Ni wachache wenye kuijua JamiiForums

Ni wachache wenye kuijua JamiiForums

Hata watu waliomo humu kuwajua ni bahati sana kama sio verified user hao ma mods tu ukipata bahati ya kuwaona ujue siku hiyo utapata barua ya promotion kazini
 
Nimeujua huu mtandao nikiwa kidato cha tano na sasa nipo chuo lakini nikimuona mwanachuo mwenzangu haujui namuona bonge la mshamba.
Maana madini ninayoyapata kwenye majukwaa kama ya biashara na uchumi na mada kali za humu ni shida.
Yaani hadi nina note book ya kuandika tittle za baadhi ya mada for future use
 
Ila wengi unawakuta wapo JF ila wanaficha tu. Mara nyingi mtu akijitathimini hadhi aliyo nayo katika jamii na vitu anavyopost JF anaona bora ibaki siri tu kama hayupo.

Mfano mimi kwenye simu yangu hata Icon ya JF App huezi iona. Nimeficha maana simu yangu nimeset gestures, nikislide up na kidole app inafunguka, na ukiniuliza nakwambia JF siijui.
 
Mkuu si unajua wabongo tunatakaga mahali ambapo unaweza kuuza sura... mastaa wengi wanaochipukia saivi wanapata umaarufu through instagram of which jamii forum haiwezekani, ndo maana watu hawapendi kujiunga coz huku kumekaa kisomi Sana!! hakuna kubinua kiuno
Poit
 
inawezekana tena wengi mno hawaijui maana ata ukiangalia idadi ya watu tuliojiunga humu ni 345968.....yani laki 3 ata na nusu atujafika hivyo ili iwe imewafikia watu wengi atleast ingekuwa na memba milioni 10 na kuendelea.
  • MEMBERS 345,968
Ni kweli mkuu lakini watu wengi wanapenda kuingia huku as guests hata mie nilitumia zaidi ya mwaka ndo nikaamua kuwa member
 
Wadau nimejaribu kufanya utafiti kwa watu tofauti walio kwenye serikali hata nje ya serikali, watu wengi nimekua nikiwakuta wanashinda kwenye mitandao ila cha kushangaza kila ninaemuuliza kuhusu jf anasema hajui.

Hapa kwa mtazamo huu nimekua nikitafakari na kujiuliza mwenyewe kwanini waliowengi hawaujui mtandao wa jf?

Nimeamua kushea na nyinyi ili tuchangie mawazo mi binafsi sikuelekezwa na mtu mtandao huu, naweza kusema ni kama bahati kuja huku na sijui nilifikaje.
Labda huko kwenu zanzibar
 
Mimi JF nilianza kuiona kwa bro wangu flani ivi wakati huo hata simu sijaanza kumiliki, enzi hizo niko primary,
 
Kuna sababu nyingi zinaifanya JamiiForums isijulikane,ila kubwa ni kuitangaza,hii kwa juu juu inaweza kuonekana kama jambo rahisi lakini sivyo!,

JamiiForums siyo mtandao wa mtu au kampuni binafsi,yaani wanaoiendesha JamiiForums sio walioiandikia code na kuifanya iwe web na mobile application kama ilivyo kwa facebook,instagram au whatsapp,ambapo hizo apps ziko chini ya maprogrammer walio ziandika code zake na hivyo wana hakimiliki ya apps zao!

,kwaiyo wanaweza wakafanya chochote kwa kuwa ni za kwao lakin hali sivyo ilivyo kwa jamiiforums,forums zinakodishwa na kuwa hosted na server za hao wanaozidesign,

kuna forums nyingi Sana duniani na kama zimedizainiwa na kampuni moja basi utakuta zote zinafanana kwa kila kitu isipokuwa lugha tu!,mfano Jamiiforums inafanana kwa kila kitu na AndroidForum isipokuwa lugha tu!

,kwaiyo huwezi kupewa mamlaka makubwa kama kumodify source code na mengine ila utakua Admin tu na kila kitu kinachohusiana na code au modification hakitakuhusu,kwaiyo wanaoiendesha jamiiforums hawazijui hata source code zake!,wao ni maadmin tu kama wewe ukiwa na website ya WordPress,

kila kitu utategemea plugins kwasababu hujui source code zake!,Kwaiyo ukizilinganisha forums na hizo high-tech apps unakosea!,Facebook utaiponda utakavyo lakin ni mara mia mbili bora kuliko jamiiforums(no-offense),Facebook inafeatures nyingi zinazotegemea a hundreds of serves na more than one programming language lakin Jamiiforums haiko hivyo,

kwa mtu asiye na ufahamu wa computer naweza kumfananishia forums na group la whatsapp ili anielewe ninachokieleza.mfano,kwenye group la whatsapp mtu akipost stori,members wanaweza kuiona na kuchangia,tofauti na whatsapp ni kwamba kwenye forums admin anapewa notification kwa email Kama kuna stories mpya imewekwa na yeye ataamua aitoe au aiache,

vivyo hivyo kwa users,ukijisajili kwenye forums admin anaweza kukutoa.Kwa kifupi ni kuwa forums zikiwa na maudhui tofauti ni kama admin mmoja ana magroup zaidi ya moja na kila moja lina mada tofauti ila users wa kila group wanaweza kuinteract na wengine kwenye group lingine bila wao kujua wanatoka group lipi!,

kwaiyo huwezi kwenda kwenye media ukaanza kuyanadi magroup yako ya whatsapp,hiyo inakua ni free advertising kwa Whatsapp wenyewe!
 
Ni kweli wengi hawaijui na Mimi niliijua kupitia Google kuna kitu nilitafuta huko lakini jibu likaja kutoka JF nikashangaa ndo mtandao gani lakini kuanzia nimejiunga am not the same.
 
JF kwa sasa imepoteza mwelekeo. May be sababu ya censorship na uvamizi wa vijana wa Facebook; na mengineyo. Mtandao wa kwanza Bongo kwa sasa ni Millard Ayo

Jamiiforums ni discussion forums (jukwaa la majadiliano sambamba na kuhabarishana) ila Millard ayo ni mtandao wa kukuhabarisha na ni sawa na Blog zingine.
 
inawezekana tena wengi mno hawaijui maana ata ukiangalia idadi ya watu tuliojiunga humu ni 345968.....yani laki 3 ata na nusu atujafika hivyo ili iwe imewafikia watu wengi atleast ingekuwa na memba milioni 10 na kuendelea.
  • MEMBERS 345,968

Kuna wenye ID's mbili mbili ,ktk hizo NUMBER
 
Yaah mimi mwenyewe nimeijua 2014 baada ya masomo ya A'level nikawa viewer na nimejiunga mwaka jana mwishoni.
 
Back
Top Bottom