Ni wachache wenye kuijua JamiiForums

Ni wachache wenye kuijua JamiiForums

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,474
Wadau nimejaribu kufanya utafiti kwa watu tofauti walio kwenye serikali hata nje ya serikali, watu wengi nimekua nikiwakuta wanashinda kwenye mitandao ila cha kushangaza kila ninaemuuliza kuhusu jf anasema hajui.

Hapa kwa mtazamo huu nimekua nikitafakari na kujiuliza mwenyewe kwanini waliowengi hawaujui mtandao wa jf?

Nimeamua kushea na nyinyi ili tuchangie mawazo mi binafsi sikuelekezwa na mtu mtandao huu, naweza kusema ni kama bahati kuja huku na sijui nilifikaje.
 
inawezekana tena wengi mno hawaijui maana ata ukiangalia idadi ya watu tuliojiunga humu ni 345968.....yani laki 3 ata na nusu atujafika hivyo ili iwe imewafikia watu wengi atleast ingekuwa na memba milioni 10 na kuendelea.
  • MEMBERS 345,968
 
Inajulikana na wenye upeo mkubwa wa kufikiri na wale wanaopenda kujua mambo yanayoihusu Tanzania na watu wake wakiwemo viongozi..kama mimi nimeijua toka 2009 nikashawishika kujiunga 2012 na nikawashawishi ndugu na jamaa zaidi ya 20 ila ni moja ya mtandao unaoheshimika na wengi huwa wanaogopa kujiunga kwa kudhani waliopo humu wengi ni wasomi na ndomana JF ina Viewers wengi ambao hawajajiunga
 
Wadau nimejaribu kufanya utafiti kwa watu tofauti walio kwenye serikali hata nje ya serikali, watu wengi nimekua nikiwakuta wanashinda kwenye mitandao ila cha kushangaza kila ninaemuuliza kuhusu jf anasema hajui. Hapa kwa mtazamo huu nimekua nikitafakari na kujiuliza mwenyewe kwanini waliowengi hawaujui mtandao wa jf.
Nimeamua kushea na nyinyi ili tuchangie mawazo mi binafsi sikuelekezwa na mtu mtandao huu, naweza kusema ni kama bahati kuja huku na sijui nilifikaje.
Mkuu umedanganyika tu,kuna watu Wengi tu huwa wanaficha mambo yao
 
Wadau nimejaribu kufanya utafiti kwa watu tofauti walio kwenye serikali hata nje ya serikali, watu wengi nimekua nikiwakuta wanashinda kwenye mitandao ila cha kushangaza kila ninaemuuliza kuhusu jf anasema hajui. Hapa kwa mtazamo huu nimekua nikitafakari na kujiuliza mwenyewe kwanini waliowengi hawaujui mtandao wa jf.
Nimeamua kushea na nyinyi ili tuchangie mawazo mi binafsi sikuelekezwa na mtu mtandao huu, naweza kusema ni kama bahati kuja huku na sijui nilifikaje.
Tufanye mkakati wa kuitangaza.
 
Wengi wanaijua sana ila hawana uwezo wa kuwa huku.
 
Uwe unaangalia na aina ya watu unaowauliza kuhusu jamii forums..

Wewe unaenda kuuliza mtu anaandika (x) badala ya (s)..

Mwingine anaandika kiswahili hata hakieleweki ataijua vipi Jf..

Wengi wanaijua Jf lakini hawawezi kuwa humu kutokana na kuogopa kuandika upuuzi na kukosolewa..maana huku nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi..

Ukiandika upuuzi mtu "anakulima" anatembea!
 
asilimia 80 ya watanzania wanatumia facebook,snapchat,badoo,tango,viber,instagram,whatsapp na imo.vyengine paka wasikie mtu maarafu anatumia
 
Mkuu si unajua wabongo tunatakaga mahali ambapo unaweza kuuza sura... mastaa wengi wanaochipukia saivi wanapata umaarufu through instagram of which jamii forum haiwezekani, ndo maana watu hawapendi kujiunga coz huku kumekaa kisomi Sana!! hakuna kubinua kiuno
 
Back
Top Bottom