Ni upuuzi kutoza 300/- Ubungo Bus Terminal.

Ni upuuzi kutoza 300/- Ubungo Bus Terminal.

Ubungo bus terminal ni kichaka cha walanguzi,mods pandisheni huu uzi kwenye social medias zote wauone wadau, watoe nyongo zao labda tunaweza pata ahueni
Ubungo mule ni kichako, dampo la wakabaji, Matapeli, mazingira mule ni mabaya
Abiria wengi wakikaribia mule huingia na wasiwasi

Ova
 
Huwa wanakagua tarehe
Nyie huwa mnatoa pesa kumbe [emoji23] [emoji23] [emoji23] mimi nina tiketi zaidi ya 5 kwenye wallet nikifika natoa nawaonesha na kuingia.

Nataka kuandika barua ya kuomba radhi kwa uhujumu uchumi.
 
Si hapo tu , kuna maeneo mengi, hakuna value 4 money, Rais anapotoa tamko akiwa eneo Fulani ( machinjio ya vingunguti) maana yake maeneo yote yenye ukakasi YAJITAFAKARI.

Hivi nyinyi viongozi Wa Dar, mpaka aje Mh Magufuli aje awaambie msitoze ushuru mpaka mboreshe huduma kwa wadau.

Msimchoshe kama asivyowachosha, mmeshindwa pisheni.

Mh Magufuli KONGOLE nchi inasonga.
Ukisha mpa chake mwenye mkoa wake wwe unafanya chochote unachotaka labda Raisi aingilie kati kama alivyoingilia kati huko Vingunguti!
 
Kuna wale wapiga debe kuanzia ‘sheli’ pale, kuna mkwara wanatangazia abiria ‘kama huna tiketi pitia huku’..... ukibabaika tu anajua wewe huna tiketi anakukomalia akupeleke ofisini.
Mimi wale wapiga debe wakini komalia huwa nawaambia wanipeleke kwenye ma bus yanayokwenda Zanzibar basi hapo hapo wanajiona wao ndiyo wakuja na wanakua wapole wananiacha nasepa zangu na mambo yangu!!
 
Issue nyingine ni stendi pale mbezi mwisho kuna vyoo vya kulipia shilingi 500 lakini hawatoi risiti kitu ambacho kinainyima halmashauri/manispaa mapato.Yaani watu wanaweka pesa mfukoni tu kuna haja ya kupaza sauti ili ushuru wetu tunaotozwa ufanyie mambo ya maendeleo.
Sawia kabisa mkuu, umeelezea kila kitu.... kongole kwa Mlimani City.
 
AWAMU HII HAKUNA UPIGAJI.
[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
AWAMU HII HAKUNA UPIGAJI.
[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]

Kalagabaho, vile vikaratasi pale wanakupa kama risiti unajua kama ni vyao tu wamechapisha..!!
 
bob ndio umeanza kwenda ubungo terminal leo?? au huwa husafiri safiri sana?? Maana hako kautaratibu kapo mikoa mingi tu na tuliishazoea.

Njia za kukwepa huo usumbufu ni kuwa na ticket hata iliyotumika halafu unapita fasta kama unaharaka vile.

Kama huna ticket basi toa noti ya 10,000 huku unatembea kwenda mbele mimi sijawahi kuona wakipokea.
 
Hii ni kero kubwa na inafanyika kienyeji sana, watu wa hovyo wanakusanya ‘ushuru’ kiholela tu na bila shaka pesa wanajipigia tu ndio maana miaka nenda rudi hakufanyiki lolote pale..... kama airport nasindikiza na kupokea wageni bila kiingilio hapo Ubungo kuna nini..?

Uzi tayari.
bora umeliona hilo,,ila kule Babati Manyara kuna kastendi kao kapo vichakani kichenzi,,stendi ipo km kambi ya wakimbizi maana kulia,kushote,kaskazini ma magharibi kote imezungukwa na machaka ambayo ukiingia tu humo machakani hutoki bila kukumbana na nyoka hatari,,lakini cha ajabu kuingia steni hapo kwa abiria au mtu anayeenda kupokea mgeni wake ni lazima atoe kiingilio,nadhani ni 200 au 300 kwa kichwa,,,maajabu kweli kweli,,,si bora hata huko ubungo jmn??,,,sasa pale machakani kiingilio ni cha nini jamani??,,au kuna live band huko ndani??
 
Back
Top Bottom