Ni wapi nianzie? Naombeni mawazo yenu MMU

Ni wapi nianzie? Naombeni mawazo yenu MMU

34 bado kijana mdogo sana huna hata haja ya kua naa haraka wewe bado mdogo mno ila sababu ya kujifananisha na wengine ndio unajiona umechelewa hujachelewa popote, mfano ukiwa na mtoto ukiwa na miaka 40 ukifika miaka 70 mwanao atakua na miaka 30 nini mbaya hapo?
Good boss,, 70 kwa 30 sio mbaya
 
Kuna umri mwanadamu akifikia huwa anapaswa kuomba ushauri tu na sio maamuzi.

Ulipofikia kwa sasa unapaswa kujiamulia ya kwako kwa kuzingatia ushauri wao kama tu unaona unakufaa.

Muoaji ni wewe sasa jubilee na makaburi vinahusiana nini na ndoa yako? Kama upo tayari kwa ndoa, toa taarifa tu, anaehisi anahusika atakuja kushirikiana na wewe, anaehisi jubilee ya babu ni muhimu zaidi na aende kwa babu watakuta ushaoa tu.

Maisha yanakwenda kasi mno kuridhisha kila mtu, mwisho wa siku anaehusika na furaha na huzuni yako ni wewe mwenyewe. Wengine wasindikizaji tu.
 
Habari yako ndugu yangu
Kaka usiumizwe kabisa na kitu kinaitwa ndoa abadan!, ndoa ni utapeli, ndoa ni scam,ndoa ni utumwa,ndoa ni kifungo,ndoa ni mateso,unaoa ili iweje? **** ziko mingi sana kaka,tafuta wanawake watatu wazuri wenye tabia nzuri kiasi wazalishe,wahudumie na wanao, somesha wanao na uishi kwa furaha, ulishawaza kutombewa? Yaaani mkeo anainamishwa,anawekwa dudu anamwagiwa ndani, anachubuka kei? Achana na ndoa, utakosa uhuru binafsi na utaishi maisha ya majuto,binafsi,embu focus na maendeleo kaka,halafu wanawake wengi sana ni wazuri, why uoe ulombe mmoja mpaka siku unakata roho? Naenda kula mke wa jamaa yangu nitakucheki baadae
 
Hili jambo linanitafakarisha sana wanajamii!!

Habari!?

Mimi ni kijana wa makamo, natoka familia ya kawaida, baba alikua mtumishi na mama ni mama wa nyumbani tu!

Nina changamoto Moja hivi, naomba kushea mnipe mawazo walau nijue naanzia wapi.

Nina miaka 34 Sasa naelekea 35, Sina familia swala ambalo nilikua na sisitizwa sana na baba (si baba mzazi, mama aliolewa nikiwa nimezaliwa), baba huyu ananipenda sana, hivyo mara kadhaa huniomba ushauri na msaada na mara nyingi namsaidia, ikiwa ni pamoja na kuwasomesha wadogo zangu.

Mwaka Juzi niliachana na mchumba Ambae nilidhani tungeoana, ni mambo ya vijana Kila mtu ana sababu zake. (Ameshaolewa na Wana maisha Yao)

Ilibdi niwaze kumpata mtu Ambae ninafahamiana nae, anatoka maeneo ya nyumbani.

Kuna binti mmoja ni mtoto wa rafiki yake na baba, walikua marafiki sana, huyo binti niliwahi kumtongoza kipindi Cha nyuma, wakati tunasoma aligoma, nikamwacha. Baba yake alifariki na wakati anafariki baba ni kama alikua mwangalizi wa familia hii.

Katika pita zangu juzi nikiwa single nimeachana na aliekuwa mchumba, nikakutana nae, ameachwa na waliekuwa nae na kibaya zaidi ana mtoto mmoja.

Nilimweka karibu kwanza kumchunguza, nilivutiwa nae kwa vingi, mapambano yake na historia mbaya sana aliokuwa akinipa kuhusu baba wa mwanae.

Tulienda muda kidogo tukaanza mahusiano, nikiwa makini sana, aaah huyu dada nilijikuta nampenda sana kama mwanzo, very organized, focused, nk nk, yaan package full, japo Kila nikisoma story za usioe single mother naishiwa pawa.

Anyway juzi hapa nikaona nimwoe, baada ya nyumbani pia kusema ni muda Sasa wa kuwa na mchumba, (baba alikua anajua tyari nilimwambia na alifurahi niwe na mtoto wa rafiki yake)

Nilijipanga nikaenda nyumbani kusema official, walifurahi na binti kwao walifurahi sana maana walikua wakitufahamu Toka tukiwa wadogo.

Shida Sasa ikaanza baada ya Mimi kurudi, nikapigiwa simu na dada mkubwa (ameachana na mume wake) ninaemfuata, akaniambia 'wewe kwanini unataka kupush sana mambo Yako wakati unaona nyumbani sahivi Kuna tukio la ukoo, Babu anataka kufanya jubilei' nilishangaa maana Mimi sikua na hizo taarifa, na kwa maelezo ya baba, mwezi wa 10 mwaka huu nilikua niwe na ndoa.

Nikamwambia asirudie kuniambia hivyo maana mm sijalazimisha chochote! Na nilikua sijui lolote,


Kilichofuata baba aliniambia ataenda kwa wakwe kuanza michakato, nikawa napigwa kalenda sana, mwisho akaniambia tatizo ni pesa nikamtumia, lkn Bado nikawa napigwa kalenda.

Hatimaye siku Moja mama akanipigia simu usiku, akaniambia, wewe...... Huoni Kuna Nini hapa nyumbani, tukio la Babu, na tunataka tutengeneze makaburi ya ukoo, nikamwambia mama mbona hivyo vitu havina gharama na vinaweza kwenda pamoja, akapata kigugumizi akaanza kunipa sababu zingine mwisho nikaanza kuonekana mkosaji Tena.. nikanyamaza.

Week kadhaa siku Moja baba akanipigia simu mchana akaniambia, usiwe unaongea nao sana hao, subiri mwakani hata mwezi wa kumi huko tutafanikisha...

Nilishangaa sana maana mwanzo nilikua nahamasishwa sana lkn sahv yamekuwa hayo...


Nipeni mawazo watu wangu wa maana, nianzie wapi? Nisije jikuta nachelewa zaidi na zaidi!
Ukiwa mtu mzima mambo mengine uwe unaamua tu mwenyewe ukitegemea sana kupangiwa mambo na mama sijui dada watakukwamisha shauri yako
 
Umekosea Sana huyo single mother ungemsaidia Kama amekwama Ila kumuoa ni makosa Makubwa unaenda kufanya .


Pili - unabidi kutumia Akili kufanya maamuzi na sio kuendeshwa na inawezekana wewe ni Bread winner katika hiyo familia , wameingiwa na hofu baada ya Kutangaza Ndoa wakihisi hautakuwa na habari nao ukioa .


Cha kufanya

-Achana na single mother na kaa nao mbali hao watu wamechafukwa roho na nafsi watakuumiza vibaya mno kwakuwa wako na bad experience kwenye mahusiano.



Wanawake ambao hawafai kusogelewa ni

-Single mothers
-Broke women
-And a woman who is unhappy

Ukikutana na wanawake wa hivi wasaidie walipokwama Ila usianzishe nao mahusiano.
Sasa mkuu mama ake aliolewa na baba mwengine akiwa na watoto na life likawa good.....acha kijana abahatishe bahati yake,yakimshinda atabwaga manyanga.

Mwanaume hakosei kuoa....labda atapoteza pesa tu
 
Habari yako ndugu yangu
Kaka usiumizwe kabisa na kitu kinaitwa ndoa abadan!, ndoa ni utapeli, ndoa ni scam,ndoa ni utumwa,ndoa ni kifungo,ndoa ni mateso,unaoa ili iweje? **** ziko mingi sana kaka,tafuta wanawake watatu wazuri wenye tabia nzuri kiasi wazalishe,wahudumie na wanao, somesha wanao na uishi kwa furaha, ulishawaza kutombewa? Yaaani mkeo anainamishwa,anawekwa dudu anamwagiwa ndani, anachubuka kei? Achana na ndoa, utakosa uhuru binafsi na utaishi maisha ya majuto,binafsi,embu focus na maendeleo kaka,halafu wanawake wengi sana ni wazuri, why uoe ulombe mmoja mpaka siku unakata roho? Naenda kula mke wa jamaa yangu nitakucheki baadae
We fala nimecheka sana,,, watakupaka mafuta
 
Single mother sikushauri bora hata malaya anaweza kutulia ,single mother au mwanamke mwenye mtoto automatically ameshahamisha mapenzi yake kwa mwanae.


Huyo atajali sana furaha ya mwanae ,usije kushangaa pakiwa na event ya mtoto wake ,baba wa mtoto huyo akaja na kupewa kipaumbele wewe ukabaki unatoa macho... Single mother na huyo jamaa wameshaunganishwa na kiroho kupitia mtoto labda mmoja kati yao afe ...Usikubali kabisa.


Vile vile ,tambua kwamba unaenda kuwa baba wa kambo moja kwa moja ,halafu pia elewa hautoweza kumzuia huyo kuzungumza na mzazi mwenzie kufanya hivyo ni kumnyima haki ya kupata malezi ya wazazi wote wawili huyo mtoto uliyemkuta.

Wanawake wanapenda ndoa kwa vile inawapa heshima kuliko hata pesa ila wengi hawana mapenzi ndani ya ndoa ,hapo ameshazaa so thamani yake imeshuka amekukubali ila ungemkuta kwenye peak asingekukubali ila ule ukweli anamkubali huyo jamaa aliyezaa naye.


Bora kuoa malaya ila single mother hapana kabisa..!
 
Nahisi kuna jambo linaendelea ila ni hisia tu, jaribu kuchunguza kwa watu wa karibu yani shangazi baba mdogo, mkubwa mama dogo,mkubwa wajomba marafiki wa karibu ndugu jamaa nk
 
Nikwambie kitu, fanya maongezi ya kiudadisi na mama yako kuna jambo utaligundua. Ila katika yote usikilize sana ushauri wa mama yako, yeye anajua zaidi namna ya kuishi na hao watu wa upande wa baba yako ikizingatiwa hata yeye huenda alipitia figisu nyingi wakati wewe ukiwa mdogo.

Laakini pia huenda kuna historia fulani juu ya huyo binti ambayo unafichwa usiijue. Usishtuke kuja kuambiwa huyo ni dada yako au tuseme mtoto wa huyo baba yako.
 
Inaonekana huyo binti ana matatizo wazazi hawataki kukwambia ongea nao vizuri wazazi wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom