Ni vigumu sana kuwatofautisha Zitto na Halima Mdee

Kamanda
Wakati wa uchaguzi mkuu 2020 aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chadema Halima Mdee aliutangazia umma kuwa amekamata mabegi yenye kura feki akasema hatotambua matokeo yake leo kaungana na waliomuibia kura.

Jana kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo ya Muhambwe na Buhigwe.

Asubuhi: Zitto Kabwe, tumetekwa na watu wenye mapanga maisha yetu yako hatarini, kuna magari matatu yamejaza maboksi yenye kura feki.

Jioni: Zitto, naipongeza CCM kwa ushindi wa halali kabisa Tume ya Uchaguzi imefanyakazi yake kwa weledi.

Binafsi nashindwa kuwatofautisha wanasiasa hawa wawili ndumilakuwili ukiwaacha (Mrema, Cheyo na Lipumba) matendo yao yanafanana kwa kiwango kikubwa ni waongo, wanafiki, wasaliti, hawaaminiki na wachonganishi. Wanataka wao ndio waonekane wanajua siasa kuliko wengine na la mwisho zaidi wote wawili ni ‘Opportunist’ wanaangalia maslahi yao kwanza.
 
Zito haaminiki ni kawaida yake unafiki ndo maana alikuwa hapatani na mwenfazake.
Awaombe msamaha watanzania kwa kuzusha uongo.
 
Mimi sikubaliani kabisa na uvunjifu wa katiba unaofanywa na Dola kwenye sakata la kina Mdee.

Ila hawa MACHAGA kuanzisha league za kumshambulia kila anayekosana na Mbowe ni uwendawazimu wa kipuuzi kabisa.
Ligi ya Mbowe na dola kuvuja katiba vinahusiana vipi.
 
Post inamhusu Zitto Kabwe na Halima Mdee, lakini michango ya vijana wa MATAGA na UVCCM imehamishia mashambulizi kwa Mbowe. Hakika Mbowe ni mwamba wa siasa za mageuzi Tanzania
 
Sijawahi kumwamini Zitto !! Kuna muda nilijitahidi sana kufanya hivyo ila nafsi ikanigomea hadi leo hii.
Kwenye siasa Zitto ni mjanja sana akiwa na uhitaji fulani atakuja kuomba ushirikiano akiona hapati anachotaka huwa haoni aibu kuwasaliti wenzake kwa visingizio cha kila chama kina maamuzi yake.

Baada ya uchaguzi wa 2020 Chadema na ACT waliingia makubaliano ya kutoshiriki uchaguzi wowote chini ya tume hii baadae akasema ATC watagombea eti wanamjaribu Mama.
 
kweli kabisa, huu ndiyo msingi wa hoja yangu kwamba huyu jamaa any time anaweza kufanya U-turn na kukukaanga bila kujali madhara utakayoyapata kama Wewe, Chama chenu ama taifa kwa ujumla, anaangalia maslahi yake kwanza.

Unakwenda kufanya nini kwenye uchaguzi mdogo kama
1. Mfumo ni uleule
2. Tume ni ile ile
3. Sheria ni zilezile
4. Watu ni walewale na wanafanya kazi kwa mtindo uleule ( Wasimamizi na mapolice)
5. Mtangaza mshindi ni yuleyule na anariport kwa boss wake yule yule ambaye ni Mwenyekiti wa chama mnachogombaniana nafasi.
6. Unakwenda kwenye uchaguzi bila lalamiko lako hata moja kufanyiwa kazi, ukijipa moyo kwamba mwendazake kashaenda wacha tumjaribu bi - mkubwa....

Zitto bana wakati mwingine...
 
Mimi nafikiri kama Zitto kachagua ‘siasa njaa’ aachwe na harakati zake na upande mwingine uendelee na mipango yake, kumlazimisha mtu mzima kama Zitto kushirikiana ni kupoteza muda anajua anachokitafuta, ni sawa na kumnyang’anya fisi fupa hawezi kuliachia.
 
Ni vigumu sana kutofautisha chuki ya CHADEMA mliyonayo kwa Zitto na chuki waliyonayo CCM kwa Tundu Lissu.

Kitu pekee ambacho CHADEMA hamjakifanya kwa Zitto ni risasi 36 tu.
Duh!.… We jamaa wewe, hiyo sentensi yako ya mwisho waombe radhi Chedema.
 
Wakati wa uchaguzi mkuu 2020 aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chadema Halima Mdee aliutangazia umma kuwa amekamata mabegi yenye kura feki akasema hatotambua matokeo yake leo kaungana na waliomuibia kura.

Jana kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo ya Muhambwe na Buhigwe.

Asubuhi: Zitto Kabwe, tumetekwa na watu wenye mapanga maisha yetu yako hatarini, kuna magari matatu yamejaza maboksi yenye kura feki.

Jioni: Zitto, naipongeza CCM kwa ushindi wa halali kabisa Tume ya Uchaguzi imefanyakazi yake kwa weledi.

Binafsi nashindwa kuwatofautisha wanasiasa hawa wawili ndumilakuwili ukiwaacha (Mrema, Cheyo na Lipumba) matendo yao yanafanana kwa kiwango kikubwa ni waongo, wanafiki, wasaliti, hawaaminiki na wachonganishi. Wanataka wao ndio waonekane wanajua siasa kuliko wengine na la mwisho zaidi wote wawili ni ‘Opportunist’ wanaangalia maslahi yao kwanza.
Hebu imagine tu huyu ndie alikuwa anataka uenyekiti wa chadema.
 
Zito haaminiki ni kawaida yake unafiki ndo maana alikuwa hapatani na mwenfazake.
Awaombe msamaha watanzania kwa kuzusha uongo.
Zitto akishindwa uchahuzi husingizia WENZAKE wamemuangusha badala ya aliyeshindana naye CCM, na anaposema wenzangu wameniangusha mara nyingi humaanisha CHADEMA.

“Tuliamua kushiriki Uchaguzi. Wenzetu waliamua kususia. Tuliheshimu maamuzi yao. Tukapata Taarifa za kura feki, tukasema. Wenzetu wakasema ‘tuliwaambia’. Tukadhibiti kura feki. Lakini tukashindwa. Tuka-concede. Wenzetu wamenuna, wanatoka povu. Ni ushamba tu. Concession is so normal”. Zitto Kabwe.
 
Mimi nafikiri kama Zitto kachagua ‘siasa njaa’ aachwe na harakati zake na upande mwingine uendelee na mipango yake, kumlazimisha mtu mzima kama Zitto kushirikiana ni kupoteza muda anajua anachokitafuta, ni sawa na kumnyang’anya fisi fupa hawezi kuliachia.
Ni lini CHADEMA walishawahi kukaa na kukubaliana kuwa watashirikiana na chama kingine.

Leta hata uthibitisho wa agenda yoyote unaoonesha kuwa CHADEMA waliomba na kupigania kushirikiana na chama kingine.

CHADEMA huwa wakiona mgombea wao anakubalika hawataki kabisa ushirikiano na mtu. Kama unataka ushirikiano ni wewe ndio utatakiwa kuwaunga mkono.

Ni kundi la watu wabinafsi sana.
 
Kinachonishangaza kwa CHADEMA ni kumdharau Mdee kama vile ni takataka fulani. Mdee ameumizwa Mara ngapi kwa ajili ya CHADEMA? Hivi hiyo dhambi ya kwenda bungeni imemfanya Mdee kukosa thamani kiasi hicho?
Narudia kusema kwamba kama mnatuaminisha kuwa Mwendazake alikuwa Dikteta, mnayajua yaliyowakuta hao wanawake kabla ya kuapishwa? Wakati huo inasemekana nguvu ya dola ilitumika hata kumtoa mtu gerezani ili aapishwe. Kama ninyi mlivyotuamisha ina maana utawala wa amwendazake ulitumia nguvu ya dola kuhakikisha hawa wanawake wote wanaingia mtegoni.
Ni nguvu hiyo hiyo iliyosababisha wengine watoroke nchi, wengine kujisalimisha kabisa kwa kujiunga na sisiem, wengine kuishia magerezani. Hivi kwa nini hawa wanawake ndiyo waonekane wadhambi zaidi? CHADEMA mna haki kweli ya kuifundisha sisiem hekima? Kwa nini msipambane na mfumo mnaoamini ni kandamizi uliopelekea hao akidada kujisalimisha? Hilo tukio la hao Dada zenu mlioambatana nao siku zote kwenye siasa ya nchi hii na leo kuonekana takataka mbele zenu mkifanikiwa kuwaondoa mtakuwa mumetatua tatizo la nchi hii? Mnataka watoke muweke wake zenu?
 
Back
Top Bottom