Sidhani kama anaogopwa, lakini ninadhani kwamba hana simile. Anapaswa kuwa mtendaji, kwa maana ya kwamba akitoa kauli kwa kukurupuka, basi Rais awepo kwa ajili ya kuirekebisha. Ni mfuatiliaji sana na anataka mabadiliko ya haraka kwa kila jambo. Hana simile, sasa mambo mengine hayawezekani kwenda hivyo.
Ni dhahiri Magufuli angekuwa Rais angeshaagiza jengo la TANESCO livunjwe, sasa maamuzi ya level ya urais hayawezi kuwa yanafanywa kirahisi namna hiyo. Anatakiwa tu awe ni mtendaji, tukimpa kazi ya kufuatilia utekelezaji wa ilani, hatapindisha. Na ikitokea akapindisha, Rais atarekebisha. Sasa niambie yeye ndo Rais halafu amewaambia watu wapige mbizi kama hawawezi kulipa nauli. Tell me wananchi wamemjia juu what will happen?
Labda mtu ambaye ningesema ana staha nzuri na umakini mkubwa naweza kusema Mwakyembe. Lakini Magufuli, hapana. Yeye afanye kazi katika level ya mtendaji mkuu (PM).