Sante! Urahis wa maisha upo kivip au ndiyo vile chakula na nyumvmba cheap kumbe hamna mzunguko wa pesa.. !
Labda nitumie kiswahili lugha imekuchanganya
Ninaposema opportunities nilimaanisha kuna fursa nyingi za kumuingizia mtu kipato endapo ataamua kuzitumia hizo fursa.
Kwa upande wa maisha nayo yako chini pamoja na mzunguko wa pesa kuwa mkubwa bado maisha si ghali kwa ujumla wake si chakula,nyumba na mavazi pia,yaani ile basic needs utazipata kwa gharama ndogo sana mbeya
Mbeya fursa za kibiashara ni nyingi inategemea na interest yako ww iko upande upi,kama unapenda biashara ya mazao ule mkoa ndo ghala la chakula,na ni mkoa ulio mpakani mwa Zambia na Malawi hapo mbeya utafanya biashara na wakongo,wazimbabwe,wazambia,wamalawi na ata waafrika kusini.kwenye boda pale Tunduma au bora ya Malawi Kule kyela
Lakini pia umezungumzia uzoefu wa tours hii pia ni opportunity ambayo IPO siku hizi mbeya kuna Songwe international airport ndege za kimataifa zimeanza kutua pale na wageni kila kukicha wanaingia pale mbeya kwa ajili ya kutembelea vivutio vilivyo nyanda za juu kusini,mbeya pana kampunii nyingi za tours
Ningekushauri kabla ya yote nenda kwanza kafanye survey kidogo kaa ata wiki then uje uende arusha ukae wiki nako
Naamini baada ya hizi survey utapata jibu sahihi kabisa
Nikutakie kila lakheri katika safari yako yakuhamisha makazi