Nibaki na mwanaume yupi kati ya hawa?

Nibaki na mwanaume yupi kati ya hawa?

Aisee,unapanganya panganya mpaka hueleweki,unagusa huku kabla hujamaliza unarukia kule!
 
Ni aibu pamoja na kuzalishwa na kuwa single mother bado hujui sifa za mwanaume mzuri kwa ndoa. Endelea tu kuwa peke yako mpaka utakapopata adabu.
 
Habari zenu wadau,

Mimi ni mgeni humu ndani nikaona siyo mbaya nika share nanyi ili nipate maoni yenu tofauti. Nina mpenzi ambaye kanitolea posa huyu mwanaume ananipenda sana tatizo ni dini yeye muislamu mimi mkristo.

Na kabla ya kuja home kutoa posa alishaulizwa kabisa kama utabadili dini kuwa mkristo utaruhusiwa kuleta hio barua akajibu yuko tayari kubadili na barua ikaletwa, mwisho wa siku mambo yakabadilika ndugu zake baadhi ya ndugu zake wamekubali kubadili dini baadhi wamekataa.

Sasa hivi karibuni kanipigia simu anadai anataka tukaishi wote. Binafsi siko tayari kwa sasa kuishi na mwanaume mpaka pale nitakapomaliza mipango yangu kuweka sawa, na ukizingatia kipato cha huyu mwanaume ni kidogo tofauti na mimi,kwa upande mwingine kabla ya huyu kaka kuna mwanaume mwingine ananipenda sana na mimi pia nampenda, tatizo ni mtu mwenye wivu siyo mchoyo ila malengo hana kabisa ya kuja kuishi na mimi na hata wazazi wangu kipindi cha nyuma tulivyotambulishana wakaniambia huyu atanipotezea muda.Niko njia panda niende wapi huyu ambaye atanipotezea muda au yule aliyenitolea posa? Na huyu aliyenitolea posa sina mapenzi nae kabisa.

Naombeni mnishauri jamani huyu aliyenitolea posa kabila lake makonde na huyu hana malengo na mimi kabila lake muhaya na mkumbuke kuwa kwa sasa sina mpango wa kuishi na mwanaume naona nikibaki kivyangu ndo nakuwa na furaha zaidi kuliko kuwa na mwanaume, bila kusahau nina mtoto ambaye nampenda sana ndo furaha yangu ya kwanza iliyobakia, ikumbukwe kuwa hawa wanaume hakuna hata niliyezaa nae mtoto au watoto.
Soma paragraph yako ya mwisho utakuta jibu la swali lako hapo
 
Hapo nimeelewa ikumbukwe zako tu. Eniwei, naona mwenyewe hujui unachokitaka lakini ikumbukwe wewe ni single mother.
 
Huwezi kuchanganya mafuta na maji kamwe..nilichokiona ni dini tofauti

Kuna watu hawataoa/kuolewa kwasababu wamezaliwa hivyo,kuna watu wamewafanya hivyo au wameamua kumtumikia mungu -Jesus

Kuzaa sio sababu
 
1466359972665.jpg
 
Ningekuwa mimi ningebaki tu na uyo muhaya maana malengo yetu yako sawa
 
Back
Top Bottom