Nifanyeje niwe na uelewa mdogo?

Nifanyeje niwe na uelewa mdogo?

Yaani kuwa na uelewa wa mambo mbambali ni mateso makubwa hasa kwenye nchi ya Tanzania nimegundua watu wenye uelewa mdogo wa mambo (ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi) wana raha kubwa sana na wanafurahia maisha vizuri, yaani kwao bora liende hawajui chochote kinachoendelea.

Kuna mambo mengi makubwa yanatokea tena yakuogopesha kwa mtu mwenye kufikiri vizuri, lakini wenzagu wenye uelewa mdogo wala hawapati machungu yoyote yale maisha kwao yanasonga mbele kama vile hakuna kinachotokea, kiufupi wenzagu raha wanayo.

Sasa naomba mnipatie mbinu ya kuondoa uelewa wa kutafakari na kuchambua mambo, ili niwe kama zezeta fulani na mi nifurahie maisha.
Nimeona njia pekee ya kufurahia maisha apa Bongo ni kuwa na uelewa mdogo wa mambo.
Huna haja ya kufanya chochote.
 
Inaonekana una jali sana kuhusu jamii na nchi yako,
Nilikuwa nawaza kuhusu haya masuala ya wabunge kuleta maendeleo finyu na wannchi kuwachagua kila mara nikawa nawasikitia, ila sasa hata wakifa sijali, dunia ina matatizo na mimi sio mtu wa kuya solve
mimi nilikuwa hivyo zamani ila kwa sasa nilishajijenga vizuri, sijali sana kuhusu kinachotokea kwa watu wengine as long as nipo okay
 
Bangi ni msaada mzuri sana kwako, vuta kutwa Mara tatu na shushi viwili kutwa Mara sita..baada ya hapo leta mrejesho na ukikaa kimya tutajua tumefanikiwa tiba yetu...
 
Yaani una uelewa mkubwa lakini bado unashindwa kutumia huo uelewa wako ku-solve tatizo lako mwenyewe tena in downward movement!!
 
Yaani una uelewa mkubwa lakini bado unashindwa kutumia huo uelewa wako ku-solve tatizo lako mwenyewe tena in downward movement!!
teteheee,wengine tunaweza kwa upward movement
 
1. Achana na JF
2. Acha kusikiliza na kuangalia taarifa za habari na kusoma magazeti
3. Acha kabisa kufuatilia current events zozote zile
4. Shinda Instagram na uwafuate wasanii wa bongo fleva na bongo movie
5. Tafuta team ya kujiunga nayo - kama team Wema, team Mondi, team Kiba, n.k.

Hayo yote sio dawa kwa sababu bado ataongea na watu, atatembea, na kupata huduma mbalimbali. Hivi namba 4 na 5 hazimfanyi mtu afikirie? Kuna mambo mengine hayawezi kuwa reversed; mfano, kuongezeka kimo.
 
Nenda kafanye operation ya kichwa. Wakupunguze ubongo utakuwa na uelewa mdogo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hayo yote sio dawa kwa sababu bado ataongea na watu, atatembea, na kupata huduma mbalimbali. Hivi namba 4 na 5 hazimfanyi mtu afikirie? Kuna mambo mengine hayawezi kuwa reversed; mfano, kuongezeka kimo.
Hivi katika dunia hii kweli ikosekane dawa ya kupunguza IQ?
 
Naongelea uelewa mkubwa,,lakini sio ule wa level ya gineus.
Sawa mkuu,mimi nilifikiri kuwa unatutishia tu!......Kumbe kule kwenye jukwaa la greater thinkers watu wenye uelewa mkubwa ni watu wadogo sana wala hawatakiwi kule! 🙂
 
Sawa mkuu,mimi nilifikiri kuwa unatutishia tu!......Kumbe kule kwenye jukwaa la greater thinkers watu wenye uelewa mkubwa ni watu wadogo sana wala hawatakiwi kule! 🙂
namaanisha nina uelewa mkubwa lakini sijafikia level ya kule jukwaa la greater thinkers.
 
Mkuu kuanzia namba moja hadi tatu uko sahihi na utamsaidia kwa hii shida yake.
Namba nne na tano ataongeza maarifa ya upande wa pili, atabobea huko kwenye ma team na umbea ambayo nayo itamsumbua. Kwa ufupi yeye hataki apate shida na kitu anachokifaham. Akaishi porini kwa watindiga na wadzabe!!

Aliyekwambia Wahadzabe na Watindiga ni wajinga ni nani?
 
Aliyekwambia Wahadzabe na Watindiga ni wajinga ni nani?

You completely missed my point, hao sio kwamba ni wajinga, hataweza kuelewana nao kwa chochote atakua na maisha yake na wenyewe wanaendelea na maisha yao.
 
You completely missed my point, hao sio kwamba ni wajinga, hataweza kuelewana nao kwa chochote atakua na maisha yake na wenyewe wanaendelea na maisha yao.
Naona una point ya msingi
 
Yaani kuwa na uelewa wa mambo mbambali ni mateso makubwa hasa kwenye nchi ya Tanzania nimegundua watu wenye uelewa mdogo wa mambo (ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi) wana raha kubwa sana na wanafurahia maisha vizuri, yaani kwao bora liende hawajui chochote kinachoendelea.

Kuna mambo mengi makubwa yanatokea tena yakuogopesha kwa mtu mwenye kufikiri vizuri, lakini wenzagu wenye uelewa mdogo wala hawapati machungu yoyote yale maisha kwao yanasonga mbele kama vile hakuna kinachotokea, kiufupi wenzagu raha wanayo.

Sasa naomba mnipatie mbinu ya kuondoa uelewa wa kutafakari na kuchambua mambo, ili niwe kama zezeta fulani na mi nifurahie maisha.
Nimeona njia pekee ya kufurahia maisha apa Bongo ni kuwa na uelewa mdogo wa mambo.
Hadi hapo nahc huna uelewa mkubwa maana ungekua na uelewa mkubwa ungeisha jiongeza kitambo
 
Iyo ni njia ya kuelekea kwenye ukichaa ,,sitaki kuingia kwenye ule utafiti wa 4:1
Basi tambua hili: Kila mtu aliye hai lazima awe na stress..hakuna mwenye furaha siku zote..
Kuna wanaoteswa na siasa,,mapenzi,, mziki (tm kiba na mond)...umaskini na kadhalika...so hiyo ni hali ya kawaida
 
Back
Top Bottom