Free ideas
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 3,508
- 2,058
- Thread starter
-
- #241
Ni Matatizo ya watu wanaokariri umesahau tu, wewe ni mmoja wa wanatumia maswali kujibu maswali...
Mi huwa sikariri bali natumia akili na pia nafikir kwamba nini ni nn.siko kama wewe mkuu ulichoambiwa ndo hicho hicho unakomalia mpka leo.toa uoga kijana usitishwe na maneno ya watu.
Kwa nini unafikiri ujuzi kwamba Mungu ndiye aliyeumba Ulimwengu na vyote vijazavyo na ndiye archtecture , designer,Engineer, Artist, na mathematician aliyeweka Constant zote ni kutokana na UOGA ? UOGA wa jambo gani ? natishwa na NANI ? kweli kauli kama hizi hazitokani na kukariri ?
Mwanadam pale anapofikiri/anapowaza kushindwa ndo anapomuumba mungu.,nilishasema katika uz flan kwamba HAKUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KUONESHA UWEPO WA MUNGU,NA MIMI NAJUA HAYUPO,so kama we unaamini yupo lete ushahidi kithibitisha hapa
Hujielewi, unapimaje kwamba ushahidi kuhusu kitu fulani ni wa kutosha au lah ? unahitaji aina gani ya ushahidi ? huwezi kujibu swali hili kama ilivyokawaida yako,japo nina hakika hujielewi.
Angalia hoja uliyo quote hapo juu ? umezungumzia kuhusu Uoga na unazungumzia mara nyingi,umeulizwa Uoga utokane na nini,na Uoga uwe ni kwa jambo gani ? badala ya kujibu kama ulivyoulizwa umekuja na kushusha kariri zako, Pseudoscientist hujielewi tu...
Mkanganyiko na sio kidogo Mkuu, ni watu wengi ikiwemo hata mimi kwa kipindi kirefu niliamini kwamba Lucifer ina muwakilisha IBILISI, Lakini baada ya kupitia maandiko mbalimbali na maelezo mengi ya namna kuisoma Biblia na Kuelewa ndiyo nilipoweza nami kupata ufahamu wa kwamba kumbe ni makosa ya kifasiri tu,Chanzo cha Mkanganyiko ni maandiko yaliyomo kwenye Kitabu cha Isaya 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! (KJV)
Kweli Ibilisi ndiye Nyota ya asubuhi ?
Tukiyachunguza maandiko vizuri tutaona kwenye ufunuo 22:16 ''Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi''
Hivyo Bwana Yesu Mwenyewe alijitambulisha kwamba yeye ndiye Nyota yenye Kung'aa ya asubuhi.
Yapo maandiko mengine ambayo yanathibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Nyota ya asubuhi.
2 Petro 1:19 19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Ufunuo wa Yohana 2:28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
Ni wazi kwamba Nyota ya asubuhi ni sifa ambayo ni ya kipekee kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kamwe haiwezi kuwa ni sifa ya Shetani/Ibilisi.
Kiini cha mkanganyiko.
Mkanganyiko umetokana na maelezo yanayopatikana katika tafsiri ya Biblia ya KJV Isaya 14:12 (Hasa katika Kiingereza ambapo limetumike neno LUCIFER) kama ilivyoelezwa hapo juu, Neno Lucifer limetumika kama utambulisho wa nyota ya asubuhi,ikiwa ni katika maelezo ambayo ukiyasoma kwa haraka unaweza fikiri yanamzungumzia IBILISI na kumpa sifa ya Nyota ya asubuhi. Hasa ukisoma Isaya14:12 kama ulivyo.
Isaya 14:12-15
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Ukiisoma maandiko haya kwa makini utagundua si kweli kwamba shetani anapewa sifa na ukuu wa kwamba yeye ni Nyota ya Asubuhi bali ni lugha ya ''Kebehi'' dhidi ya majikwezo ya IBILISI,na kujipa sifa kwamba yeye ni LUCIFER (Nyota ya Asubuhi) na inaonyesha jinsi ambavyo kujikweza kwake kumedhiriwa hadi kushushwa chini mpaka kuzimu,wakati alijinasibu kuwa yeye atapaa kupita vipimo vya mawingu na kuwa sawa na aliye juu!
Ukitambua kwamba Lugha ilikuwa si kumsifia Ibilisi bali kubeza kujikweza kwake na kujipa sifa asizokuwa nazo utagundua kwamba bado matumizi ya neno LUCIFER kwamba ni Ibilisi yanakinzana na ukweli, kwamba alijiita LUCIFER kujikweza tu,lakini kiukweli hana sifa hizo hata chembe.
Mkuu ngoja nami niseme neno hapa kuhusiana na hii kitu
Kwanza nakubaliana na wale wanaosema kuwa Lucifer ndie ibilisi kwasababu zifuatazo
Kwanza Lucifer ni neno lililotokana na neno la kilatini lenye maana ya "mwenye nuru" au "aliyetiwa nuru".Jina hilo alipewa wakati bado ni malaika mbinguni na alikuwa ni kinara wa sifa na alikuwa ni mwenye kutoa nuru kweli.Alipokokosa ule ukinara wake aliokuwa nao huko mbinguni wa uimbaji aliondoka nao lakini akawa hana tena ile nuru lakini hiyo haikubadilisha kuwa ndie Lucifer
Nikija kweye hiyo mista ri uliyoi quote iko hivi;
Isaya 14:12 inasema:
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
Na ufunuo 22:16 inasema;
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
Mkuu hapo kuna maneno haya "ile nyota ya kung'aa ya asubuhi" ambayo ni maneno ya Yesu na "Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi".Hayo maneno yana maana tofauti na hayazungumzii kitu kimoja
Asubuhi ni tofauti na alfajiri
Lakini pia kuna kitu wengi hawakioni hapo,ambacho hawakioni hapo ni hiki "mwana wa subuhi" Lucifer ametajwa kuwa ni "mwana wa asubuhi" kwasababu Yesu ambae ni nyota ya asubuhi ndie aliyemuumba Lucifer ndio maana anaitwa hivyo
Lucifer kuitwa nyota ya alfajiri kuna maana kuwa sio nyota ya subuhi,Nyota ya alfajiri iko na inajulikana jina lake nadhani ni venus [sina uhakika] na nyota ya subuhi ni jua
Lucifer anaitwa nyota ya alfajiri na Yesu nyota ya asubuhi kwakuwa ni kweli Lucifer ana nuru [kama ilivyo nyota ya asubuhi [venus] na Yesu nae ana nuru lakini ni kuzidi ile ya alfajiri [Jua]
Hiyo ni rahisi kujulikana kwasababu Jua lina nuru kuliko nyota,lakini zaidi sana nyota nazo zinatoa nuru kutoka kwenye jua hivyo kuthibitisha kuwa ni mwana wa asubuhi kwakuwa kwanza bila Yesu hakuna nyota kwamaana ya uumbaji lakini pia bila Yesu hakuna nyota kwamaana ya nyota kutoa mwanga wake kwenye jua
Kwa kifupi uwepo wa nyota unategemea uwepo wa jua,kwa maneno mengine uwepo wa Lucifer unategemea amri ya Yesu
Kwa ufafanuzi huo mdogo nadhani nitakuwa nimeeleweka kwa kiwango cha kutosha
Ubarikiwe
CC: Kaunga , MaxShimba , @Shlendler Stefano Mtangoo !!
I stand to be corrected!
Ungejielewa usingekuwa unauliza maswali na kutaka ujibiwe kama unavotaka.huku hutaki kusema unachodhan n sahihi.we ndo hujielewi na hujui kama hujielewi.,waweza niita vyovyote lakini haibadilishi ukwel
Yote haya umetumia fikra zako tu?
You are so geneous! Bravo mkuu!
Tatizo kwangu ni pale ambapo LUCIFER inatumika kama ndiye kwa kujiita yeye mwenyewe kwamba ndiye Nyota ya alfajiri,mwana wa asubuhi ! lakini ukisoma Isaya 14:12, Isaya hakuwa anamsifia huyo Nyota ya Alfajiri bali alikuwa anamkebehi kwa kujikweza kwake na namna alivyoshuhshwa hadi kuzimu, mantiki ya kujiita Lucifer ilikuwa ni kujipa sifa za Yesu,hivyo kukosekana kwa neno Mwafaka la Kiingereza ndiko kulikopelekea neno LUCIFER kwa maana yake halisi ya Mwenye NURU ama ALIYETIWA NURU Huyu mwenye sifa hizi ni Yesu Kristo,hasa hilo ndilo ninalomaanisha.
''Kwanza Lucifer ni neno lililotokana na neno la kilatini lenye maana ya "mwenye nuru" au "aliyetiwa nuru".Jina hilo alipewa wakati bado ni malaika mbinguni na alikuwa ni kinara wa sifa na alikuwa ni mwenye kutoa nuru kweli
Nime koleza hapo kwa kuwa ni mazoea yaliyo mfanya Ibilisi aitwe Lucifer si kwamba ni Jina la Kupewa toka alipoasi,kilichotokea baada ya mkanganyiko wa matumizi ya neno kwenye Isaya 14:12, baadhi ya machapisho yalianza kuacha kutumia neno Devil/Satan na kutumia Lucifer badala yake.
Ni vema tutafakari pamoja na kusahihishana ili baadae tuelewana na kutumia kwa kadri ya jina husika.
Ki ukweli bado sijasawishika na mawazo au muamala wowote kuhusu hili la freemason kuwa si dini ya mashetani! Nikwanini ukitaka kujiunga cha kwanza kabisa unapewa zawadi ya gari aina ya VOLKSWAGEN? PILI. mambo yao ni ya siri mnoo kuliko mashirika au magroup yeyote ya utajiri duniani?
Pseudoscience is any belief system or methodology which tries to gain legitimacy by wearing the trappings of science, but fails to abide by the rigorous methodology and standards of evidence that demarcate true science. Although pseudoscience is designed to have the appearance of being scientific, it lacks any of the substance of science.
Promoters of pseudoscience often adopt the vocabulary of science, describing conjectures as theories or laws, often providing supposed evidence from observation, expert testimonials, or even developing what appear to be mathematical models of their ideas. However, in pseudoscience there is no real honest attempt to follow the scientific method, provide falsifiable predictions, or develop double blind experiments. Pseudoscientists often use the tactic of cheating the scientific method.
[TABLE="class: toc"]
[TR]
[TD]cc Rational Wiki
Labda ukisoma hapa utajielewa wewe ijiitaye mwanasayansi unayejibu maswali kwa kuuliza maswali.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mkuu hawa jamaa hutoa kafara hata binadamu mkuu! Unaukumbuka ushuhuda uliotolewa na yule mchungaji baada ya Kanumba kufariki? Pia nina ushuda wa binti aliyekuwa akituumikia Freemason kwa kipindi kirefu? Kama unatumia whtsap nipe namba umsikilize huyu afu uniambie kwanini unadai freemason hawahusiki na utoaji kafara wa binadamu je nikweli
Mkuu,
Kuna mambo ambayo napenda uyafahamu
1:Lucifer ni jina la Shetani,naomba ujue tu kuwa Shetani sio jina bali ni sifa kama ilivyo Mungu,huyu mwenye sifa ya Shetani ana jina lake ambalo ni Lucicer,najua aunafahamu kuwa Mungu nae ana jina lake
2:Shetani hakujiita hivyo bali hilo ni jina lake alilopewa na Mungu
3:Shetani kuitwa mwenye nuru hakumpunguzii kitu Yesu,hawa wote ni wenye nuru ila kuna mmoja ni nuru zaidi na ni chanzo cha mwingine,rejea maelezo yangu hapo juu utaona ni nani chanzo au sababu ya mwingine kuwepo
4:Nilikuambia kuwa kuna tofauti kati ya alfajiri na asubuhi,lakini zaidi sana nilikuambia kuwa nyota ya asubuhi ni venas na ya asubuhi ni Jua,haya yote yametumika kuwawakilisha Shetani na Yesu na hivyo viwili vinathibitisha ni kipi kinamtegemea yupi katika uhai
Lakini pia nikakuambia kuwa Shetani anaitwa mwana wa asubuhi kwakuwa aliumbwa na Yesu,nadhani unajua vile ambavyo nyota zinategemea uwepo wa jua kuwepo
Kwa hiyo hakuna makosa yoyote yale Shetani kuitwa au kujiita Lucifer kwakuwa ndio jina lake!
Mkuu,
Kuna mambo ambayo napenda uyafahamu
1:Lucifer ni jina la Shetani,naomba ujue tu kuwa Shetani sio jina bali ni sifa kama ilivyo Mungu,huyu mwenye sifa ya Shetani ana jina lake ambalo ni Lucicer,najua aunafahamu kuwa Mungu nae ana jina lake
Nimetoa maelezo ya neno LUCIFER kuandikwa mara moja tena kwenye Biblia ya KJV na chanzo cha kutumiwa neno hilo nimeeleza Mkuu.
Ama kuhusu Shetani kuitwa Lucifer nje ya mkanganyiko wa matumizi ya neno Lucifer kwenye Isaya 14:12 nakiri kwako kwamba sijui na sijawahi kusoma popote.
2:Shetani hakujiita hivyo bali hilo ni jina lake alilopewa na Mungu
Kwa kadri ya uchunguzi,pamoja na kujulikana kupitia Isaya 14:12 kwamba Shetani aliitwa Lucifer kutokana na kujisifu kuwa ni mkuu hana aliye mkuu chini hata juu,japo kwa kurejea Isaya 14:4, tunaona Isaya allitumwa kutengeneza Methali kwa ajili ya Mtawala wa Babeli aliyekuwa na majivuno na kiburi dhidi ya Mungu. Hivyo yawezekana sana kwamba Lucifer aliyekuwa anazungumziwa na kukebehiwa kwa mafumbo na Nabii Isaya ni Mtawala wala Babeli,binadam mwenye mwili na si Shetani.
3:Shetani kuitwa mwenye nuru hakumpunguzii kitu Yesu,hawa wote ni wenye nuru ila kuna mmoja ni nuru zaidi na ni chanzo cha mwingine,rejea maelezo yangu hapo juu utaona ni nani chanzo au sababu ya mwingine kuwepo
4:Nilikuambia kuwa kuna tofauti kati ya alfajiri na asubuhi,lakini zaidi sana nilikuambia kuwa nyota ya asubuhi ni venas na ya asubuhi ni Jua,haya yote yametumika kuwawakilisha Shetani na Yesu na hivyo viwili vinathibitisha ni kipi kinamtegemea yupi katika uhai
Yah, Mkuu kwa kutafsiri neno Morning,kiswahili unaweza kusema Alfajiri au asubuhi na ukawa sahihi kwa tafsiri zote.
Lakini pia nikakuambia kuwa Shetani anaitwa mwana wa asubuhi kwakuwa aliumbwa na Yesu,nadhani unajua vile ambavyo nyota zinategemea uwepo wa jua kuwepo
Kwa hiyo hakuna makosa yoyote yale Shetani kuitwa au kujiita Lucifer kwakuwa ndio jina lake!
Mkuu nashauri tuendelee kuchunguza maandiko, ili tujue ukweli usio na mawaa, lakini kumbuka nimeeleza hapo juu kwamba Neno Lucifer limeandikwa mara moja tu ndani ya Biblia,tena kwenye Biblia tafsiri ya KJV kwenye Isaya 14:12 tu. Labda kama kuna sehemu nyingine ambayo unajua Ibilisi au Shetani ameitwa Lucifer nitafurahi kujifunza...
MAPUNGUFU NILIYOYAONA/HOJA ZISIZO ELEWEKA KUTOKA KWA FREE IDEAS.
1) "Nimekuwa nikijaribu kila wakati kufikiri na kufanya tafiti kwa kutumia akili binafsi bila machapisho wala vitabu rejeaa ma msaada hadithi za kusimuliwa,"
Rejea mwanzoni kabisa mwa thread yake, amekiri kutokutumia VITABU, REJEA, wala Hadithi za kusimuliwa.
2) "Free Mason ama wajenzi huru,ni jamiii ama kikundi ambacho kina misingi toka zaman sana enzi za mfalme solomon,"
Ulipataje kuigundua enzi ya mfalme solomoni bila kusimuliwa ama kusoma?, Je uliishi katika enzi hiyo?
3) "hakuna kitabu cha masonic rules kinachoeleza wazi kwamba hakuna mungu,ila rules zoa zinaonesha misimamo na personal charachters za mwanadam ambazo hazina uhusiano na kisichoonekana."
Hivi vitabu vyao umevisomea wapi wakati research hii ilikua ni ya kutokuhitaji reference yoyote isipokuwa uwezo wako binafsi wa kufikiria?
4) "na kwa imani na plan zao utatimia kabla ya mwaka 2040,lengo lao ni kuona watu wote wanakuwa kitu kimoja na kuunda umoja mahal pote katika uso wa dunia"
Hizi plan zao umezisomea wapi mkuu? kwa sababu hukuwa na haja na reference yoyote, ama unataka kutudhihirishia umeweza kuishi maisha ya mbeleni zaidi(2040) kisha ukaona utekelezaji wa matakwa yao?
NB: Hizo ni baadhi ya mada zilizonifanya nishindwe kuielewa Hoja kuu ya ndugu Free ideas.