Ni upuuzi kutoza 300/- Ubungo Bus Terminal.

Ni upuuzi kutoza 300/- Ubungo Bus Terminal.

Chaka liko nyuma kule wanakooshea mabus,halafu ile asubuhi kuna wezi wanakaa parking mle ndani na vicorolla vyao,wanapiga power window,redio,side mirror,na walinzi wa wanawajua,
Hakuna usalama hata kidogo
Abiria wengi wakifikiria kushukia hapo Wanajua ni maumivu
Alafu bado pia Kuna polisi feki mule
Na mpaka Sasa mazingira ya mule Kuna watu wanayalinda

Ova
 
Hii ni kero kubwa na inafanyika kienyeji sana, watu wa hovyo wanakusanya ‘ushuru’ kiholela tu na bila shaka pesa wanajipigia tu ndio maana miaka nenda rudi hakufanyiki lolote pale..... kama airport nasindikiza na kupokea wageni bila kiingilio hapo Ubungo kuna nini..?

Uzi tayari.
Nilitaka ni comment na neno baya sana kwa hao watu wa ubungo ila nimeeleweka
 
Na kule juu ya daraja la mwendokasi sijui wanawaacha wapiga debe wa nini, wanawashika watu hovyo hasa jinsia ya ke, sio ustaarabu kabisa
 
Na kule juu ya daraja la mwendokasi sijui wanawaacha wapiga debe wa nini, wanawashika watu hovyo hasa jinsia ya ke, sio ustaarabu kabisa

Kuna wale wapiga debe kuanzia ‘sheli’ pale, kuna mkwara wanatangazia abiria ‘kama huna tiketi pitia huku’..... ukibabaika tu anajua wewe huna tiketi anakukomalia akupeleke ofisini.
 
Nyembe zilinisaidia kipondi kimoja hivi pale mwenge magari ya mikoroshini yalikuwa yanapakia karibia na mataa. Basi gari ikija teja yupo busy anafungua mabegi ya kupgia search fasta. Mie ule mfuko wa nyuma nilfungua topaz 10 mpya!
Nkaziweka na kufungua zipu kidogo nimtamanishe. Then nkagombania daladala! nkasikia mjomba anasema watu wengine waganga, wachawi miwembe ya nini?
Hahaha....
Kuna siku utakuja kunikumbuka kuwa Santino aliwahi kuniambia anatembea na sindano na nyembe kwenye wallet.
 
Nyembe zilinisaidia kipondi kimoja hivi pale mwenge magari ya mikoroshini yalikuwa yanapakia karibia na mataa. Basi gari ikija teja yupo busy anafungua mabegi ya kupgia search fasta. Mie ule mfuko wa nyuma nilfungua topaz 10 mpya!
Nkaziweka na kufungua zipu kidogo nimtamanishe. Then nkagombania daladala! nkasikia mjomba anasema watu wengine waganga, wachawi miwembe ya nini?
Hahaha....

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uzi bora kabisa wa leo.........
Hivi hela wakusanya za Nini....
*mazingira mabovu/hakuna sehemu za abiria kukaa za kutosha
*vyoo vichafu na unalipa Tena
*Kuna vibaka,
*Kila basi inalipa tena,
*taa haziwaki kwa sehemu kubwa/Giza,
*mpangilio wa basi hovyo hakuna sign/maelekezo

Airport/jni na Mlimani city Kila siku wanaingia maelfu ya watu kwa kupishana, ila VYOO VISAFI SANA na HAKUNA KULIPIA, mazingira mazuri kuliko ubungo/bt shida Nini...

jamiiforum @maximello na wadau wengine hebu hii mada isambazeni Hadi kwenye platform zingine ijadiriwe tupate majibu
 
Hii ni kero kubwa na inafanyika kienyeji sana, watu wa hovyo wanakusanya ‘ushuru’ kiholela tu na bila shaka pesa wanajipigia tu ndio maana miaka nenda rudi hakufanyiki lolote pale..... kama airport nasindikiza na kupokea wageni bila kiingilio hapo Ubungo kuna nini..?

Uzi tayari.
Si hapo tu , kuna maeneo mengi, hakuna value 4 money, Rais anapotoa tamko akiwa eneo Fulani ( machinjio ya vingunguti) maana yake maeneo yote yenye ukakasi YAJITAFAKARI.

Hivi nyinyi viongozi Wa Dar, mpaka aje Mh Magufuli aje awaambie msitoze ushuru mpaka mboreshe huduma kwa wadau.

Msimchoshe kama asivyowachosha, mmeshindwa pisheni.

Mh Magufuli KONGOLE nchi inasonga.
 
Kuna wale wapiga debe kuanzia ‘sheli’ pale, kuna mkwara wanatangazia abiria ‘kama huna tiketi pitia huku’..... ukibabaika tu anajua wewe huna tiketi anakukomalia akupeleke ofisini.
Yani kama upo akilini mwangu, nilikutana na hii kitu. Lengo langu ni kwenda kuchukua mzigo nilitumiwa, nimeshuka kwe' mwendokasi kumbe ukifika kule juu kwe' daraja Kuna option mbili aidha uende uelekeo wa kuingia ndani wanakopandia mabasi au nje zilipo ofisi kwa ajili ya kuchukua mzigo.
Si akanichanganya yule mpigadebe akasema pita huku nikajikuta natokea ndani ambako ilinipasa nilipe ushuru, wkt ilikua hakuna haja sababu nilitakiwa niende kwe' ofisi kuchukua mzigo na kusepa zangu. Ni ela ndogo but iliniuma plus usumbufu.
 
Mmmh ngoja kwanza nisome comment ntarudi baadae
 
Ubungo bus terminal ni kichaka cha walanguzi,mods pandisheni huu uzi kwenye social medias zote wauone wadau, watoe nyongo zao labda tunaweza pata ahueni
 
Uzi bora kabisa ya leo.........
Hivi hela wakusanya za Nini....
*mazingira mabovu/hakuna sehemu za abiria kukaa za kutosha
*vyoo vichafu na unalipa Tena
*Kuna vibaka,
*Kila basi inalipa tena,
*taa haziwaki kwa sehemu kubwa/Giza,
*mpangilio wa basi hovyo hakuna sign/maelekezo

Airport/jni na Mlimani city Kila siku wanaingia maelfu ya watu kwa kupishana, ila VYOO VISAFI SANA na HAKUNA KULIPIA, mazingira mazuri kuliko ubungo/bt shida Nini...

jamiiforum @maximello na wadau wengine hebu hii mada isambazeni Hadi kwenye platform zingine ijadiriwe tupate majibu

Sawia kabisa mkuu, umeelezea kila kitu.... kongole kwa Mlimani City.
 
Back
Top Bottom