Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
980
1,085
Wakuu kwema?

Kuna jambo limekua likinitafuna kwa miaka mingi saana kuhusu mimi na mama yangu sina hata chembe ya upendo nae ila hela namtumia namsaidia kwa maana ni Maskini samahani kwa kusema hivi.

kwa kifupi kabisa mimi nimetoka kwa mama yangu nikiwa na umri wa miaka 3 nakuja kuonana na mama yangu nikiwa na umri wa miaka 19 kwa kipindi chote hicho mama yangu sikuwahi kumuona wala kusikia sauti yake siku nakutanishwa nae nilishindwa kufahamu mama mkubwa ndo alinitambulisha.. hakuwahi kunilipia ada, hakuwa kunipa hela ya yoyote .

Mimi nimelelewa na Bibi yangu na baba nampenda saana bibi yangu kuliko mama yangu mama yangu huwa ananipigia simu analalamika kwa nini simpigii simu? nakosa cha kumjibu namuomba tuu msamaha natamani kumpenda ila nashindwa naombeni msaada kama naweza kuwa na upendo na mama yangu

Asanteni.
 
Pole sana Mkuu
 
Pole sana
 
Sio kwamba humpendi bali hamna bond ya mama na mtoto kati yenu, na hiyo ni sababu ya distance iliyokuwepo katika kipindi chote cha ukuaji wako.

Kwa hiyo hamna cha ajabu hapo, bibi aliekulea kwako atakua na ukaribu zaidi kuliko mama mzazi.

Kwa hiyo futa kauli ya kwamba humpendi.

Wamama wanapitia mengi muda mwingine wanachukua maamuzi magumu ya kuacha watoto nyuma.
 
Kumpenda mtu ni hisia "Feeling" wewe huna hisia na Mama yako coz hakuishi na wewe,huna hisia nae,

Inaonekana kulikua na matatizo kati ya Baba yako na Mama yako,bila shaka waliachana ukiwa mdogo sana,

Sasa,ugomvi wa wazazi wako,wewe haukuhusu,hakuna umuhimu wa wewe sasa hivi kujua nini hasa kilitokea,kua karibu na Mama yako na utaanza kua na hisia nae kisha utampenda,kama una kwako,mchukue Mama yako uishi nae,kumtumia tu hela haitoshi,mzazi huhitaji upendo toka kwa mwanae,

The way utakavyodeal na Mama yako basi tegemea na watoto wako watadeal na wewe hivyo hivyo,bado hujachelewa,do something ili uwe karibu na Mama yako,upendo utakuja wenyewe tu,it's a self control.
 
Kuna watu wamezaliwa hawawajui mama zao!. We leo hii unamchukia mama ako na husemi chanzo ni nin mpaka kumchukia we una matatizo binafsi ndugu!..

Au maelezo hayajakamilika kuna jambo hutaki Kuliweka sawa ila sio kumchukia maza kisa hujaishi nae kwa muda mrefu
 
Ukweli Ni kuwa kuzaa tu hakusaidii hakikisheni mnatoa huduma na upendo Kwa watoto ....

Huyu jamaa alikosa upendo WA mama katika makuzi yake ,Hana hisia wala ukaribu na mama yake ..

Kiufupi Yuko sawa kabisa .....

Na hili ndio kizazi kinachokuja Kwa sasa ...

Wazazi wengi Ni wapuuzi ,wanashindwa kulea watoto wao Kwa ukaribu na kuwapa upendo ,familia inatawanyika ...Badae wanakuwa mnaanza kuwalaumu ....

Mfano ommy dimpoz Hana muda kabisa na baba yake na wala mim simlaumu kabisa Yule jamaa ,naamini hata mbinguni atafika ...wazazi wengi Ni wajinga Sana
 
Wakati unalelewa na bibi uliambiwa yapi kuhusu mama yako? Kama kuna uliyoambiwa kumhusu yakakufanya uwe hivyo naamini hayo ndio sababu ya hali uliyonayo sasa.

Je kama ni hivyo ulishawahi kuchunguza kujua uhalisia ni upi? Aisee mkuu mpende mama yako hata aweje, we mpende tu ndio mzazi wako.
 
nimejaribu Saana nimeshindwa
 
Back
Top Bottom