Habari gani wangugu?
Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k
Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..
Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.
Karibuni!!
Wabongo kwa kukatishana tamaa!
Nilivyo mwelewa mleta mada sio kwamba anataka kukimbia bongo moja kwa moja,ila anataka awe mbali na nchi hii hata kama ni miaka kadhaa walau apate international exposure
Graduate ana millioni saba anataka kwenda kubeba boksi Mashariki ya mbali (halafu hajui hata mashariki ya mbali ni wapi), TUNAHITAJI KUANGALIA UPYA MFUMO MZIMA WA ELIMU NA WOTE TULIOWAPA DHAMANA! Hiyo 7M hapa bongo ukifanya kweli utakuwa na zaidi ya 80M ndani ya mwaka mmoja tu! Kama unaenda matembezi hiyo pesa yako ndani ya wiki unarudi bila kitu mfukoni! CHAGUO NI LAKO.
Mzee bila shaka unayo habari juu ya phd holders wa Nigeria kubeba boksi pale London na US itakuja kuwa mimi degree holder wa juzi nisiye hata na uzoefu wa miezi mitano ya kufanya kazi officialy kwenye taasisi yoyote hapa Bongo.
Ukinielewa baadae nipe ushauri kulingana na mukatadha niliojikita tafadhali ndugu.
Wabongo kwa kukatishana tamaa!
Nilivyo mwelewa mleta mada sio kwamba anataka kukimbia bongo moja kwa moja,ila anataka awe mbali na nchi hii hata kama ni miaka kadhaa walau apate international exposure
Sasa hiyo ya kuolewa ni juu yake mwenyewe kama atakuwa ameamua.. Point yake yeye ni kwenda nje kupata exposure haijalishi kama huko atapata mafanikio au laKukimbia bongo au kutokimbia bongo ni yeye, kama anaona kuna maslahi aende tu, nadhani ndiyo maana anauliza hapa "AKABEBE BOX MAJUU"? Haya sasa wadau wamemwambia kuwa sku hizi maboksi wanabeba wenyewe, na yeye ana 7M hiyo pesa inatosha kupata return ticket tu na kubakiwa na chenji kidogo ya maziwa, unataka mwenzio akaolewe?!!
Wewe ndiyo haujanielewa, namaanisha huko kichwani kwako tayari kuna ujuzi wa kutosha, ukijumlisha na mtaji ulionao una nafasi nzuri zaidi ya kutoka hapa bongo kuliko unakotaka kwenda. BTW, naona wadau wengi tu wamekushauri, tena walioko huko unakotaka kwenda, NADHANI MPAKA SASA UMESHAFANYA UAMUZI!
Umenivunjia heshima kaka, nikaolewe tena kidume cha mbegu. Jitahidi kuwa muungwana ndugu.Kukimbia bongo au kutokimbia bongo ni yeye, kama anaona kuna maslahi aende tu, nadhani ndiyo maana anauliza hapa "AKABEBE BOX MAJUU"? Haya sasa wadau wamemwambia kuwa sku hizi maboksi wanabeba wenyewe, na yeye ana 7M hiyo pesa inatosha kupata return ticket tu na kubakiwa na chenji kidogo ya maziwa, unataka mwenzio akaolewe?!!
Umenivunjia heshima kaka, nikaolewe tena kidume cha mbegu. Jitahidi kuwa muungwana ndugu.
sijuwi kama nimekuelewa lakini nitakupa nilivyofahamu mimi
Majuu hukatazwi kuenda, watu wanakwenda kila leo na wengine wanarudi,
Suali ninalotaka kujuwa, unafanyakazi gani kwasasa? mil 7 ulizitengeneza vipi? nini malengo yako kimaisha ? una umri gani?
Kwenda majuu na kutengeneza pesa ni bahati, kwani maisha ya juu ni tofauti na ya kwetu, kiutamaduni silka na hata mila ziko tofauti,
wako watu walienda majuu kwa kuuza rasilimali ya familia kwa kutegemea akirudi atarudi na pesa ya uhakika, matokeo yake mpaka leo wameganda majuu hawana pesa na kurudi hawawezi,
Wako walioenda kwa masomo na kubaki huko mpaka leo bado wanajaribu kutafuta pesa bado hawajaipata
Kuna waliokwenda majuu " hawakupata pesa lakini walisoma maisha na kupata ujanja na kurudi nyumbani" maisha yao yamebadilika baada ya kurudi na ujanja sio pesa,
Kuna watu waliondoka na pesa ya uhakika kutoka bongo eti tu kwenda majuu wanashindwa kurudi kwani pesa imepotea na hawakupata kitu
Kuna waliokwenda majuu na kuwa na malengo wamerudi na pesa yao na ujanja wa majuu
Ninakuuliza tena nini malengo yako?
Habari gani wangugu?
Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k
Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..
Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.
Karibuni!!
Nisamehe MKuu, sikumaanisha kuolewa kwa maana ya ndoa, nimemaanisha majanga! Lakini kiutalii naona bado7M ni ndogo, na ukirejea nyumbani unaanza moja au? Nakushauri uizungushe, baada ya mwaka unaweza kuwa vizuri ukapata pesa ya kwenda kwa raha zako mkuu. NI MAWAZO TU!
Habari gani wangugu?
Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k
Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..
Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.
Karibuni!!
Mkuu, kama umehitimu shahada juzi tu na inategemea ni shahada ipi, basi ungafikiria kutunga business plan nzuri tu ya kuanzisha biashara ambayo ingekufanya uwe mjasirimali.
Unaweza kufikiria biashara yoyote ile ndogo ambayo kwa mtaji wa kiasi ulicho nacho wa 7m unaweza kwenda benki na kuomba uongezewe mtaji zaidi ili kuanzisha biashara yako.
Mwanzo ni mgumu lakini fikiria ni biashara ipi ndogo na rahisi kuanzisha ambayo itakupa kama 10m kwa mwaka kama alivosema mmoja wetu hapo juu.
Pili, unaweza kuanza kuingiza faida ndani ya miaka 2 au zidi na hapo ndipo unaweza kufikiria kwenda kupumzika katika nchi unazofikiria ambazo umezitaja maana ukienda sasa hivi na pesa hiyo ambayo haizidi hata dola 3000 unakuwa unatania.
Nchi ulizozitaja kwa sasa hazina jipya zaidi ya kuhakikisha zinawasaidia wananchi wao ingawa serikali za nchi hizo zinabana sana matumizi katika kutoa huduma kwa wananchi ambazo zinaitwa "cuts".
Hali hio imesababisha maisha kuwa magumu sana kwa mtu ambae hafanyi kazi achilia mbali yule ambae ndio kwanza ametia mguu ndani ya nchi hizo, kwani ni kweli unakaribishwa lakini kama kawaida, mgeni ni siku ya kwanza na pili lakini ya tatu ntakuonyesha "jobcentre" ukaanze kutafuta kazi ili uanze kunisaidia kulipa kodi ya nyumba.
Mwisho, kwenye suala la kutembea, ili ukajifunze wenzetu walivyoendelea inabidi sasa ufikirie kuhusu nchi kama China ambao huenda siku za karibuni watathibitihswa kwamba wameipita USA kiuchumi. Huko ndipo kuna kila nafasi ya kutengeza mawasiliano na developers wa mawazo yako ya kuanzisha biashara au ubunifu iwe hata mashine ya kuharibu visima vya uzalishaji mbuu pale Daesaama.
Graduate, umesoma kwa kodi zetu, tumekufundisha uzalendo na mengineyo kweli unawaza kuzama nje na kufanya kazi za vibarua
Fursa zote zilizopo hapa za kufuga nyuki, kilimo cha mpunga mahindi pamba nk
Hapa nina wacwac na huo ugraduate wako
si kila mtu amesoma kwa kodi zako wengine hatujawai kula kodi yako ata sh 1