Nifanyaje ili nisipende sana, naomba ushauri

Nifanyaje ili nisipende sana, naomba ushauri

Kafara
Huwa si panic ila inauma unapokuwa wewe tu ndio umkumbuke mwenzio hata siku 5 zaweza pita asishtuke. Mpaka nilishafikiria nitafute mchepuko ili nisimuwaze sana.
 
Last edited by a moderator:
Wewe kama umetendwa zaidi ya mara moja utakuwa haufai hata kidogo. Mimi huwa na stand single as a man, naakijilenga anadakwa na kuliwa
 
Msema yote,

Asante mpendwa wangu hatujaachana isipokuwa mimi ndio najiona kama nahangaika yeye walaa! Mimi ni mwajiriwa na nina kipato cha kawaida ila ndio kila kitu najihudumia mwenyewe yaani hata vizawadi vidogo hakuna sijui kuna watu wako hivyo.

JF nimekuwa nikisoma tu kwakweli inasaidia na wabarikiwe wote wanaotoa ushauri kwa moyo.
 
Last edited by a moderator:
ABUBAKAR SHEKAU
Pole kaka kwa uliyopitia, mimi huwa siachwi ila huwa nikiona visa vimezidi najiengua mwenyewe, kina wakati najiuliza au kupenda kwa dhati ni alinacha tu, maana mimi nikiwa na mtu ni huyo huyo tu labda nalo ni kosa.

Natamani niruke ruke lakini ndio siwezi
 
Last edited by a moderator:
Asante tatizo the right hajaandikwa usoni ntakaribisha wangapi ?

Akitokea utajua tu ni kama nyumba unajua tu hii nyumba itanifaa kuishi na zingine unazitazama unasema hapana
 
shosti mashemeji wanne na wote wanakuliza? Ngoja nikupe zoezi. Chukua karatasi 4, kila karatasi andika jina la shemeji mmoja, igawe katikati, upande mmoja andika mazuri yake, upande mwingine andika mapungufu yake hasa yale yanayokuumiza. Ukimaliza hiyo kazi chukua karatasi ya 5 chambua tabia zilizojirudia kwa wanaume wote hao (yaani zinazofanana).

Ukimaliza utagundua wewe ndo mwenye tatizo linalokufanya uvutiwe na wanaume wa aina hiyo. Kazi inabaki kwako kujua ni kwa nini unavutia watu wasiokupenda?

Bila shaka yoyote kuna watu waliokupenda na mpaka leo wanakupenda ila we unawaona hawana maana. Wewe na akili zako hizi ulizotumia kuandika hapa unajua kabisa unataka mapenzi lakini kuna akili nyingine ambayo inakudhibiti inakataa mapenzi. Wewe ndo unajua malezi na makuzi yako.

Uhuru wako utaupata siku ukibadilika wewe. Hao wakaka leo wakiulizwa waseme kitu kuhusu wewe watasema wewe ni king'ang'anizi, mara nyingi tu wameshajaribu kukuacha ila we unakomaa nao tu.

Nisamehe nimeusemea moyo ila tatizo lako si geni. Yaliyomo yamo.
 
Asante tatizo the right hajaandikwa usoni ntakaribisha wangapi ?

Endelea kukaribisha mwayego,utampata tu prince charming wako,au ndio umegive up unataka kuwa mtawa? 😆
 
Kupenda sana ndio kupi? Ukijitizama unaona wasiopenda sana wanafanya nini cha tofauti na wewe? Hujatueleza anayekutenda anakufanyia nini au wewe unamfanyia nini tofauti??

Kwa wanaume wanne kama ndio hao tu umekuwa nao kwa miaka yako 30, unastahili pongezi. Kuna quote moja naipenda sana inasema,"never get too attached to someone because you never know who they are talking to,missing,waiting on,wishing they was with,or fucking".

Usijitoe kwa mtu hadi ujione mhanga wa kupenda sana,nenda umbali huo wa kupenda sana kwa kupendwa/kuthaminiwa sana kwa kupewa heshima ya kuwa mchumba/ mke wa mtu..... Hawa wapita njia,ukiwapenda sana hivyo wanaona kuna wanakoweza pata zaidi yako.

Self Love is the best love! I leave you with this beautiful quote from With this Ring Movie, " realize that life is short and if you spend all your time waiting on a job or the One, that you waste a perfectly good chance to be happy.

I do. Then by the power vested in you, I make a new vow that single or married, working or not, that you will never wait for anything outside of yourself to change, before you choose to be happy. You may kiss the new you."
 
Nominomi Je, ulishafanya maombi/Duaa za dhati, ili huyo Mwenza aelekee? Jipange na uanze therapy za kiimani.....
utamtuliza sawiya !!
 
Last edited by a moderator:
Pole kaka kwa uliyopitia, mimi huwa siachwi ila huwa nikiona visa vimezidi najiengua mwenyewe, kina wakati najiuliza au kupenda kwa dhati ni alinacha tu, maana mimi nikiwa na mtu ni huyo huyo tu labda nalo ni kosa. Natamani niruke ruke lakini ndio siwezi

kakudanganya nani huwa huachwi? Hivyo visa mpaka mwenyewe unaona vimezidi ndo unaondoka ndo kuachwa kwenyewe. Akufukuzaye hakwambii toka. Sentesi yako ya mwisho inaonyesha we ni dada mzuri na unastahili mazuri.

Usikate tamaa. Tulia tu kwanza ushughulikie akili na nafsi yako. Siyo utulie eti kwa kujikip bize na mambo mengine. Siku hauko bize utarudi kule kule.
 
Njoo kwangu mm nae nimetendwa kwa kupenda...tunaweza kuwa na maumivu sawa...safari sawa na malengo sawa...karibu sana tupozane na kuanza safari mupyaaaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom