Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,093
- 43,276
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
- Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
- Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
- Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
- Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
- Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
- Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?