa ni kwaajili ya nini? si bora ile hela ingetumika kununua solar kama ndo hivyo? Kama mmeamua kunishawishi nitumie solar kuanzia sasa, basi nirudishieni ile hela yangu halafu mje mng'oe nguzo yenu na nyaya zenu hapa home maana zinaniletea ghasia tu.
   
 12. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngeleja alianza kama waziri wa umeme akawa waziri wa mgao na sasa kawa waziri wa giza na maafa hospitalini,huwezi amini idadi ya akina mama waliofarki kwenye meza za upasuaji kwa kukatika umeme.
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Hizo ziwache umewekeza for the near future, si unajuwa nyerere aliiacha hii nchi nyang'a nyang'a na hivi sasa ndio Mkuu JMK anaweka mambo yote swaaafi,maumeme mengi tu yanakuja hivi karibuni, wala usiwe na shaka. Maendeleo ya haraka haraka ya JMK ndio yanafanya umeme tulioachiwa na nyerere, mwinyi n\ mkapa usitutoshe kabisa kwa sasa, matumizi yanazidi mara kumi zaidi kwa mwaka kwa miaka mitano mfululizo kwa sasa, kabla ya hapo ilikuwa ukuwaji wa asilimia 10 kwa kila miaka mitano.
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mi nikisikia eti symbion niwababaishaji kuanzia alieongea mpaka aliewakaribisha nawapa CLAP na kuona wote niwasaliti wa kaeneo ketu haka katz..
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tuondolee ujinga wako kila kukicha nasikia watu wakikulalamikia kumbe mambo yenyewe ni haya ? tusubiri miaka mingapi ? eti kaeni mkao wa kula umeme waja hata kwenye shughuli si wote wanaonawa hula,kama hata kauli ya rais haiaminiki basi kuna tatizo kubwa la kiutawala.
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Karibu sana JF.
   
 17. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Karibu sana utakutana na wenzeko
   
 18. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  karibu ila angalia wasije waka ku ban wenyewe
   
 19. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  ..........................karibu sana............sitasema hovyo kwa kuwa sina charge ya kutosha kutokana na kukosa umeme tangu juzi,...................kheri yako wewe una hasira mwenzio hasira sina kwani tangu juzi sina umeme hasira nitatolea wapi.................................................kheri wewe uko busy na simu yako kushare mawazo na great thinkers humo ndani................mimi nitawapata wapi kwani computer yangu haiwaki umeme hakuna.....................................kheri wewe utaandamana maana taarifa ya maandamano utaipata.........................................................................,mimi sitoa andamana maana sitopata taarifa ya maandamano hayo kutokana na kukatika kwa umeme ambao umeikosesha simu yangu na computer mawasiliano na greatthinkers,..................................................wacha nisiseme hovyo kama wewe,............................................................siku njema......................................siendi nyumbani hamna umeme,..........................................baa pia hakuendeki kwani bia za baridi hakuna kisa umeme umekatika.....................nasema tena sisemi hovyo,
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  Karibu, sema usigope sema, ila ujue utafungiwa, sema tu.
   
Loading...