Nifanye nini ili kupunguza chuki yangu dhidi ya nyoka?

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
28,700
Reaction score
71,119
Wakuu habari,

Naomba Ushauri nifanye nini ili kupunguza chuki kubwa niliyonayo dhidi ya nyoka.

Sijawahi kuumwa na nyoka wala watu wa familia yangu hakuna aliyewahi kuumwa na nyoka lakini nina chuki kubwa sana dhidi ya nyoka.

Yaani nikimuona nyoka iwe shambani au nyumbani ni lazima nimuue, hata kama nipo njiani narudi kutoka shamba ikatokea nikamuona nyoka nitamtafuta mpaka nimuue.

Nikiwa naendesha gari ikitokea nyoka akakatisha barabara lazima nihakikishe namkanyaga.

Vitendo vyangu hivi vinanifanya nijihisi mimi ni mtu mkatili sana.

Karibuni kwa mjadala.
 
Kama hawaja kukosea kitu then unawafata unawaua your abnormal
 
Wakuu habari,

Naomba Ushauri nifanye nini ili kupunguza chuki kubwa niliyonayo dhidi ya nyoka.

Sijawahi kuumwa na nyoka wala watu wa familia yangu hakuna aliyewahi kuumwa na nyoka lakini nina chuki kubwa sana dhidi ya nyoka.

Yaani nikimuona nyoka iwe shambani au nyumbani ni lazima nimuue, hata kama nipo njiani narudi kutoka shamba ikatokea nikamuona nyoka nitamtafuta mpaka nimuue.

Nikiwa naendesha gari ikitokea nyoka akakatisha barabara lazima nihakikishe namkanyaga.

Vitendo vyangu hivi vinanifanya nijihisi mimi ni mtu mkatili sana.

Karibuni kwa mjadala.

Mimi tatizo langu ni lingine sina chuki na Nyoka bali namuogopa, hakuna kiumbe kinaniogopesha kama Nyoka, hata akiwa amekufa nikimuona mwili wote husisimka na kuishiwa nguvu, ni ajabu lkn nina woga wa Nyoka usio na mfano!
 
Dah kweli watu tunatofautiana,easter nilienda zoo nikapiga picha na nyoka kabisa kwa kuwashika ila chatu ndio niliogopa haha asije akanimeza bure
 
Nyoka nawapenda sana na siwezi kuwadhuru hata siku moja.
Shambani wapo wengi aina nyingi na nimepiga marufuku wauwawe kwani wananisaidia sana kula panya.
Wana kazi kubwa kwanini wauwawe?
Tena wafanyakazi wameisha wazoea na wakiwaona wanaondoka zao na kuwapa amani.
 
Mimi tatizo langu ni lingine sina chuki na Nyoka bali namuogopa, hakuna kiumbe kinaniogopesha kama Nyoka, hata akiwa amekufa nikimuona mwili wote husisimka na kuishiwa nguvu, ni ajabu lkn nina woga wa Nyoka usio na mfano!
Hahahahahaha nimecheka sana Hahahahahaha
 
Huyo ni adui yetu wa kudumu, shukuru kwa kumuwahi kabla hajakuwahi. Kaa mbali Na vichaka iko siku utapoteza pambano
 
Wengine nyoka tushalala nao,tushakoswakoswa sana tu
Nyie hamjagaaa Porini nn

Ova
 
Lazima kutakuwa na kitu hakiko sawa
Mimi marehemu bibi yangu alikuwa na hulka hiyo
Alishakuwa mtu mzima saana lakini kama atatokea nyoka yuko tayari kumfuata hata juu ya dari
 
Mimi sio tu kumuogopa, yaan ata clip zake huwa siangalii kwenye media yoyote
 
Lazima kutakuwa na kitu hakiko sawa
Mimi marehemu bibi yangu alikuwa na hulka hiyo
Alishakuwa mtu mzima saana lakini kama atatokea nyoka yuko tayari kumfuata hata juu ya dari
Huyo bibi yako ana tabia kama zetu sisi wanyamwezi wa Kaliua kule ulinduwanoni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom