Nigeria: Matukio ya utekaji bado ni mwiba kwa wananchi

Nigeria: Matukio ya utekaji bado ni mwiba kwa wananchi

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Afrika taabu sana aisee!

Watu wenye silaha wamevamia Kijiji cha Chacho kilichopo jimbo la Sokoto, kaskazini magharibi mwa Nigeria, na kuwateka Wanawake 13, akiwemo mtoto mdogo.Utekaji huo ulitokea usiku wa Novemba 29, na umeongeza hofu miongoni mwa wakazi kutokana na ongezeko la matukio ya utekaji nyara katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mashuhuda wameripoti kuwa watekaji walivamia nyumba moja na kuwachukua kwa nguvu watu waliokuwemo ndani.

HABARI-Watu wenye silaha wamevamia Kijiji cha Chacho kilichopo jimbo la Sokoto, kaskazini maghar.jpg


Aidha, ripoti nyingine zinaonyesha kwamba wanafunzi wa shule kadhaa kaskazini mwa Nigeria pia wamekuwa wahanga wa utekaji, ambapo makundi ya kihalifu hufanya utekaji kwa lengo la kupata fidia au kudai malipo kutoka kwa familia zao.Kijiji cha Chacho kimeripotiwa kushambuliwa mara kadhaa na makundi ya kihalifu yenye silaha yanayojulikana kama “Habints.” Inaelezwa kuwa mwezi Oktoba mwaka huu, watu 13 walitekwa na kulazimishwa kulipa fedha ili kuachiwa huru.

Matukio ya utekaji yamekuwa tishio kubwa katika kaskazini mwa Nigeria, ikiwemo utekaji wa raia na wanafunzi kwa ajili ya fedha na mali nyingine.Kukabiliana na hali hiyo, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, hivi karibuni alitangaza hali ya dharura ya kiusalama, huku akiahidi kuongeza idadi ya vikosi vya usalama na kutoa ajira mpya katika vyombo vya ulinzi ili kudhibiti matukio hayo, hatua ambazo makundi ya haki za binadamu na Wananchi wanazilalamikia wakieleza kuwa haziendani na ukubwa wa tatizo
 
Back
Top Bottom