Ni watatu tu wanaofaa urais 2015

Ni watatu tu wanaofaa urais 2015

Lowasa kwanza atuambie vizuri kuhusu Richmond, bado hajanasuka.

Magufuli atuambie kwanza uuzaji wa nyumba za serikali, na ile ya kwake aliyoinunua pale Ali Hassan Road, na amemuuzia nani ama ni yeye anayefanya uwekezaji pale.

Dr Slaa peke yake ndiye anayesimama bila lawama.

Itabidi na sisi tufanye kama Kenya, wagombea urais ni lazima wapite Integrity Test.

na huyu dr slaa mbona anakibana sana chama kimlipe pesa nyingi? Halafu anaiba wake za watu?. Huyu nae hafai ataleta uzinzi ikulu.
 
1. Wote hawa ni wachapa kazi
2. Wote hawa wanamsimamo.
3. Wote hawa wana vision na nchi
4. Wote hawa wanamaamuzi magumu kwa maendeleo ya nchi.
5. Wote hawa wakotayari kusimamia sheria kwa watendaji
na vigezo vingine vingi tu.
4.mwigulu nchemba
5.wassira steven
6.maji marefu.
7.michae kamuhanda
8.kingunge ngombale mwiru.
 
Huwa namwona Magufuli anaweza nyoosha nchi, kama Kagame alivyoweza ibadilisha Rwanda. Huyu anathubutu na yupo Kwa ajili ya watu Si mbinafsi!
 
Katika viongozi waliopo sasa hapa nchini kwetu haijalishi ametokea chama gani, wafuatao ndio wanaofaa kuwa rais mwaka 2015:

1. Edward Lowassa
2. John Magufuli
3. Dr. Slaa.

Wengine ni porojo tu.

we ni umbwa¬ mwizi huyo namba moja wa nini?umetumwa!hivi kwanini hatujifunzi pamoja na kuwa mjini ambapo info zipo za kutosha>?hivi hii nchi ilipofika tuna sababu ya kuwaa kumpa nchi mwizi??anayetaka urais kwa gharama yoyote ile? ma-chiziiiiiiiiiiiiiiiii wakubwa nyie!
 
Katika viongozi waliopo sasa hapa nchini kwetu haijalishi ametokea chama gani, wafuatao ndio wanaofaa kuwa rais mwaka 2015:

1. Edward Lowassa
2. John Magufuli
3. Dr. Slaa.

Wengine ni porojo tu.

Huyo mzee ameshakataliwa 2010 mkilazimisha tutamkataa tena sasa ni zamu ya Zitto .

Wengine udini tu!

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Last edited by a moderator:
Lowasa hafai ila sijui vigezo ulivyotumia
ukisoma hotuba za Nyerere jamaa huyu hafai kabisaaa
kwasababu sijasikia akiongea juu ya rushwa za kimtandao
ndani ya CCM, na yeye zote zinahusishwa na yeye.
Kha! Hutuba za nyerere za nini tena? Tutumie akili zetu.



Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Ndio uhuru wa kuabudu endelea kuwa muumini wa mtume Nyerere,ni wendawazimu kuamini kila alilosema Nyerere lilikuwa sahihi au leo taifa la Tanzania haliwezi kwenda bila yeye.
Mkuu naona hujanielewa vizuri....ni kama vile umejawa na jazba....sijasema kwamba kila alichokisema kilikuwa sahihi...yeye ni mwanadamu..kama mimi na wewe. Lakini lazima tukubali alikuwa na upeo mkubwa sana..na haya utaona kama ukiwa unaweza kufikiria ukiwa huru. Kwa kifupi haya tunayoyaona leo ni yeye Mtume Nyerere ndiyo aliyachelewesha.....aliyaona....aliingilia kati akayapoteza.....yalikuwa yaonekane mara baada ya utawala wa Mwinyi..Tumshukuru angalau tuliishi kwa miaka 10 ya raha na nidhamu....kama hulioni hili basi ujue una jambo linaziba nuru ya macho yako.....
 
we ni umbwa¬ mwizi huyo namba moja wa nini?umetumwa!hivi kwanini hatujifunzi pamoja na kuwa mjini ambapo info zipo za kutosha>?hivi hii nchi ilipofika tuna sababu ya kuwaa kumpa nchi mwizi??anayetaka urais kwa gharama yoyote ile? ma-chiziiiiiiiiiiiiiiiii wakubwa nyie!
Punguza jazba mkuu....utapandwa na presha....wezi wote wako magerezani....:sleepy:
 
Mwanzilishi wa uzi huu alikosea kupanga accordingly ni hivi inatakiwa

1. Dr. Slaa.
2. Edward Lowassa
3. John Magufuli
 
Nimefuatilia comment zote kwa karibu sana inaonesha watu wanamkubali sana EL. Kwa mujibu wa hapa JF EL anaweza akaongoza nchi.
 
Nimefuatilia comment zote kwa karibu sana inaonesha watu wanamkubali sana EL. Kwa mujibu wa hapa JF EL anaweza akaongoza nchi.
Haijalishi kama unakubaliwa au haukubaliwi...."Kushinda uchaguzi ni mbinu tu" - JMK
 
pamoja na kumlaumu lowasa sana nani anaweza kutaja amekamatwa wapi na kosa na hajapelewkwa kustakiwa na je kwa nn tunamshupalia mtu fisadi na yet anataka uraisi??

Unawezaje kugombea uraisi wakati wewe ni fisadi haiingii akilini kwamba mtu anataka kwa nguvu kugombea urais wakati yeye ni fisadi na kingine kwa nn hao waliomtuhumu wasimpeleke mahakamani wanamwogopa nn mie ushauri wangu agombee tu kama watu watampenda watamchangua.Tuache maneno ya mtaani jamani.

Naongea hivi ni upeo wangu sio kama hata kinifa atakuja kny msiba.
 
Mkuu mimi siwezi kuvisemea vyama vya upinzani, hisipokuwa nafikili kwa Chama tawala wawe makini, wasipendekeze Wanachama ambao wanaonekana wakipewa/teuliwa kwenye ngazi ya U-RAISI watapenda sana kulipiza visasi, tukifanya kosa hilo TAIFA letu litayumba sana.

Ukiwasikiliza kwenye media wanaonekana wako radhi kuwapa cha mtema kuni mahasimu wao pindi waki ingia IKULU - one could read between the line, wako determined kabisa ingawa hawasemi openly (AKATULE), hii si dalili nzuri kusema kweli.

Mbona watu hawampendekezi Mh. PINDA waziri mkuu, jamaa katulia sana huyu, hana makundi na anajuwa mambo mengi kuhusu TAIFA letu, kakaa IKULU karibu maisha yake yote - katika kuleta harmony ndani ya Taifa letu Mh.Pinda anatufaa SANA, msikilizeni vizuri anapojibu maswali au anapo-deal na very controversial issues (vilivyo kaa ndio sivyo) haogopi mtu au kusema ukweli bila kujali lawama - Yuko level headed KWELI KWELI.

Hiyo ikishindikana basi apewe Mh.Membe, kwa sababu zile zile nilisopendekeza hapo juu i.e HARMONY, waziri mkuu atokane na hawa wafuatao: Mh. Magufuli , Mh.Prof. Tiba, Mh. Mwakyembe.
 
Sasa naomba tutafakari hii thread tena niliitoa 2012.
 
Back
Top Bottom