Ni wakati sasa makanisa na misikiti kulipa kodi ili wapate uchungu na kusimamia HAKI

Ni wakati sasa makanisa na misikiti kulipa kodi ili wapate uchungu na kusimamia HAKI

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,691
Reaction score
2,303
Makanisa na misikiti kutolipa kodi ni RuSHWA kwa viongozi wao ili wasikemee maovu au ili waitetee serikali kwa uovu wake.

Kwa misingi hiyo makanisa na misikiti anze kitoa stakabadhi za malipo za EFD kwa kila pesa wanayopokea na kwa kila shughuli watakayoendesha.

Haiingiit akilini eti mfanyabisshara yeye apeleke hesabu zake tra hata kama hajafanya biashara yoyote akishindwa alipe faini ila makanisa na misikiti wao hapana.
 
Ushaambiwa wale hawafanyi biashara watalipaje kodi?
 
Ushaambiwa wale hawafanyi biashara watalipaje kodi?
Hawafanyi biashara kwahiyo unasupport ujinga huo?RC wana maduka,nyumba za kupangisha,frames,hostels,nk wanapata pesa halafu unaleta ujinga,uwe serious!!
 
😄😄😄😄tutaacha kwenda kanisani yani hela yangu iliwe na hao jamaaa
 
Hawafanyi biashara kwahiyo unasupport ujinga huo?RC wana maduka,nyumba za kupangisha,frames,hostels,nk wanapata pesa halafu unaleta ujinga,uwe serious!!
Kwa uelewa wangu, kanisa halilipi kodi ila kama wana uwekezaji huo uwekezaji unalipa kodi...

Kwa mfano kanisa likifungua duka ni lazima walipe kodi...

Niko tayari kusahihishwa.
 
Kwa uelewa wangu, kanisa halilipi kodi ila kama wana uwekezaji huo uwekezaji unalipa kodi...

Kwa mfano kanisa likifungua duka ni lazima walipe kodi...

Niko tayari kusahihishwa.
Uko sahihi ndivyo ilivyo!
Kanisa au msikiti ukianzisha kitega uchumi chochote huwa wanalipa kodi!
 
Uko sahihi ndivyo ilivyo!
Kanisa au msikiti ukianzisha kitega uchumi chochote huwa wanalipa kodi!
Soma uzi vzr na uuelewe unacholisema kimesemwa tayari bali sadaka na vitu wanaavyoingiza nchini navyo vitozwe kodi sasa
 
Ezra 7:11-26
Ifuatayo ni barua ambayo Artashasta alimpa Ezra, kuhani na mwandishi, na mwenye ujuzi katika amri na masharti ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli.
12“Kutoka kwa Artashasta, mfalme wa wafalme, kwa Ezra, kuhani na mtu mwenye ujuzi katika sheria ya Mungu wa mbinguni; Wasalaam!”
13“Ninaamuru kwamba katika utawala wangu, Mwisraeli yeyote, au kuhani wao, au Mlawi, akitaka kurudi Yerusalemu kwa hiari yake, anaweza kwenda pamoja nawe.
14“Mimi pamoja na washauri wangu saba, tunakutuma uende ufanye uchunguzi huko Yuda na Yerusalemu kuona kama sheria ya Mungu wako ambayo umekabidhiwa inafuatwa kikamilifu. 15Utachukua fedha na dhahabu ambayo mimi na washauri wangu tumemtolea kwa hiari Mungu wa Israeli ambaye hekalu lake limo mjini Yerusalemu. 16Utachukua pia fedha na dhahabu yote utakayokusanya katika mkoa wote wa Babuloni, pamoja na matoleo ya hiari waliyotoa Waisraeli na makuhani wao kwa ajili ya nyumba ya Mungu wao iliyoko Yerusalemu. 17Fedha hiyo utaitumia kwa uangalifu sana kununua mafahali, kondoo dume, wanakondoo na tambiko ya nafaka na divai, na kuvitoa madhabahuni katika nyumba ya Mungu wenu iliyoko Yerusalemu. 18Fedha na dhahabu itakayobaki unaweza kuitumia pamoja na wananchi wenzako kama mtakavyopenda, kufuatana na mapenzi ya Mungu. 19Vyombo ambavyo umekabidhiwa kwa ajili ya ibada ya nyumba ya Mungu wako, utamtolea Mungu wa Yerusalemu. 20Ukihitaji kitu kingine chochote kwa ajili ya nyumba ya Mungu wako unaweza kukipata kutoka katika hazina ya mfalme. 21Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa waweka hazina wote katika mkoa wa magharibi ya mto Eufrate kwamba chochote atakachohitaji Ezra, kuhani na mwandishi wa sheria ya Mungu wa mbinguni, mtampa, tena bila kusita, 22fedha kiasi atakacho mpaka kufikia kilo 3,400, ngano kilo 10,000, divai lita 2,000, mafuta lita 2,000, na chumvi kiasi chochote atakachohitaji. 23Kila kitu alichoagiza Mungu wa mbinguni kwa ajili ya nyumba yake, ni lazima kitekelezwe kikamilifu, asije akaukasirikia ufalme wangu au wanangu. 24Tunawafahamisheni pia kuwa ni marufuku kuwadai kodi ya mapato, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, walinda mlango, wafanyakazi au watumishi wengine wa nyumba hii ya Mungu. 25Nawe Ezra, kwa kutumia hekima aliyokupa Mungu wako, hiyo uliyonayo, chagua mahakimu, na waamuzi watakaowaongoza wakazi wote wa mkoa wa magharibi ya Eufrate ambao wanaishi kufuatana na sheria ya Mungu wako. Na yule ambaye haijui sheria hiyo, mfundishe. 26Mtu yeyote ambaye hatatii sheria ya Mungu wako na ya mfalme, na ahukumiwe mara moja: Kufa, kuhamishwa, kunyanganywa mali yake au kufungwa.”
 
Back
Top Bottom