Ni zipi hasa sifa za kuwa Kiongozi ndani ya UVCCM?

Ni zipi hasa sifa za kuwa Kiongozi ndani ya UVCCM?

Halaiser

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
4,739
Reaction score
7,671
Kumekuwepo na maneno ya sintofahamu toka kwa Viongozi wa UVCCM kwa nyakati tofauti. Hawaangalii umri wala nafasi ya mtu kwenye Jamii.
 
Kumekuwepo na maneno ya sintofahamu toka kwa Viongozi wa UVCCM kwa nyakati tofauti. Hawaangalii umri wala nafasi ya mtu kwenye Jamii.View attachment 3539643
downloadfile.jpg
downloadfile.jpg
downloadfile.jpg
 
Nchi hii ni wazi inahitaji ukombozi wa kweli. Bila kuwa na mapinduzi ya fikra hatutatoka hapa tulipo.

Kijana mdogo aliyezaliwa baada ya CCM kuanzishwa eti anasimama kuwazodoa Waanzishi wa CCM yenyewe?

Tunakwenda kufanya nn kwenye Nyumba za Ibada kama hatuwezi kuwaheshimu wala kuwapenda Viongozi wetu wa Kiroho?

Anasema tusichanganye Dini na siasa. Kwanini kabla hatujaanza shughuli za kisiasa huwa tunawaomba Viongozi wale watufungulie kwa Dua?? Mnawaalika kwenye shughuli za kisiasa wa kazi gani?

Kazi ya Viongozi wa Dini siyo kuwabembeleza waovu eti waache dhambi. Bali kuwakemea waache uovu wao.

Haiwezekani watu wanatekwa wanapotezwa halafu wakae kimya. Haiwezekani Mchunga Kondoo amuone mbwa mwitu akimshamulia Kondoo wake eti akae kimya. Mambo ya ajabu tena ya kusikitisha sana.
 
Back
Top Bottom