Nikaenda kumzika ibilisi wangu....!

...mzee mwenzangu, kuna pahala pameandikwa "muishi na wake zenu kwa akili!"...

Enhee....huu mkasa haufadhaishi sana iwapo unazingatia huo wosia wa kale...."Uishi na mkeo kwa akili!"
Mbu kwa hiyo na mimi niishi kwa akili na mama Ngina....................? LOL
 
Last edited by a moderator:
Hapo timing umenena! Mie nikiona mwanaume anamfanyia mkewe vibweka huwa namuhurumia yeye mwanaume. Mi nikifanyiwa visa huwa nauliza 'hivi ligi na mie utaiweza kweli!?'. Ukimuamsha alielala utalala wewe, wahenga hao sio mie!

Mbu, malizia vitabu vinasema 'msiwachokoze watoto wenu'. Mke kama mwanao, usimchokoroe, utajuuta!
waweza kuta hata mkeo ana nyumba na magari, lakini vyote viko kwa dada, mama na mashoga zake.....

habari haijanishtua, kwani wengi wa wake zetu wana usiri na ni malaika kwenye sura zetu, na iwe hivyo ili sisi na waototo wetu tuishi kwa amani....

YNWA....
 
Last edited by a moderator:
nafikiri kuna haja ya kuset ka program ukifa kumbukumbuzakao chafu zotwe kwenye laptop, face book simu na kwengine zijifute automaticaly. dah ndio maana sijaweza mpa mtu moy wangu, tupendane hivi hivi kishkaji sikuchungi, sikufuatilii we fanya uwezavyo usinivuruge na kunichafue tu.
:A S confused:
 
hebu ngoja nicheki na mama yeyoo, sijui tayari keshaanza kujenga?
 
Nilienda kumzika ibilisi wangu!

Ilikuwa ni ajali kubwa na hata mimi sijui niliweza vipi kupona. Dereva na mke wangu walifia pale pale kwenye eneo la tukio. Tulikuwa tukitokea Chalinze kurudi Dar es salaam baaada ya kukagua shamba ambalo ilikuwa tulinunue katika kijiji cha Msata wilayani Bagamoyo. Mbele kidogo ya mji wa Chalinze ndipo ajali hiyo ilipotokea . Dereva wetu alikuwa akijaribu kulipita lori fulani lakini wakati huo huo gurudumu la mbele la gari letu lilipasuka na kusababisha gari kuyumba ambapo lililivaa lile lori. Kufuatia kuligonga huko, gari letu lilirudishwa katikati ya barabara ambapo liligongana uso kwa uso na gari lingine lililokuwa linakuja mbele yetu. Sikujua kilichotokea hadi baada ya siku mbili Muhimbili.

 
Ilishawekwa na Mtambuzi humu..............
hawa viumbe sio wa kuwaamini 100%
 
Last edited by a moderator:
my God, imeniskitisha na kuniuma sana. Pole kaka MUNGU AKUSAHAULISHE HAYA.
 
Chenge hiyo kali, kila kichaka kipe hadhi yake. Duniani hakuna mwaminifu kwa kiasi ulichomwamini mkeo. tunamezea tu ili kulinda amani, familia, taifa na dunia ili vitawalike kaka. kwa msingi huo, utawala wa duia, ndoa na mapenzi mengineyo vimejaa unafiki.
 
Mbona inafanana na uzi mmoja uliwekwa jukwaa la MMU wiki chache zilizopita?
 
Back
Top Bottom