Niishi nae vipi huyu mwenza

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,431
5,073
Napata wakati mgumu katika mazungumzo yetu.

Yani sio muongeaji kabisa, hadi mimi ndo niulize au nianzishe mada, ukimuuliza swali hasa la msingi anaweza akachukua ata sekunde 20 yuko kimya ndo ajibu, au asikujibu kabisa akwambie atakujibu siku nyingine. Kuna muda anasema kabisa kua sijakumisi bado.

Nahisi yuko tofauti sana na binadamu wengine anaishi ulimwengu wa kivyake vyake. Pia hii inanifanya nisiwe sure kama ananipenda au la. Muda mwingi mimi nakua ndo mzungumzaji na kutawala mazungumzo.

Kuna muda ukimwambia kua hua namfikiria sana anasema kwani sina marafiki wa kukaa nao kuongea. Sasa sijui ananibagua au ndo mtu wa vipi. Ananipa ugumu sana kumzoea.

Ni mara chache sana mtaongea nae aanzishe mada lakini hazizidi sana.
Hataki sehemu yenye watu wengi
 
Shida inakuja pale Senguine Extroverted anapodate na Meliconile Introverted..Mkuu haya mambo ya Personalities yana effects kubwa kwenye mahusiano ya watu. Kama unaona hutaweza kumvumilia bora umuache atapata wa kufaana nae.. Kumbuka personality sio Behaviour ambayo unaweza badirisha..
 
Maybe tatizo ni hili







Amechoka story....if you know what i mean
 
Shida inakuja pale Singuine Extroverted anapodate na Meliconile Introverted..Mkuu haya mambo ya Personalities yana effects kubwa kwenye mahusiano ya watu. Kama unaona hutaweza kumvumilia bora umuache atapata wa kufaana nae.. Kumbuka personality sio Behaviour ambayo unaweza badirisha..
Sijakuelewa mkuu kuna maneno umetumia ni mageni kwangu,
 
Sijakuelewa mkuu kuna maneno umetumia ni mageni kwangu,
Kwa ufupi ni kua.. Personalities za binaadamu zimegawanyika makundi mawili ambayo ni Extrovert (Waongeaji) na Introvert (wakimya )

Hayo makundi mawaili nayo yamwgawanyika makundi mawili mawili na kila kundi lina binaadamu wenye sifa tofauti na kundi lingine
 
Huyo ni mimi kabisaa!
Kuna mambo ya msingi sana ya kuongea na kuyafanyia utekelezaji, mambo ya kusema I miss you too hebu waachie watoto wa secondary mkuu!!

Sijui nazeeka mimi jamani!!
mbona yeye si mtu mzima ?
 
Kwa ufupi ni kua.. Personalities za binaadamu zimegawanyika makundi mawili ambayo ni Extrovert (Waongeaji) na Introvert (wakimya )

Hayo makundi mawaili nayo yamwgawanyika makundu mawili mawili na kila kundi lina binaadamu wenye sifa tofauti na kundi lingine
inaonekana ni field pana. Nisaidie tu tips kama zipo
 
inaonekana ni field pana. Nisaidie tu tips kama zipo
Psychology ni field pana mno..maana ndio imebeba na kugusa kila nyanja ya maisha na mazingira ya binaadamu.. Psychology ndio sayansi yenyewe..Kwa muonekano mpenzio yupo kundi hili lenye sifa hizi...
MELANCOLIN

Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo;

- Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
- Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
- Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
- Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
- Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati

- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)

Sifa zao nyingine ni pamoja na;

- Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
- Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine

- Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)

- Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasani si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)

- Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)

- Wakata tamaa wanapokosolewa.
- Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.

Nyinginezo ni;

- Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)

- Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.

- Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
- Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao

- Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa).

- Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.

- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.

- Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.

- Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani

Pia, wanafahamika kwa;

- Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)

- Wana busara na hekima nyingi
- Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
- Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
- Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
- Ni kundi la watu wanoridhika haraka

- Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa.

- Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.

- Kundi linalopenda amani na utulivu
- Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto

- Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu.

Wana sifa nyingi sana, nyinginezo ni;

- Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa

- Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
- Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
- Wakati mwingine hupenda kujikataa.
- Ni waaminifu na wasema ukweli
- Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
- Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
- Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu

- Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick

Kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani].

- Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}

- Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua.

Mifano ya watu wa kundi hili: Musa (wa biblia) Yesu Kristo, Bob Marley, Celin Dion.
 
Najiona mimi kabisa.

Nashukuru nilie nae ananielewa.

Sio maringo ndivyo tulivyo, na tunapenda kweli. Kama wewe muongeaji, kiguu na njia, mtu wa outings basi hamtawezana.

Kuna ndugu hapo juu kaongelea mambo ya Extroverts na Introverts yuko sahihi sana. Kuna wakati nilijiona kituko mpaka nilipoyasoma soma hayo maswala mtandaoni ndio nikajiona na mimi ni binadamu sio kituko.

Mko dunia mbili tofauti, either join him/her au sepa. You cant fight


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napata wakati mgumu katika mazungumzo yetu.
Yan sio muongeaji kabisa, hadi mimi ndo niulize au nianzishe mada, ukimuuliza swali hasa la msingi anaweza akachukua ata sekunde 20 yuko kimya ndo ajibu, au asikujibu kabisa akwambie atakujibu siku nyingine. Kuna muda anasema kabisa kua sijakumisi bado.
Nahisi yuko tofauti sana na binadamu wengine anaishi ulimwengu wa kivyake vyake. Pia hii inanifanya nisiwe sure kama ananipenda au la. Muda mwingi mimi nakua ndo mzungumzaji na kutawala mazungumzo. Kuna muda ukimwambia kua hua namfikiria sana anasema kwani sina marafiki wa kukaa nao kuongea. Sasa sijui ananibagua au ndo mtu wa vipi. Ananipa ugumu sana kumzoea
Ni mara chache sana mtaongea nae aanzishe mada lakini hazizidi sana.
Hataki sehemu yenye watu wengi
Mchunguze anapenda Mambo gani vitu vipi anapenda kuvifatilia,Basi kuwa unavidokoa atafunguka tu.. mpe nafasi ya kuwa pekee pale anapotaka kuwa hapo anajichaji mwenzio!!
Huenda bado anahitaji muda wa kukusoma zaidi na akija kuzama zaidi usimtese!!
Muelewe vile alivyo,usimkere endelea kumpa nafasi yake Kama wewe navyostahili.
Shida inakuja pale Senguine Extroverted anapodate na Meliconile Introverted..Mkuu haya mambo ya Personalities yana effects kubwa kwenye mahusiano ya watu. Kama unaona hutaweza kumvumilia bora umuache atapata wa kufaana nae.. Kumbuka personality sio Behaviour ambayo unaweza badirisha..
Mkuu kitabia hivi ndivyo inavyostahili ni couple inayoshibishana,yani inaziba mapungufu ya mwenzake na wanaweza kudumu muda mrefu zaidi! Chamsingi wanatakiwa wajuane tu..
Introvert wanamtindo wa kudge maamuzi waliyofanya kama Ni sahihi au bado!! Na pia wanamtindo wa kusubiri mahusiano na yakifika wanaruka!!😜😜
Kajamaa kavumilie tu ila kama ni ka Sanguine katapata tabu kidogo maana huwa havitulii vinamchecheto! Na havijui kutunza mambo si unajionea kimekuja kulalama hapa!! Ila mwenzake unakuta yupo cool kabisa hana kelele😜😜
 
Back
Top Bottom