Pole sana, maumivu ya mapenzi ni hatari sana binafsi nimepitia kwani nilimpenda mtu (binti) mpaka nkimkosa nahis baridi, nilijitolea kwa kila kitu kwake lakini alivokuja kunitenda nilihisi kifo kitanichukua muda wowote,
Sifa na shukrani ziwaendee wana JF kwani nilileta shida yangu hiyo hapa walinishauri vema sana nkapata faraja japo mpaka leo nashindwa kusahau, japo hujatueleza ilikuwaje mpaka mkaachana,
Tafadhali kaa na jiweke bize na mambo yako pia usithubutu kuyatafuta mapenzi ndugu, mpenzi/ mchumba/ mume/ mke wa kweli huja mwenyewe hivo muombe Mungu sana akupitishe salama katika kipindi hiki kigumu, mwisho weka malengo yako na jitahidi kuyafata ili kufika malengo yako,
MWENYEZI MUNGU AWE NAWE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU MPENDWA