Uchaguzi 2020 Ni wakati wa wafanyabiashara na Wadau wa Sekta Binafsi kumwadhibu Rais Magufuli

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Huu ni wito kwa Wafanyabiashara na Wadau wote wa Sekta Binafsi. Tafadhali sana ili maisha yenu yarejee kwenye kukuza na kuimarisha biashara zenu muondoeni huyu mtu kwenye sanduku la kura.

Mpigeni za uso ili mumkumbushe kwamba serikali iliyostaraabika duniani kote haimiliki njia za uchumi na pia haifanyi biashara bali inaweka mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Kwa miaka yote mitano Rais Magufuli amewaona wafanyabiashara na sekta binafsi kama wezi na adui wa Taifa. KITU AMBACHO SIYO KWELI HATA KIDOGO.

Rais Magufuli haamini kwamba Sekta Binafsi na biashara ni msingi wa uchumi imara.

Mfano mmoja pekee ni namna alivyoua mashirika binafsi ya ndege mfano wa fastJet, ingelikuwa ni Rais mwenye maono asingeliweza kununua midege ya serikali kwa fedha cash za Watanzania bali angetafuta wawekezaji wa uhakika tu wakawekeza kwenye shirika la ATCL ambalo bado lingefanya kazi ileile ya kuitangaza nchi, kuleta watalii n.k.

Fedha alizopeleka kwa anaowaita mabeberu ingeliboresha elimu ambayo tayari haina ubora wowote kwenye soko la ajira hata la Afrika Mashariki achana na soko la ajira la dunia.

NI HAYO TU KWA LEO, NAWATAKIA SIKU NJEMA.
 
M
Naunga hoja hii mkono, aadhibiwe bila huruma!
Mlikuwa mafisadi wa kibiashara sasa mnaumwa, na kwenye miladi ya serikali mlikuwa mnatengeneza chini ya kiwango kwa ghalama kubwa na sio kumaliza kwa wakati, sasa joto linawachoma manalialia.

Tulieni sindano iwaingie.
 
M
Mlikuwa mafisadi wa kibiashara sasa mnaumwa, na kwenye miladi ya serikari mlikuwa mnatengeneza chini ya kiwango kwa ghalama kubwa na sio kumaliza kwa wakati, sasa joto linawachoma manalialia.

Tulieni sindano iwaingie.
Waweza kutuonesha mradi hata mmoja ulioujenga Rais Magufuli kwa viwango bora vya kidunia utakaodumu hata miaka 5? Wewe subiri kushuhudia hasara ambavyo mtu huyu amelipatia Taifa kwa miradi yake ya one man show na ya kukurupuka.
 
CreativityCode,

Wakiwamo hawa wanaoathirika huku kwa uzembe wa mamlaka uliopitiliza:

IMG_20200810_152339_062.jpg

IMG_20200808_085621_609.jpg

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea
 
M
Mlikuwa mafisadi wa kibiashara sasa mnaumwa, na kwenye miladi ya serikari mlikuwa mnatengeneza chini ya kiwango kwa ghalama kubwa na sio kumaliza kwa wakati, sasa joto linawachoma manalialia.

Tulieni sindano iwaingie.
Mkuu mtoa hoja kazungumzia kuhususu kuboresha elimu hujaona kama ni hoja pia angalia hadi Leo kuandika maneno kwa usahihi hauwezi angalia maneno haya chini.

Mladi

Ghalama

Lakini wewe huwezi jua hayo unaona sawa tu si ajabu ukawa umehitimu hadi chuo kikuu.
 
Mpiga kura nawasoma kisha nasema hiiiii.

Sema nyie watu mnabadili saana ID, nawaambieni nawapa miaka 10 tu, mtamlilia Magufuli kama wengi wenu mnavyomlilia JK.

Mliyemtukana na kumwambia ni goigoi, kageuza nchi shamba la bibi. Ni suala la muda tu.
 
CreativityCode,

Acha ndugu kuna Rhino cement, Quality Group, Bank M, Shivacom, Smile communications, Schlumberger( Hawa ni kampuni ya kuchimba mafuta Mtwara na LINDI), Shoprite Supermakert, Nakumatt, Choppies Supermarket, Tumaini Hospital, Impala hotels bado wa Maduka ya kariakoo pale.

Huyu mzee Kaharibu hii nchi nawaambia
 
Kuna Ukiowataja hhaoo hadi roho imeniuma...waliondoka kwa maumivu makali sana
 
Acha ndugu kuna Rhino cement, Quality Group, Bank M, Shivacom, Smile communications, Schlumberger( Hawa ni kampuni ya kuchimba mafuta Mtwara na LINDI), Shoprite Supermakert, Nakumatt, Choppies Supermarket, Tumaini Hospital, Impala hotels bado wa Maduka ya kariakoo pale.

Huyu mzee Kaharibu hii nchi nawaambia

Walizoea kulipa kodi kiujanja ujanja, na hiyo ndo shida ya wafanya biashara wa Afrika, hata faida wanazopata za kifisadi huwa hawazitunzi kwa tahadhali mambo yakibadilika.
 
Walizoea kulipa kodi kiujanja ujanja, na hiyo ndo shida ya wafanya biashara wa afrika, hata faida wanazopata za kifisadi huwa hawazitunzi kwa tahadhali mambo yakibadilika.
Kwa iyo Kama Kuna issues za kikodi badala mkae nao kujadili nyie mnawafirisi na kuwafanya waondoke????

Hiyo ni akili au matope???? Unajua watu wangapi wamepoteza ajira na familia ngapi zimeathilika kwa hao watu kupoteza ajira???? Unajua wawekezaji wangapi wamesita kuja baada ya kuona hayo??? Unajua kwa wao kutokuwepo tu hata kodi ndogo Tuliyokuwa tunapata kutoka kwao tumeikosa???

Kweli CCM hivyo vichwa mnafugia nywele tu!!
 
Kwa iyo Kama Kuna issues za kikodi badala mkae nao kujadili nyie mnawafirisi na kuwafanya waondoke?

Hiyo ni akili au matope? Unajua watu wangapi wamepoteza ajira na familia ngapi Zim wat Hillis kwa hao watu kupoteza ajira? Unajua wawekezaji wangapi wamesita kuja baada ya kuona hayo??? Unajua kwa wao kutokuwepo tu hata kodi ndogo Tuliyokuwa tunapata kutoka kwao tumeikosa?

Kweli CCM hivyo vichwa mnafugia nywele tu!
Huwezi kudaiwa kodi milioni kumi na wakati umebaki na laki tano ukaweza kufanya majadiliano, na ndo maana nimesema waafrica, ukipata pesa itokanyo.na ufisadi huwezi kuitunza bali unatumia hovyo, sasa siku ukidaiwa unakuta huna kila kitu.
 
Sidhan kama kuna mtu mwenye akili timamu anamlilia Jk.Wewe sema kinachofanyika ni watu kufanya comparison, sasa kama hakuna wanaomlilia Jk bali kumlinganisha tu na jpm nakuona jk alikua na afadhali sidhani kama kuna wakumlilia Jpm, labda wale wanaonufaika naye.Na hiyo ipo dunia nzima kwamba kiongoxi huwezi kupendwa na wote na wala kuchukiwa na wote.
Mpiga kura nawasoma kisha nasema hiiiii.

Sema nyie watu mnabadili saana ID....nawaambieni nawapa miaka 10 tu...mtamlilia Magufuli kama wengi wenu mnavyomlilia JK.

Mliyemtukana na kumwambia ni goigoi...kageuza nchi shamba la bibi. Ni suala la muda tu.
 
Huwezi kudaiwa kodi milioni kumi na wakati umebaki na laki tano ukaweza kufanya majadiliano, na ndo maana nimesema waafrica, ukipata pesa itokanyo.na ufisadi huwezi kuitunza bali unatumia hovyo, sasa siku ukidaiwa unakuta huna kila kitu.
Kwa iyo hao wote hawakuwa na pesa. Samahani nakutukana ndugu. Akili yako haina akili! Watu wameumia kwa kukosa ajira na familia zao zinateseka alafu mnaleta maneno ya kebehi hapa? Kweli CCM sio watu kabisa.
 
Kwa iyo Kama Kuna issues za kikodi badala mkae nao kujadili nyie mnawafirisi na kuwafanya waondoke?

Hiyo ni akili au matope? Unajua watu wangapi wamepoteza ajira na familia ngapi Zim wat Hillis kwa hao watu kupoteza ajira? Unajua wawekezaji wangapi wamesita kuja baada ya kuona hayo??? Unajua kwa wao kutokuwepo tu hata kodi ndogo Tuliyokuwa tunapata kutoka kwao tumeikosa?

Kweli CCM hivyo vichwa mnafugia nywele tu!
Mbona hata mbele watu wanataifishwa kwa kukwepa kodi
Na kwao hakuna kosa kubwa kama kukwepa kodi
 
Huyo jamaa hujui lolote kakaririshwa.Ukimpiga maswali ya msingi utaitwa mchochezi au sio mzalendo.
Kwa iyo Kama Kuna issues za kikodi badala mkae nao kujadili nyie mnawafirisi na kuwafanya waondoke????

Hiyo ni akili au matope???? Unajua watu wangapi wamepoteza ajira na familia ngapi zimeathilika kwa hao watu kupoteza ajira???? Unajua wawekezaji wangapi wamesita kuja baada ya kuona hayo??? Unajua kwa wao kutokuwepo tu hata kodi ndogo Tuliyokuwa tunapata kutoka kwao tumeikosa???

Kweli CCM hivyo vichwa mnafugia nywele tu!!
 
Sidhan kama kuna mtu mwenye akili timamu anamlilia JK. Wewe sema kinachofanyika ni watu kufanya comparison, sasa kama hakuna wanaomlilia Jk bali kumlinganisha tu na jpm nakuona JK alikua na afadhali sidhani kama kuna wakumlilia Jpm, labda wale wanaonufaika naye.Na hiyo ipo dunia nzima kwamba kiongoxi huwezi kupendwa na wote na wala kuchukiwa na wote.
Magufuli anafanya mengi mabaya kuliko kikwete hadi watu wanamiss kikwete. Ushawai ona Kikwete anawadhihaki watu waliopatwa na maafa?
 
Mbona hata mbele watu wanataifishwa kwa kukwepa kodi
Na kwao hakuna kosa kubwa kama kukwepa kodi
Unajua mbele mpaka kitu kitaifishwe wanapitia hatua gani?

Messi alishawai kuwa na kesi ya kodi ulishawai sikia account yake imekuwa freezed??? Au amezuia kucheza mpira hadi kesi yake ya kodi ilipoisha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom