Ni vigumu kwa Mwafrika Dr Tedros Ghebreyesus kuendelea kuongoza WHO, Marekani yaondoa fedha za mchango nyuma ya pazia, yashinikiza Tedros aondolewe

Atoke ni mjinga sana huyu jamaa..!

Kuficha taarifa za hatari ya huu ugonjwa kwa kuangalia maslahi ya china kunapelekea dunia kuingia kuzimu na hawa virusi.

Kwanini walichelewa kutoa tahadhari ya mapema kwa dunia kukaa mbali na China ili kutoa mwanya wa kushughulikia hawa virusi wakiwa China.

Kuna uzembe mkubwa umeigharimu dunia na maisha ya watu yanateketea kwasababu ya ujinga wa Mchina. Wachina ni watu wabinafsi kabisa kwenye hii dunia. Na inafaa dunia kuwawajibisha kwa uzembe walio ufanya wapuuzi hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kawawajibishe MKUU.

Sent using My COVID-19
 
Dr Tedros alianza kuonekana kwenye televisheni duniani akitoa maelezo mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.

Pia aliweza kuonekana akijibu masuali mbalimbali ya waandishi wa habari juu ya maendeleo ya ugonjwa huo na taarifa zingine nyingi tu kupitia mitandao kama ya twitter na kadhalika.

Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus ambae ni raia wa Ethiopia, alichaguliwa kuongoza WHO miaka mitatu ilopita kwa kipindi cha miaka mitano katika mkutano mkuu wa shirika hilo ambalo lipo chini ya Umoja wa Mataifa.

Ni Mkurugenzi wa kwanza ambae alichaguliwa kutoka kwenye kundi la wagombea zaidi ya mmoja na ni Mkurugenzi wa kwanza kuongoza shirika hiko kutoka bara la Afrika.

Dr Tedros kitaalam ni mtafiti wa ugonjwa wa Malaria na alipokuwa nchini kwake aliwahi kushika nafasi za uwaziri wa afya na uwaziri wa mambo ya nje toka mwaka 2012 hari 2016.

Dr Tedros ana shahada ya kwanza ya sayansi ya bilojia alohitimu kutoka chou kikuu ya Asmara (sasa mji mkuu wa Eritrea) mwaka 1986.

Pia baadae mwaka 1993 Dr Tedros alihitimu shahada ya uzamili inayohusu magonjwa ya kuambukiza kutoka chou kikuu cha London kitivo cha tiba za magonjwa ya kitropiki na baadae mwaka 2000 akafuzu shahada ya uzamivu kuhusu afya ya jamii kutoka chou kikuu cha Nottingham nchini Uingereza.

Katika kazi ambazo Dr Tedros amenekana amezifanya kwa ufanisi ni pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi katika mkoa wa Tigray ambao alipangiwa kazi, na ugojwa wa uti wa mgongo kwa asilimia 69.

Pia chini ya uangalizi wake Dr Tedros alihakikisha kila hospitali, kituo cha afya na cliniki mkoani humo vinaunganishwa na mtandao wa kompyuta na kunakuweko na mtandao wa intenet ambao haukatiki mambo ambayo hayakuwahi kuwepo mkoani humo.

Jambo jingine kubwa ambalo mtaalam huyu alilifanya kwa nchi yake ni kuhakikisha kila kilomita 10 kunakuwa na kituo kinachotoa huduma za afya na kuwezesha asilimia 60 ya wananchi wanapata huduma hizo.

Pamoja na sifa hizo pia Dr Tedros amesimamia kampeni dhidi ya magonjwa kama wa kifua kikuu, uzazi wa mpangp na kusaidia kuzuia mimba za utotoni na kuboresha afya za akina mama na watoto.

Dr Tedros anaelezwa na vyanzo mbalimbali kwamba ana sifa au skills za uhamasihaji na ni mhamasishaji na mjenga mzuri na ana uwezo wa kuleta hoja na kuhamasisha jambo na likakubalika.

Bila shaka kutokana na rekodi hii shirika la afya duniani lenea makao yake makuu mjini Geneva nchini Switzerland likamchagua Dr Tedros kutoka kwenye kundi la watahiwa wengine wenye sifa mbalimbali.

Leo hii Rais Donald Trump anatangaza kusitisha mchango wa Marekani kwa WHO akitoa sababu kwamba shirika hilo la afya duniani limeshindwa kusimamia kimadhubuti ugonjwa wa COVID-19 na pia limeshindwa kuibana China ambayo imekuwa haitoi ushirikiano khasa wa kupeana taarifa kuhusu taarifa za ugonjwa huo.

Pia katika madai hayo Rais Trump akasema WHO haikupaswa kuipongeza China kwa kuwa wazi kwenye kutoa taarifa za ugonjwa wa COVID-19.

Pia baadae Jumatano Rais Trump kuona hio haitoshi akaamua kusema kabisa dukuduku lake kwamba China imekuwa inadanganya katika taarifa zake za ugonjwa wa COVID 19.

Marekani ni mchangiaji mkubwa kwenye shirika hilo kiasi cha dola milioni 400 kwa mwaka na China imejibu kwa kuiomba Marekani ifikirie uamuzi wake huo.

Pia Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedros naye amesema WHO inasikitishwa na uamuzi huo wa serikali ya Marekani chini lakini inaamini kwamba uamuzi huo utafikirwa upya na Rais Donald Trump.

Mpaka sasa nchi nyingi hazijatoa tamko lolote lile kuhusiana na uamuzi huo wa Marekani wala kujibu kauli zinazotoka Washington lakini baadhi wameanza kuonekana wanaunga mkono kaui za Rais Trump.

Nchini Uingereza mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi wa nje la MI6 bwana John Sawer amesema kwamba China ilificha kwa dunia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa COVID -19.

Jasusi Sawer amesema ujasusi ni kupata taarifa ambazo zimefichwa usizipate kutoka kwenye nchi na wahusika wengine. Lakini kulikuwa na ufichwaji wa taarifa za awali zilizokuwa zikitolewa tangu mlipuko uanze mwezi Disemba na januari kwa nchi za magharibi na Marekani.

Madai hayo ya jasusi huyo mbobezi yanalingana na madai ya majasusi wa Marekani na vyanzo vingine mbalimbali ambao walimpatia raisi Trump taarifa kwamba pamoja na kirusi COVID -19 kutokea kiasili lakini kuna kila dalili kwamba kirusi huyo alitengenezwa kwenye maabara ya Virolijia mjini Wuhan.

Taarifa hizo zimeeendelea kudai kuwa kulikuwa na mwanafunzi wa kike katika maabara hiyo ambae hakufuata protokali za matumizi ya maabara hiyo na kwenda nyumbani akiwa ameambukizwa kirusi hichi kicha kwenda kumuamnukiza rafiki wake wa kiume ambae naeoi Kesho yake alikwenda kwenye soko la wanyama ambalo halikuwa katika mazingira mazuri ya usafi.

Rais Donald Trump akihojiwa na mwandishi wa Fox News bwana John Robert ambae aluliza kwamba, ‘Multiple sources are telling Fox the US government now has high confidence that while the coronavirus is a naturally occurring virus, it emanated from a virology lab in Wuhan.

Rais Trump akajibu kwa kusema ,‘I don’t want to say that John, but I will tell you, more and more were hearing the story and we’ll see.’

Rais Trump pia alionyesha kukubaliana na vyanzo vya bwana Robert kwa kusema,, ‘and when you’re saying multiple sources there's a case when you can use the word sources. But we are doing a very thorough examination of this horrible situation.’

Ikumbukwe pia katika kipindi hicho daktari mmoja nchini China Dr Li Wenliang alikufa baada ya kuambukizwa ugnjwa huo na kabla ya kifo chake aliwaonya marafiki zake juu ya ubaya wa ugonjwa huo na baadae kuitwa kwenye kamati ya maadili ya chama cha kikomunisti.

Sasa mpira umeelekezwa kwa Dr Tedros kwamba ameisaidia China kudharaiu taarifa za awali za mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 na hiyo ikiwa ni baada ya wataalam na wachunguzi mbalimbali kuunza kutaka Mtaalam huyo ajiuzulu nafasi yake hiyo ya ukurugenzi mkuu.

Dr Tedros amejikuta katika mgogoro wa mataifa haya makubwa Marekani na China, mgogoro ambao ni wa muda mrefu na kitovu chake kikiwa ni mkataba wa kibiashara.

Lakini bila kufahamu nafasi yake haikuwa ni ya kudumu malai hapo na wengi watu wasio waafrika hawakuwa wanafurahia kwa mtu kama Dr Tedros kushika nafasi hiyo na kuzungumza na vyombo vya habari vya dunia.

Wiki ilopita bara la Afrika na waafrika walitoa kauli za kumuunga mkono Dr Tedros huku mwenyekiti wa Umoja wa Afrika bwana Moussa Faki Mahamat akisisitiza umoja kwenye kupambana na ugonjwa huo hatari.

Rais Kagame wa Rwanda nae alitoa kauli yake kupitia mtandao wa Twiter kusema kwamba huu si wakati wa siasa bali nguvu ya pamoja kupigana na ugonjwa wa COVID-19. Viongozi wengne walotoa kauli za kumuunga mkono Dr Tedros ni wa nchi za Afrika Kusini, Namibia na Nigeria.

Lakini mazingira yanayozidi kutengenezwa yanaweka njia ya kuondolewa kwa mtaalam huyo ili mataifa ya magharibi yweze kutekeleza ajenda zao.

Dr Tedros anajaribu kuunganisha juhudi kwa nchi wanachama wapatao 194 zijitahidi kuchangia shirika hilo na akifanikiwa kwenye hili basi atatoboa.
Hata mm naunga mkono kuondolewa kwake . Hoja ya uafrika isiwekwe kabisa mbona koffe Anani aliongoza . Dr anaficha ukweli Bila shaka wachina wamesha mnunua tuu siunajua China wapo karibu na wale wanunuaji watu hivyo kumnunua Dr sio shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mm naunga mkono kuondolewa kwake . Hoja ya uafrika isiwekwe kabisa mbona koffe Anani aliongoza . Dr anaficha ukweli Bila shaka wachina wamesha mnunua tuu siunajua China wapo karibu na wale wanunuaji watu hivyo kumnunua Dr sio shida

Sent using Jamii Forums mobile app

Dr Tedros amepata watetezi wengi.

Kwenye mkutano wa G20 ulofanyika hivi karibuni viongozi wa mataifa mengi ya magharibi wamepinga jitihada za raisi Trump za kutaka kumtoa Dr Tedros awe mbuzi wa kafara.
 
You have no proof whatsoever kwamba China ilikuwa ikimwambia Dr. Tedros kufanya kitu ana yeye anaact. By the way kila Nchi inapaswa kufanya tafiti zake na kujilinda accordingly. Kuna evidence kwamba CDC ya USA waliiona hii kitu mapema na wakaanza kuchukua hatua kimyakimya. Obama alionya kitu kama hii mapema kabisa lakini people did not listen at all au walipuuza. Nchi Kama South Korea na Singapore waliact faster.

Bottom line: hatuwezi kuwabebesha lawama WHO if somebody somewhere failed miserably to act timely, decisively and in a professional manner.
Jukumu la kiafya la ulimwengu liko kwa nani?. Kama sio WHO. Hivi Trump angefunga mipaka mapema usingekuja na lawama kwamba jamaa ni mbaguzi?. Basi kama ni hivyo shirika la afya lisiwepo la nini sasa?. Halifai abadan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom