Ni vigumu sana kuwatofautisha Zitto na Halima Mdee

Mimi nachukia matendo ya CHADEMA na siyo mwanachama wala msukule wa chama chochote kile.
Unachukia matendo ya Chadema yanayotendwa na mwanaCCM?

Hahaa sili nyama ya nguruwe ila mchuzi wake nakunywa. 😃😃😃😃
 
Ni lini CHADEMA walishawahi kukaa na kukubaliana kuwa watashirikiana na chama kingine.

Leta hata uthibitisho wa agenda yoyote unaoonesha kuwa CHADEMA waliomba na kupigania kushirikiana na chama kingine.

CHADEMA huwa wakiona mgombea wao anakubalika hawataki kabisa ushirikiano na mtu. Kama unataka ushirikiano ni wewe ndio utatakiwa kuwaunga mkono.

Ni kundi la watu wabinafsi sana.

Ubinafsi ndio tatizo kubwa linalowasumbua CHADEMA. Kutoka kwa viongozi wao mpaka wafuasi wao
 
Simchukii kila mwanaCHADEMA kwasababu mimi ni muumini wa UTU na sipendi UNAFIKI.

Watu wapuuzi na makatili wako vyama vyote na watu wema wako vyama vyote.

Chuki ya CHADEMA kwa Zitto imekuwa too much. Ni sawa na chuki ya CCM kwa Lissu.

Hivi siku mkipata madaraka Zitto atapona kweli?

Leo tena mmeanza kumshambulia Mdee, wiki kadhaa nyuma mlikuwa mnamshambulia Nyalandu.

Chuki nzito za nini?
CHADEMA inadai serikali itengeneze mifumo sio watu, lakini wao wanapambana na watu sio mifumo. Too much siasa.
 
Ila Chadema hadi saa hii game liko upande wao waendelee kuzichanga karata vema. Simama na shikilia hapo hapo unapoamini na endapo watu wanakuelewa komaaa tu. Hii Kitu mdio Mbowe anaitekeleza vema yaaani. No matter whaaaaaat!

Katiba Mpya & Tume Huru.

Yaani nyingine poroje tuuuuu, tupa kuleeeee 👉
 
Wakati wa uchaguzi mkuu 2020 aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chadema Halima Mdee aliutangazia umma kuwa amekamata mabegi yenye kura feki akasema hatotambua matokeo yake leo kaungana na waliomuibia kura.

Jana kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo ya Muhambwe na Buhigwe.

Asubuhi: Zitto Kabwe, tumetekwa na watu wenye mapanga maisha yetu yako hatarini, kuna magari matatu yamejaza maboksi yenye kura feki.

Jioni: Zitto, naipongeza CCM kwa ushindi wa halali kabisa Tume ya Uchaguzi imefanyakazi yake kwa weledi.

Binafsi nashindwa kuwatofautisha wanasiasa hawa wawili ndumilakuwili ukiwaacha (Mrema, Cheyo na Lipumba) matendo yao yanafanana kwa kiwango kikubwa ni waongo, wanafiki, wasaliti, hawaaminiki na wachonganishi. Wanataka wao ndio waonekane wanajua siasa kuliko wengine na la mwisho zaidi wote wawili ni ‘Opportunist’ wanaangalia maslahi yao kwanza.
Hakuna tafauti yoyote ile kati ya hao wawili,kuna wakati wakati wa Magufuli alipomuondoa waziri wa Madini Zitto alikuwa anajipendekeza sana kwa mwendazake alitegemea atapewa yeye, sasa hivi mama kasema katika uteuzi wake hatoangalia chama au lolote lile kwahiyo bwamdogo ameanza kujipendekeza.
 
Wakati wa uchaguzi mkuu 2020 aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chadema Halima Mdee aliutangazia umma kuwa amekamata mabegi yenye kura feki akasema hatotambua matokeo yake leo kaungana na waliomuibia kura.

Jana kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo ya Muhambwe na Buhigwe.

Asubuhi: Zitto Kabwe, tumetekwa na watu wenye mapanga maisha yetu yako hatarini, kuna magari matatu yamejaza maboksi yenye kura feki.

Jioni: Zitto, naipongeza CCM kwa ushindi wa halali kabisa Tume ya Uchaguzi imefanyakazi yake kwa weledi.

Binafsi nashindwa kuwatofautisha wanasiasa hawa wawili ndumilakuwili ukiwaacha (Mrema, Cheyo na Lipumba) matendo yao yanafanana kwa kiwango kikubwa ni waongo, wanafiki, wasaliti, hawaaminiki na wachonganishi. Wanataka wao ndio waonekane wanajua siasa kuliko wengine na la mwisho zaidi wote wawili ni ‘Opportunist’ wanaangalia maslahi yao kwanza.
Hawa hapa
Screenshot_20201208-061300.jpg
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom