Ni zipi mbinu za kudhibiti wizi kwenye duka la jumla?

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,421
Hello JF,

Moja kwa moja kwenye bandiko

Mimi ni mmoja wa wamiliki wa Duka la Jumla kiukweli hi biashara inalipa sana hasa inalipa faida ya milion 1.5 kwa mwezi kabla ya kutoa malipo ya wafanyakazi na Kodi ya pango nabaki na 600k au 700k Kama faida, kwa Duka moja.

Hivyo kutokana na biashara kukua nimefungua zaidi ya maduka 4 ya jumla katika mikoa ya Tanga Arusha Mwanza

Dar ndio mean Office ilipo

Biashara ambazo nazi-manege

Tomato, pemepers biscuits, kalamu, Super Grue, madaftari, pipi Big G, nk.

Changamoto ipo kwenye kulinda wafanyakazi wasiibie sana hadi kupelekea biashara kufa

Je, ni mifumo gani ya ulinzi niiweke ili kulinda Mahesabu pamoja na store?

1618206107437.png
 
Unahitaji CCTV kwa ajili ya kufuatilia yanayoendelea katika maduka yako. Unahitaji well thought interconnection ya hizo CCTV na internet ili uwe na access popote.

Pili unahitaji accounting software ambayo inaweza kufanya inventory management ili kufanya tracking ya purchase, sales, profit and loss na kujua financial position yako.

Kwa upande wa Software kama unataka serious consultant unaweza kunicheck inbox. Ni kama tu uko serious. Yale mambo ya kupotezeana muda huwa sina muda nayo.
 
Sijaona aliyeshauri bado kuhusu kutafuta watu ambao ni waaminifu na uaminifu wao utakuja pale umewalipa vizuri,unaweza ukafunga CCTV camera even ukakaa na kijana dukani still ukapigwa.

Nina experience na haya mambo,vijana huwa wanachonga deal na wateja wazoefu wa duka lako au wajanja wajanja walio nje mfano hapo umesema unauza biscuits, siujui bado utofauti wa bei kati ya carton ya biskut na tomato ipi kubwa ila wanachofanya huchana boksi la tomato na kuzitoa na kulijaza biscuits (ni mf kama kimoja wapo kitakuwa na bei kubwa zaidi) na kulifunga vizuri kisha anampanga mtu “bwana njoo dukani toa order ya tomato” mimi mteja nikija nakulipa wewe boss pesa ya thamani ya tomato let's say 30,000/= wewe utaagiza kamtolee tomato akiingia store anatoa lile box alilojaza biskut zenye thamani mf 70,000/= na box inapita mbele yako ukijua ni tomato kumbe sivyo.

Ni changamoto sana,may be kama alivyoshauri mdau hapo juu uwe na software utakayotumia kulinda mali zako nayo pia ni gharama nahisi but bora kuwa nayo.
 
Sijaona aliyeshauri bado kuhusu kutafuta watu ambao ni waaminifu na uaminifu wao utakuja pale umewalipa vizuri,unaweza ukafunga CCTV camera even ukakaa na kijana dukani still ukapigwa.

Nina experience na haya mambo,vijana huwa wanachonga deal na wateja wazoefu wa duka lako au wajanja wajanja walio nje mfano hapo umesema unauza biscuits, siujui bado utofauti wa bei kati ya carton ya biskut na tomato ipi kubwa ila wanachofanya huchana boksi la tomato na kuzitoa na kulijaza biscuits (ni mf kama kimoja wapo kitakuwa na bei kubwa zaidi) na kulifunga vizuri kisha anampanga mtu “bwana njoo dukani toa order ya tomato” mimi mteja nikija nakulipa wewe boss pesa ya thamani ya tomato let's say 30,000/= wewe utasema kamtolee tomato akiingia store anatoa lile box alilojaza biskut zenye thamani mf 70,000/= na box inapita mbele yako ukijua ni tomato kumbe sivyo.

Ni changamoto sana,may be kama alivyoshauri mdau hapo juu uwe na software utakayotumia kulinda mali zako nayo pia ni gharama nahisi but bora kuwa nayo.
ahsante mkuu kwa mchango wako izo software zinafanyaje kazi
 
Hahaha kumbe ndivyo ilivyo
 
Hakuna haja ya camera, ujiwa na software ya inventory management, camera ni kujiongezea gharama. Maana hata ikiondoka carton moja ya item moja hesabu zinagoma . Cha kufanya kila item moja iwe displayed kwenye ngazi halaf zingine zote zinabakia store. Kwa hiyo mteja akija ataangalia sample kwenye item ambayo ipo kwenye ngszi then muuzaji ataangalia hiyo item kama ipo kwa kiasi gani kwenye system na kujulisha mteja kama ipo ama imeisha sasa kule store kutakuwa na store keeper naye ana comouter ilounganishwa kwenye system yeye kazi yake nikuregister vitu vinavyotoka na kuingia na bei za kununulia na kuuzia, na kutakuwa na watu wanaobeba vitu kutoa store kuleta kwa mteja, sasa ikipotea hata item moja wale wabebaji na mtu wa store kata kwenye mishahara yao. Wewe utabaki sehem tu kuangalia report tu . Na kwa vile una maduka mengi system inakuwa vizuri ikiwa online.
 
Back
Top Bottom