wanaitaka iwe kama nchi huru isiwe na mchanganyiko na wabara na hata serikali yao wanataka ijitegemee labda hapa mie niongezee kisub question hivi mfano muungano ukavunjika na zanzibar ikawa taifa linalojitegemea wanaweza kua na maendeleo kuipita bara?
inatisha,inaonyesha kuwa una hasira sana
yaa...bora waone hasira katika hiyo avatar , tumechoshwa na siasa hizi za kuburuzana... OUR TIME HAS COME...
mbona watu wamehudhuria sherehe za muungano ati? tela kule kule zanzibari, kulikuwa na kundi lililoandamana kupinga hizi sherehe kufanyika humo kisiwani?
mbona watu wamehudhuria sherehe za muungano ati? tela kule kule zanzibari, kulikuwa na kundi lililoandamana kupinga hizi sherehe kufanyika humo kisiwani?
Kaitka uwanja wa Amani Stadium katika sherehe za muungano walihuzuria uwanja huo,asilimia 95 ni watanganyika 5 ni wazanzbari wasaliti tena wale wafanya kazi wa serikali ya zanzbar kwa kulazimishwa kuenda sherehe hizo.mbona watu wamehudhuria sherehe za muungano ati? tela kule kule zanzibari, kulikuwa na kundi lililoandamana kupinga hizi sherehe kufanyika humo kisiwani?
Vongozi mara nyingi wanaghiribu watu kwa kutumia matatizo hewa kuonekana kuwa halisi. Katika hstoria wanasiasa wenye 'charisma' ya kusema wamepeleka nchi zao kwenye matatizo makubwa kuliko mwanzo. Km. Hitler na wayahudikuwa matajiri kuliko wajerumani asilia, Habyarimana na interahamwe yake kuhusu watutsi. Sasa huko kuona majengo yanajengwa Dar, masikini na si Tanganyika yote, ndio mtizamo wa uchochezi.
Zanzibar kama wanataka kuwa soverign state kama Monaco na Luxembourg si waseme tu. Tanagnyika itahandle, kwa makubaliano, kwa niaba yao yale wtakayoona hawawezi. Hivyo hatuna sababu ya kuwa na Tanzania tenge. Kama noma naiwe noma ndivyo waimbaji wa taaabu watuambiavyo. Hali ya hewa imeshachafuka.
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
- Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
- Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
- Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
- Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
- Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
- Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?

Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
- Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
- Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
- Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
- Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
- Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
- Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?
Sio muhimu kuwa na maendeleo kuipita bara....Muhimu kuwa huru. By the way, Zanzibar ilishawahi kuwa ya 3 katika Afrika kuwa na GDP kubwa...enzi hizo.
mzee mwanakiji huwa naheshimu sana michango yako.
lkn bado huwa najiuliza nini hasa msimamo wako kuhusu zenj.
nakumbuka zenj ilipoambiwa sio nchi uliandika makala nyingi tu za kutofurahishwa na neno lile na ulifika na kutaka wazenj wajikomboe.
wanapotaka kujikomboa umegeuka na unahoji upande wa pili
Hapa watu wanadanganyana tu; Zanzibar inaweza kuwa nchi huru kabisa nje ya Muungano na ikawa na mambo yake yote. Hilo wala si tatizo. Wanaofikiria kuwa kwa kufanya hivyo Zanzibar itageuka Pepo kwa kweli wanajipa matumaini ya uongo tu yenye ghilba ndani yake. Zanzibar itakapogeuka pepo itageuka pepo kwa wale waliokuwa na pepo hiyo kabla ya 1964. Na watakapoanza kujijengea pepo yao tena matatizo yale yale yatatokea tena na mapinduzi mengine yatafanyika na wakati huo yatakapotokea Tanzania (itakuwepo bila ya shaka) itabidi waingilie kati na safari hiyo kuiannex kabisa Zanzibar! - nawaza tu.
Mkuu.Hapa watu wanadanganyana tu; Zanzibar inaweza kuwa nchi huru kabisa nje ya Muungano na ikawa na mambo yake yote. Hilo wala si tatizo. Na watakapoanza kujijengea pepo yao tena matatizo yale yale yatatokea tena na mapinduzi mengine yatafanyika na wakati huo yatakapotokea Tanzania (itakuwepo bila ya shaka) itabidi waingilie kati na safari hiyo kuiannex kabisa Zanzibar! - nawaza tu.
Mkuu Mkandara, Maalim sasa hutamsikia maana keshagawiwa keki, huyu bw hata siku moja hutamsikia hadharani akipinga muungano, ila kwenye vijimikutano vya barazani ndiko mahali pake. Hana ubavu wa kuzunguzia muungano hadharani kwasbabu atasema nini na ni yeye alimtonya mwalimu?
Wazanzibarikujitenga hewala.Hewala kwasababu kero na manung'uniko yasio na sababu za msingi yanachosha. Wale wa kawaida kama ilivyo watanzania wengine wangependa kurekebisha kasoro na kuweka mfumo unaokidhi haja ya sasa,kuna kikundi kinachosema neema ipo njiani, sijui kama neema hiyo ni kwa wote au wateule.
kinachonikera ni kulalamika bila hoja za mashiko.Muungano eti haujawatendea hata jema moja,ni maovu tu. Huu unafiki ndiyo unaudhi, kweli Muungano una matatizo lakini sitaacha kusema unafaida.
Baadhi ya kero na hoja wasizozijibu:
Mapinduzi yameletwa na Nyerere (Ghaisany na mzalendo.net), sasa wanasherehekea nini Jan 12 kama ni uvamizi.
Sijui kama wanajua nini mapinduzi kwasababu wenye nywele za kimanga wanasema a a ! kipilipili wanasema mapinduzi daima,wanaposhindwa kufikia muafaka wanashambulia Tanzania na Nyerere na kusingizia muungano.
Wanasema mambo ya muungano ni 11, sawa! ajabu hilo la mafuta sijui lilitabiriwa vipi mwaka 1964. Hatumii neno nishati kwasababu lina maana zaidi ya wanayoipenda. Katika hayo 11 mengi ni yale yanayowanufaisha wao. Hawaongelei ardhi n.k. Kila kinachowagusa wao ni cha muungano vinginevyo ni chao.
Mengine ni ya ajabu, eti kwanini mkuu wa majeshi au IGP hajawahi kutoka znz, utadhani wakuu hao wanapigiwa kura. Jamani!!! Mbona hatujawahi kuwa na CDF au IGP Mmakonde au Muha!! Ni taratibu gani zinatumika kuwapata watu hawa!!
Wanasema Luxenbourg ina watu 500,000 lakini inapewa uongozi EU, sijui wanajua kuwa ile ni european union kama E.A.C ambayo uongozi unazunguka na sasa tuna katibu mkuu kutoka Rwanda n.k. Utafananishaje na muungano wa nchi. Je tuchague watu tu kwa jiografia au uwezo. Tanzania bara walimtaka Salim bila kujali anatoka wapi, 2/3 ya Halmashauri kuu ilikubali, 2/3 kutoka znz wakaleta fitna huyo ni hizbu n.k sasa wanalalamika wanaonewa!
Wanasema wakijitenga watafutiwa visa za Oman, ah ! hili sina comment maana sijui nianzie wapi.
Wanasema Bara wanawatoza kodi ndio maana biashara inakufa, ha! walitaka vitu viingie znz halafu watumie mgongo wa muungano kuviingiza bara bure, changu ni chako, chako ni chetu!
Wanasema watapata misaada kutoka uarabuni, hata hili sina comment ! na watajiunga na OIC kana kwamba OIC ndio dawa ya matatizo hili nawatakia kheri.
Sasa hivi wanataka Tanganyika irudi, ah! hawahitaji Tanganyika wao kama wameweza kubadili katiba yao bila kuwiana na ya muungano wanashindwa nini kupeleka muswada kwa njia za sheria, wakapiga kura ya maoni wakajitenga.
Hoja ya kutaka Tanganyika ni kutaka kusema sasa tuwe na serikali ya shirikisho ili yale yanayowagusa yawe ya shirikisho, hili sikubaliani nalo maana ni kubebeshana mizigo tu, wao wavunje muungano kila mtu aishi kwa amani.
Wanasema turejee mambo 11, hata hili halina maana, maana hayo 11 mengi yanawagusa, wakati huo huo wanasema mafuta a a! hawasemi nishati. Wapi imesemwa urais ni kupokezana katika hayo 11, wapi imeandikwa mawaziri ni 1/2 kwa 1/2, wapi imesemwa mkuu wa majeshi au IGP ni kupokezana. Nina maana hata hayo 11 sijui kama wanayaelewa ni yapi.
Ukweli mambo ni mengi sana kuorodhesha, lakini la muhimu ni wao wasimame kidete kuirejesha nchi yao kati ya zile nyingi MMKJ alizoorodhesha. Mimi nawaunga mkono katika jitihada za kuirudisha znz ya kale iliyosheheni miti ya mizambarau, hewa ya jasmini, mito na asali, ile ya Sultan! lakini siungi mkono unafiki wa kuushtumu muungano bila kutaja hata kizuri kimoja. Muungano una matatIzo na hata Tanzania bara wanalamika lakini haiondo zuri moja litokanalo.
Leo wanalalamika muungano mbaya lakini mashaalah wapo Kigamboni, Msasani , Ilala n.k kama raia mwingine wa Tanzania.
Muungano ungekuwa mbaya kama wanavyoandika nusu wasingeishi huku.
Ukweli ni thawabu si dhambi lakini unafiki una aya yake, muogopeni mwenyezi mungu kwa kauli zenu.