Nifanyeje ili nifanikiwe kama Bakhresa?

Android or ios

  • ANDROID

  • iOS

Results are only viewable after voting.
Tujifariji japo

STEP 01
Ukitaka kuwa kama Bakhresa kwanza jaribu kuwa kama Reg Mengi, ukitaka kuwa kama Reg Mengi amejielezea kwenye kitabu chake.

STEP 02
Ili kufikia Billion 600 ndani ya miaka 30 mbele kwasiku inabidi uingize around 70M-80M, ili uingize 80M kwasiku njia rahisi uwe na vyanzo vya pesa vinne (4) kila kimoja kikupe 20M kwasiku.

Kwabla kuwaza kuingiza 80M kwasiku umiza akiri utawezaje kutengeneza 20M kwasiku.

Ukishapata iyo Biashara na mchakato wake na ukatengeneza kweli 20M kwasiku Diversify ×4 upate 80M kwasiku.

Question
Biashara gani utapata 20M kwasiku ??
 
"Kama Hujakuta utajiri kwenye Familia yako, hakikisha Utajiri unauanzisha wewe". - unknown.

Fanya/anzisha kitu cha kipekee ambacho hakuna mtu ameshawahi kufanya kwenye Mazingira yako, utapata hela, na kama unataka hela nyingi zaid fanya ambacho wilaya yako hakuna mtu kafanya.

Na kama unataka hela zaid fanya ambacho Nchi yako hakuna mtu anafanya.

Na kama unataka uwe tajiri zaidi fanya ambacho Africa hakuna mtu amefanya.

Na uwe tajiri zaidi, basi fanya kitu ambacho Dunia hakuna mtu anafanya na watu wakipende/wakihitaji kama ni bidhaa au wahitaji kama ni Huduma.
 
Ukitaka kuwa millionea tatua matatizo ya watu elfu moja, ukitaka kuwa billionea kama bakhresa inabidi utatue matatizo ya watu million moja, ukitaka kuwa trilionea kama bill gate au mark zuckerberg tatua matatizo ya watu bilioni moja.

Hapa ndio Tofauti ilipo.

Kaa chini sumbua sugua kichwa.
Kama una uwezo mkubwa wa kifikiri na una weza kupata Rasiliamali kwa namna yoyote ile na pia ukaweza kumaster Mazingira yako, hakika utatoboa kwenye haya maisha.

Ila tukicopy na kupaste.
Au kutwa kuuza huduma/bidhaa za watu.
Tutaishia kupata hela ya mboga.

Mo Dewji na Bakhresa wana huduma na bidhaa wanatengeneza na kusambaza Africa Mashariki yote.

Na system imetengenezwa na inazid kukua.

Sasa sisi tujidai tunafungua Duka alaf Bidhaa tunanunua kwa hao Magwiji, alaf utajirike.

Hapana.
Tutapata hela kusukuma/ kurahisisha Maisha.

Ni mawazo yangu lakini.
 
Ukitaka kuwa millionea tatua matatizo ya watu elfu moja, ukitaka kuwa billionea kama bakhresa inabidi utatue matatizo ya watu million moja, ukitaka kuwa trilionea kama bill gate au mark zuckerberg tatua matatizo ya watu bilioni moja.

Hii ndo kanuni ya utajiri ...aanzie kutatua changamoto sehemu anayoishi!
 
Mh! Nilibahatika kukutana nae ila sikumuuliza hili swali, nilichomuuliza, hua anatumia kitu gani kutafuta wazo la biashara hadi akiianzisha inafanikiwa? Akasema wengi nnaokutana nao wanaomba pesa, nikamwambia ukinipa pesa ntaitumia itaisha, sitaki kurudi tena kukuomba pesa siku ingine.

Zaidi ya kuniuliza naitwa nani, nafanya nini na naishi wapi hatukuweza kufikia muafaka na boat ilikua imefika tukashuka.

Bahati mbaya boat ilikua ndio inakaribia kutia nanga akasema hata hiyo miradi na biashara anazifanya, haziendi ki ulaini kama tunavyoona huku nje, kuna zingine zinacjangamoto na huingia hasara inabidi warekebishe au kubadili mfumo.

Awazavyo mtu, ndivyo alivyo. Ukiendelea kuwa na mawazo ya kuwa tajiri ukachukua hatua stahiki, unaweza usiwe kama Bakhresa ila utakua na pesa.

Utajiri unaanzia kichwani kwenye fikra na mawazo yako.
 
Yawezekana sana, anza biashara ndogo ndogo, iwe inakuwa, ikifika level fulani, piga bonge la deal uongeze mtaji, liwe deal la maana na omba usikamatwe, kila la heri
 
Mkuu kuwa tajiri sio kitu rahisi kwenye uchumi tulisoma kuna njia kuu 3 za utajiri.
1.Ni kurithi-hii inachukua zaidi ya 90%
2.uvumbuzi kama akina bilget,jeff bezos
3.Ni bahati nasibu
Kwa hiyo mtaala wenu unafundisha kuwekeza katika kurithi na bahati nasibu kuliko hardwork,smartness,nidhamu ya pesa and the like?
 
"Kama Hujakuta utajiri kwenye Familia yako, hakikisha Utajiri unauanzisha wewe". - unknown.

Fanya/anzisha kitu cha kipekee ambacho hakuna mtu ameshawahi kufanya kwenye Mazingira yako, utapata hela, na kama unataka hela nyingi zaid fanya ambacho wilaya yako hakuna mtu kafanya.

Na kama unataka hela zaid fanya ambacho Nchi yako hakuna mtu anafanya.

Na kama unataka uwe tajiri zaidi fanya ambacho Africa hakuna mtu amefanya.

Na uwe tajiri zaidi, basi fanya kitu ambacho Dunia hakuna mtu anafanya na watu wakipende/wakihitaji kama ni bidhaa au wahitaji kama ni Huduma.
Bahati mbaya hakuna kitu ambacho hakijafanywa!!
 
Back
Top Bottom