Nibaki na mwanaume yupi kati ya hawa?

estlyjonathan

Member
May 26, 2016
84
122
Habari zenu wadau,

Mimi ni mgeni humu ndani nikaona siyo mbaya nika share nanyi ili nipate maoni yenu tofauti. Nina mpenzi ambaye kanitolea posa huyu mwanaume ananipenda sana tatizo ni dini yeye muislamu mimi mkristo.

Na kabla ya kuja home kutoa posa alishaulizwa kabisa kama utabadili dini kuwa mkristo utaruhusiwa kuleta hio barua akajibu yuko tayari kubadili na barua ikaletwa, mwisho wa siku mambo yakabadilika ndugu zake baadhi ya ndugu zake wamekubali kubadili dini baadhi wamekataa.

Sasa hivi karibuni kanipigia simu anadai anataka tukaishi wote. Binafsi siko tayari kwa sasa kuishi na mwanaume mpaka pale nitakapomaliza mipango yangu kuweka sawa, na ukizingatia kipato cha huyu mwanaume ni kidogo tofauti na mimi,kwa upande mwingine kabla ya huyu kaka kuna mwanaume mwingine ananipenda sana na mimi pia nampenda, tatizo ni mtu mwenye wivu siyo mchoyo ila malengo hana kabisa ya kuja kuishi na mimi na hata wazazi wangu kipindi cha nyuma tulivyotambulishana wakaniambia huyu atanipotezea muda.Niko njia panda niende wapi huyu ambaye atanipotezea muda au yule aliyenitolea posa? Na huyu aliyenitolea posa sina mapenzi nae kabisa.

Naombeni mnishauri jamani huyu aliyenitolea posa kabila lake makonde na huyu hana malengo na mimi kabila lake muhaya na mkumbuke kuwa kwa sasa sina mpango wa kuishi na mwanaume naona nikibaki kivyangu ndo nakuwa na furaha zaidi kuliko kuwa na mwanaume, bila kusahau nina mtoto ambaye nampenda sana ndo furaha yangu ya kwanza iliyobakia, ikumbukwe kuwa hawa wanaume hakuna hata niliyezaa nae mtoto au watoto.
 
Mkuu alieenda /bobea madrasa na katEkesi hawa hawalandan hata kidogo mwanzo mtakuwa watamu kwel ngoja akupe mimba mtalea mtot afke stage ya mafunzo ya dini hapo utalia nakuona dunia mbaya lazm we utatak aende kwenye katekes halikadhalika na mwenzio atataka mwanae aende madrasa,,,,, KINGINE ebu wapasulie ukweli hao wanaume na sio kutupa yaliyo moyon mwako sis ambao hata hatukujui sura,,,,, kwann unawapotezea mda???? wakati we mwenyew mzaz tayar huku wenzio bado.
 
wala siwapotezei muda ni kutojitambua tu
 
Rudisha posa ya watu. Chagua mmoja kati ya hao awe mpenzi wako. Tenganisha mapenzi na mambo yako yote ya maisha. Tengeneza maisha yako peke yako, bila kumshirikisha mpenzi wako. Yeye aishi kwake na wewe uishi kwako, muwe mnatembeleana tu. Hapo maisha yatakuwa matamu sana, kwako na kwa mtoto wako.
 
Habari zenu wadau,

Mimi ni mgeni humu ndani nikaona siyo mbaya nika share nanyi ili nipate maoni yenu tofauti. Nina mpenzi ambaye kanitolea posa huyu mwanaume ananipenda sana tatizo ni dini yeye muislamu mimi mkristo.

Na kabla ya kuja home kutoa posa alishaulizwa kabisa kama utabadili dini kuwa mkristo utaruhusiwa kuleta hio barua akajibu yuko tayari kubadili na barua ikaletwa, mwisho wa siku mambo yakabadilika ndugu zake baadhi ya ndugu zake wamekubali kubadili dini baadhi wamekataa.

Sasa hivi karibuni kanipigia simu anadai anataka tukaishi wote. Binafsi siko tayari kwa sasa kuishi na mwanaume mpaka pale nitakapomaliza mipango yangu kuweka sawa, na ukizingatia kipato cha huyu mwanaume ni kidogo tofauti na mimi,kwa upande mwingine kabla ya huyu kaka kuna mwanaume mwingine ananipenda sana na mimi pia nampenda, tatizo ni mtu mwenye wivu siyo mchoyo ila malengo hana kabisa ya kuja kuishi na mimi na hata wazazi wangu kipindi cha nyuma tulivyotambulishana wakaniambia huyu atanipotezea muda.Niko njia panda niende wapi huyu ambaye atanipotezea muda au yule aliyenitolea posa? Na huyu aliyenitolea posa sina mapenzi nae kabisa.

Naombeni mnishauri jamani huyu aliyenitolea posa kabila lake makonde na huyu hana malengo na mimi kabila lake muhaya na mkumbuke kuwa kwa sasa sina mpango wa kuishi na mwanaume naona nikibaki kivyangu ndo nakuwa na furaha zaidi kuliko kuwa na mwanaume, bila kusahau nina mtoto ambaye nampenda sana ndo furaha yangu ya kwanza iliyobakia, ikumbukwe kuwa hawa wanaume hakuna hata niliyezaa nae mtoto au watoto.
Shulen haukufundishwa namna ya kupangilia mtiririko wa mawazo???
 
Back
Top Bottom