Niliajiriwa 2014 kwenye sector ya elimu (mwalimu), nimepambana na maisha ya utafutaji Si haba Mungu kanisaidia nimefanikiwa kupata mtaji kiasi,nimefungua maduka mawili, duka la mahitaji ya nyumbani jumla na rejereja na la pili ni duka la simu,vifaa vya umeme na huduma za fedha mtandaoni (Mpesa, Tigo Pesa n.k)
Duka Moja anasimamia make wangu na la pili nimeajiri vijana watatu,NAMI nikitoka kazini huwa naingia kazini kusaidia duka mojawapo,katika kufanya kazi huko nakumbana na changamoto nyingi.
Kukosa uaminifu kwa vijana, usimamizi hafifu wa kazi,kupitia changamoto hizi naona ukuaji wa biashara ya si kama vile ninavyotegemea na hili naliona hasa kipindi Cha likizo nikiwepo mwenyewe biashara yangu huwa inaimarika sana.
KWENU WAUNGWANA: Kuna muda nawaza kusitisha ajira yangu nijikite katika biashara kwani kupitia huko ntajikwamua kiuchumi zaidi. Si Kwa kudharau ualimu la hasha kwani kupitia ualimu ndo nimepata mtaji Bali ualimu huu naona hautanisaidia kufanikiwa zaidi,huwezi kuajiri mtu akutafutie million 100 ww ukabaki unatafuta laki 6 ya ualimu.
Kila ninapofikiria kuacha kazi napata mkwamo mkubwa wa mawazo, lkn pia napata msongo mkubwa wa mawazo Kwa kutotimiza majukumu yangu ya ualimu vizuri, mara nyingi natoroka kazini kwa kifupi sitekelezi majukumu yangu ipasavyo na ni dhambi kubwa naifanya, kwa wanaoujua ualimu vizuri Ili utekeleze majukumu Yako yote hautaweza kujihusisha na shughuli zingine.
Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani,msaada tafadhari Ili nijikwamue kutoka katika hili.