Kwanini Halima Mdee na wenzake ni lazima wafukuzwe?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Hili ni swali ambalo kila mwanachadema na mpenda demokrasia anatamani leo litendeke kupitia Kamati Kuu. Lakini ipi sababu hasa ya kwanini wafukuzwe? Nini faida kwa CHADEMA ikiwafukuza? Nini hasara kwa CHADEMA ikiwaacha ndani ya Chama?

Tuanze na hili la kwanza, Baada ya kinachoitwa Uchaguzi ambacho sisi CHADEMA hatutambui kama ni Uchaguzi, Chama kilikaa chini na kutotambua chochote kitokanacho na uchaguzi huo. Halima Mdee na genge lake wakiwa ni moja wajumbe katika Kamati Kuu ya Chama iliyokaa na kutotambua uchaguzi huo.

Maazimio ya Chama pamoja na mambo mengine, yalikuja na madai ya msingi makuu matatu, 1. Tume ya Uchaguzi mpya huru na Haki iundwe, 2. Uchaguzi Urudiwe chini ya Tume Huru mpya, 3. Mchakato wa Katiba mpya uendelee pale ilipoishia Tume ya Jaji Warioba.

Ili kuhakikisha madai ya CHADEMA yanaishinikiza serikali ikubali kukaa mezani, CHADEMA ilijenga msingi wa mambo makuu matatu ambayo ndio silaha yake leo na kesho.

1. Ilikuwa ni Kushikilia Viti Maalumua ambavyo kwa namna Bunge lilivyokuwa, lilikosa uhalali wa kuwa Bunge la Vyama vingi. Hii ndio ilikuwa sila kuu kabisa ambayo serikali ilikuwa lazima ihitaji maridhiano na Upinzani, na dalili za serikali kutaka maridhiano na upinzani zilishaanza kuonekana wazi.

2. Jumuiya za Kimataifa kuishinikiza Tanzania kulegeza mbinyo wa demokrasia na kueleza wazi juu ya Uchaguzi ulikuwa Batili. Hili ni silaha kubwa na tayari EU ilishatoa msimamo huo na Uingereza na Marekani zinapiga jalamba.

3. Ni mapokeo ya Umma dhidi ya Chama kabla na Baada ya Matokeo.

Hayo matatu yalikuwa na bado ni silaha muhimu kwa harakati za CHADEMA kuhakikisha haki ya kidemokrasia nchini inapatikana kwa wazi. Halima Mdee yote haya alishiriki na anayajua vema.

Maadui walifeli na wamefeli kwenye kila eneo, hawana pakuanzia wala pakuishia, Sehemu waliyoona itajaribu kuwasitiri ni kujaribu kuwarubuni wanawake hawa kupitia Halima Mdee, Si kwamba Chama hakijui mipango yao yote tangu mwanzo, Kinajua kila kitu ambacho Halima na genge lake walikuwa wakifanya nje ya mfumo wa chama. Amelilia wembe ataupata

Viti maalumu deadline ni bunge la Mwezi wa nne, Naomba kurudia kusisitiza, Viti Maalumu Deadline ni bunge la mwezi wa Nne. Chama kinajua kucheza karata hii si vile Mdee na wenzake wanavyotaka kuaminisha umma. Halima kama Mwenyekiti wa BAWACHA anajua jambo hili kuwa Chama kilikuwa na mkakati gani na Chama ndio msimamizi wa Mabaraza yote.

Sasa katika tafsiri ya vita, Mtu anayeasi mapambano kama Mdee na kuungana na watesi na kuahidiwa kulindwa daima, unamsameheje abaki kwenye Chama? Labda hicho chama kinamalengo ya kwenda waliko CUF, TLP, NCCR nk. Lakini kama kinataka kuendelea kuaminika kwa UMMA ni lazima kiondokane na watu wa aina hii.

Faida ya Kwanza wakifukuzwa ni kwamba Watakosa uhalali wa kisheria kuwa wabunge wanaowakilisha CHADEMA Bungeni hata wakilindwa na Serikali. Pili Jumuiya za Kimataifa bado zitaendelea kutotambua bunge kuwa ni la vyama vingi kwakuwa Chama Kikuu cha Upinzania hakina Mbunge yoyote Bungeni. Madai ya Upinzani mbele ya Jumuiya za kimataifa yataendelea kuwa halali na yenye nfuvu. Kwahiyo ile mishemishe ya dola kujaribu kubumba upinzani feki Bungeni itakuwa imeingia luba.

Hasara kubwa kwa CHADEMA ikiwaacha, itapoteza uaminifu kwa umma wa mamilioni ya Wapenda denokrasia duniani, Pili Jumuiya za kimataifa zitakiona kama chama kisichoaminika mbele ya Watanzania na kwamba malalamiko yote ya Chama mbele ya Jumuiya za Kimataifa yatakosa uhalali. Na tatu, sasa Dola itakuwa haina tena hata wazo tu la kusukumwa kusikiliza madai ya upinzani juu ya Tume huru ya Uchaguzi, Katiba Mpya nk.

Halima Mdee na genge lake wana machaguo mawili tu, 1. Ni kujivua Ubunge na kubaki na Chama, 2. Ni kubaki na Ubunge na kwenda kwa dola. Uchaguzi ni wao... Kamati Kuu inawasubiri waamue nayo iamue... Wananchi wameshaamua.

Ikiwa Mdee na wenzake watachagua chaguo la pili, Chama kichague moja kubaki imara kwakuondoa wahuni hawa, au Kife kifo chepesi kwa kukubaliana na vurugu za Dola.

Ok, Usikose Kusoma VITABU hivi:

1. Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Bei ni 80,000/= (Kitabu Maalumu kwa wafanyamaamumzi/waliopevuka kiakili)

2. Strategy: The Road to Power, Bei ni 1,700,000/= (Kitabu Maalumu kwa wagombea Ubunge na Urais)

3. Mapambano ya Madaraka, bei ni 30,000/= (Kitabu Maalumu kwa Wagombea uenyeviti Mitaa/vijiji, Udiwani na watu wote)

4. Mtu baada ya Mtu, Bei ni 80,000/= (Kitabu kwaajili ya wote). KIKO MITAMBONI.

Nunua kwa:

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Instagram Follow @yerickonyerere_
 
Wengi hawafahamu kwamba kwasasa "DEREVA" gari limesha mshinda, linayumba yumba barabarani tu (Things Are Out Of His Hands And Out Of Control - The Country Is In Deep Murmuring Chaos).

Na kawaida gari linapomshinda dereva basi kila atakachotaka kufanya ili kulikweka sawa na kila anavyopapatua, ndio anapo haribu zaidi na kulitoa nje ya barabara.

Sasa hivi kila mtu anajifanya mjuzi kuliko dereva, na ndio wanazidi kumchanganya na kumptoteza kabisa dereva. Huyu kawasha end-cator, yule kapiga honi, huyu kakunja sight-mirror zote (Waziri Wa Mambo Ya Nje alichokonoa mambo vibaya. AG na SPEAKER leo ndio "WAMECHOMOA BETRI" kabisa).

Kwa tulipofikia, gari linasubiri sababu tu lianguke na kuua abiria. Hakuna hatua yoyote ya kuliokoa gari wala kumsaidia dereva. Zaidi ya kumwomba mungu idadi ya wafu na majeruhi iwe ndogo.

● Kwa wenye akili na maarifa (hata wana CCM wenyewe) ndio maana wamekaa kimya na kujiweka pembeni. Wanatazama tu. Wanajua impact itakayotusibu kama taifa.

● Cha kujiuliza,

1) Kwanini siku ya leo "SERIKALI IMEONESHA INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

2) Na kwanini bunge (Speaker) ameonesha "INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

■ Nchi ina mihimili mitatu. Mihimili miwili tayari (Serikali na Bunge) vimeshakuwa "BIASED". Umebakia mhimili mmoja tu "MAHAKAMA".

■■■ Kwanini nasema "KWA TULIPOFIKIA, GARI LINATAFUTA SABABU TU YA KUANGUKA NA KUUA ABIRIA"???

PRINCIPLE KUU YA UTAWALA

"Binaadamu ana mahitaji makuu, ambayo ni "Chakula, Matibabu na kuijua kesho yake". Binaadamu hawatawaliwi kwa nguvu bila hayo matatu na utawala ukafanikiwa.

Nature ya binaadamu, akiwa "AMESHIBA (Ana chakula/pesa) basi anakua binaadamu na anatawalika kirahisi, ila akiwa na "NJAA (Hana chakula/pesa)" akili inafanya kazi kupita kiasi na anakua mnyama asiekua na uoga wowote na muogope kama Covid-19 au HIV AIDS!!!

Kifupi, binaadamu mwenye njaa hatawaliki na yuko radhi kufanya lolote.

Nchi yetu raia hawana kipato na hawana mwelekeo kwa sasa. Mbele yao ni giza nene. Muda si mrefu hawata tawalika wala kutii serikali.

JIBU.

Sisi kama taifa, asilimia 98% ya raia wanalalamika hali ni ngumu kupita kiasi (Hawana pesa kukidhi "Kupata chakula, matibabu na hawaijui kesho yao). Serikali nayo haina pesa kujiendesha yenyewe kupelekea kuongeza kodi kwa raia wasio na kipato.

Raia wangekua na pesa ya kukidhi mahitaji yao. Basi dereva angefanikiwa kuliweka gari sawa.

Hili ni "TIME BOMB (BOMU)" kwa serikali yetu, bomu hili linalosubiri muda/kiberiti tu liripuke. Kinacho chelewesha ni raia kuwa "WAOGA" bado, ila uoga ukitoweka kwa raia bomu linaripuka.

USHAURI KWA CHADEMA.

Wakikaidi na kuachana na "VITISHO VYA A.G na SPEAKER" kisha wakafanya maamuzi ya kuwafukuza "UWANACHAMA" hao 19 waliosaliti, kisha wakaongeza "PRESSURE ZAIDI NA ZAIDI" kwa dereva. Dereva watamchanganya zaidi na kupindua gari ndani ya muda mfupi sana.

Katika mapambano yoyote (hata mpira wa miguu), adui yako mwenye nguvu anapokua na "PRESSURE NA KUJIKANYAGA KANYAGA", usimpe nafasi ya kujipanga, ongeza pressure na mashambulizi zaidi ili aharibu zaidi na umjeruhi zaidi. Na kamwe usilipe fadhila ya kumpunguzia mashambulizi.

CHADEMA wakiamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite (Wasipo wafukuza hao wasaliti 19 uwanachama) basi gari litapunguza kasi kidogo, pengine dereva akajitambua na gari litadondoka upande waliokaa wao CHADEMA na kuwaua (Chama kitakufa na kupoteza wanachama kama CUF ya Lipumba).

ZINGATIO

Ili CHADEMA na ACT WAZALENDO kuleta madhara zaidi na zaidi kwa Serikali ya CCM, Chadema "KUWAFUKUZA UWANACHAMA HAO WASALITI 19" haitoshi, japo ndio maamuzi sahihi ya kuchukua.

Baada ya kuwafukuza hao 19, kama vyama vya upinzani vikuu vinapaswa kuongeza "PRESSURE ZAIDI NA ZAIDI (ADD MORE PREESURE AND MORE PRESSURE) kwa serikali na NEC kutoa majibu ya hao waliopeleka hayo majina na kusign hizo form. Isiipe serikali nafasi ya kuvuta pumzi hata kidogo wala nafasi ya kujipanga.

Serikali na NEC isipotoa majibu ya kuridhisha, basi iendelee kupiga "KELELE" katika mataifa yenye nguvu duniani pamoja na AU/UN kuingilia kati.
 
Nyerere ifike hatua chadema lazima mji tambue na mfanye siasa Kutokana na Hali ya wakati uliopo

Hayo madai yenu Hayana msingi bcoz Mnadai kwa faida yenu wanasiasa na sio faida ya wananchi

Hivi kwa akili yako unadhan jpm atarudia uchaguzi? Kwa akili yenu Kuna katiba mpya hapa soon?

Nyie mkiambiwa lipieni uchaguzi hizo ela mnazo?

Mnaacha kujijenga kwa miaka mitano hii nyie kila siku ni tume Mpya na katiba mpya utadhan hakuna kitu kingine Cha serikali kufanya zaid ya kuwasikiliza nyie tu

Kama kweli mnahoja si muende ikulu pale mkadai hiyo katiba mpya mbona unaongea ukiwa zako umekaa kigamboni huko
 
Umeongea mengi ila unachotakiwa kujua ni kuwa politics is a game if chance.

Unatumia silaha yoyote ukishapata target..
Kwa sasa kuna uwezekano wa kuisambaratisha chadema na kuwatia udhaifu zaidi..kudhoofika kwa ccm ni neema kwa chadema na kudhoofika kwa chadema ni neema kwa ccm..ndio maana 2015 mlikuwa mnashangilia kuwa ccm inaenda kumfia jk mikononi.
 
Acha upuuzi huyo JPM wako alisema CHADEMA wanachelewesha maendeleo, iweje leo CHADEMA wangeuke waleta maendeleo? Yeriko upo sahihi sanaa
Sasa jpm ndio Rais wa TZ kama hutaki Hilo vuka borders nenda msumbiji

Kazi ni kupiga kelele ambazo hazina msingi
 
Back
Top Bottom