Yohimbe bark
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 1,050
- 2,581
Habari wakuu, ni week sasa nipo chunya makongolosi kuchungulia fursa.
Kipindi natoka mbeya kuja huku nilipanda gari moja na mdada mmoja tulikaa seat za upande mmoja nikaanza kumdadisi anafanya shughuli gani huku Makongolosi akaniambia hua anaenda Soko la Mwanjelwa (anajumua) ndio lugha wanatumia akimaanisha anatafuta vipochi vya mitumba vya elfu 5&7 then analeta huku Makongolosi anauza kwa elfu 10 mpaka 15 kwa kuzungusha mtaani.
Nikamuomba aniongoze na mimi nifanye hiyo biashara nikiendelea kuzoea mazingira, dada wa watu hakua na shida akakubali so tukaweka appointment ya juzi tukutane town twende tukanunue mzigo.
Kweli siku ikawadia tukakutana nikanunua mzigo wa laki moja vipochi kama 16 hivi vya elfu 5 na elfu 7 na yeye akachukua mzigo wake safari ikaanza kwenda Makongolosi kuuza.
Aisee, tumefika kila mtu akabeba mzigo wake, tukaanza kukatiza mitaani huku namfata nyuma, mind you tulianza kuzunguka mida ya saa 7 mchana lakini mpaka saa moja usiku nilikua nimeuza vipochi viwili tuu tena kwa elfu 8000 each.
Yeye mwenyewe biashara haikua nzuri, dah nilikua nimechoka balaa yani kule kuna jua na vumbi balaa ikabidi tulale huku huku ili leo tukimbize tena, ila mpaka sasa bila bila mpaka nimechoka hapa nimekaa sehem nimepimzika nawaza tuu.
Wakuu naombeni ushauri nifanye biashara gani kwa huku ili nikuze mtaji? Lengo langu ni kufanya biashara Zambia huku nipo kukuza mtaji tuu hela iliyobaki ni 1M tuu balance.
Je, kwa mtaji huu naweza kununua dhahabu kidogo kidogo nikuze mtaji? Au nifanye nini ili mtaji ukue at least nipate profit ya 20k per day, najua biashara ni uvumilivu ila hii hapana nipo ready kufanya biashara nyingine ila hii imenishinda wakuu.
Kuna watu walinipa muongozo wa kufika huku Mungu awabariki sana na kuna wengine walinifata DM kupata abc za huku msihofu mje mjaribu na nyie penye watu hela ipo msiogope karibuni.
Mtanisamehe kwa kuandika bila kutumia paragraph coz am totally confused naombeni ushauri wakuu.