NIDA bado tatizo: Wafanyakazi wa NIDA wanachukulia watanzania hatuna akili

Wanajamii, nafikiri wafanyakazi wa NIDA wanachukulia watanzania hatuna akili. Binafsi nimejiandikisha tangu mwaka jana mwezi wa 3 lakini kila nikifuatilia kitambulisho naambiwa kwa sasa wanatoa namba tu vitambulisho wamesitisha. Kwa akili ya kawaida huu ni upumbavu uliokithiri kwa sababu;

1. Kutoa namba sidhani kama mtu ndo anapanga hizo namba, ni computer na hata wangetumia computer ya kwanza kuvumbuliwa bado wasingekuwa na spidi ndogo kiasi hiki.

2 Kuhakiki taarifa, mpaka mtu unapigwa picha fomu zako zinakuwa zimekidhi vigezo, kusema wanahakiki sina imani kama wanafuatilia mtu mmoja mmoja kulingana na taarifa alizojaza.

3. Nina imani mashine inayotoa namba ni tofauti na inayochapa vitambulisho sasa nashindwa kuelewa kwa nini utoaji namba uzuie uchapaji vitambulisho.

Mwisho kabisa kauli inayokera wanakuuliza kama umesajili laini ukisema ndiyo wanakuambia sasa we kitambulisho una haraka ya nini, yaani binafsi nimejionea kuna watu wasiofaa wamepewa mamlaka kuhudumia umma. Sasa hivi kuna baadhi ya taasisi wanataka waone ID ukisema una namba wanasema hawana access NIDA kuhakiki namba yako.
bro kuwa na maono kidogo! hao jamaa hawatokuja kamwe kutoa vitambulisho! walitaka tu kuingiza watu kwenye database
 
Wanajamii, nafikiri wafanyakazi wa NIDA wanachukulia watanzania hatuna akili. Binafsi nimejiandikisha tangu mwaka jana mwezi wa 3 lakini kila nikifuatilia kitambulisho naambiwa kwa sasa wanatoa namba tu vitambulisho wamesitisha. Kwa akili ya kawaida huu ni upumbavu uliokithiri kwa sababu;

1. Kutoa namba sidhani kama mtu ndo anapanga hizo namba, ni computer na hata wangetumia computer ya kwanza kuvumbuliwa bado wasingekuwa na spidi ndogo kiasi hiki.

2 Kuhakiki taarifa, mpaka mtu unapigwa picha fomu zako zinakuwa zimekidhi vigezo, kusema wanahakiki sina imani kama wanafuatilia mtu mmoja mmoja kulingana na taarifa alizojaza.

3. Nina imani mashine inayotoa namba ni tofauti na inayochapa vitambulisho sasa nashindwa kuelewa kwa nini utoaji namba uzuie uchapaji vitambulisho.

Mwisho kabisa kauli inayokera wanakuuliza kama umesajili laini ukisema ndiyo wanakuambia sasa we kitambulisho una haraka ya nini, yaani binafsi nimejionea kuna watu wasiofaa wamepewa mamlaka kuhudumia umma. Sasa hivi kuna baadhi ya taasisi wanataka waone ID ukisema una namba wanasema hawana access NIDA kuhakiki namba yako.
Kuna shida sana NIDA.
Ukienda kwenye ofisi zao kupata huduma unaonekana kama kinyago fulani.
Hivi wakubwa hawaoni tatizo kule NIDA?
 
Back
Top Bottom