Hakuna hela inayoniuma kama ile Tshs 300 ninayolipa pale Ubungo Bus Terminal

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,891
2,368
Wakuu habari,

Kiukweli ikitokea nina safari na inanipasa nikakatie tiketi ndani ya Kituo cha Mabasi Ubungo, basi hakuna hela inayoniuma kama ile Tshs 300/= ninayolipia pale mlangoni.

Juzi nilienda kumpokea mgeni wangu anaetoka mkoani na kwakuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuja Dar, ilinipasa kuwahi mapema pale stendi. Nikalipa kiunyonge ile 300/= kisha nikaingia ndani.

Mazingira mabovu. Sikuona hata sehemu ya kukaa kusubiri mgeni wangu hivyo ikanipasa kukaa kwenye vile vibaraza vinavyotenganisha mstari mmoja na mwingine wa parking za mabasi. Iliniuma ila sikuwa na jinsi maana ni kula vumbi tu, na basi likija na kutaka kuegesha sehemu niliyokaa inanipasa niinuke na kulipisha.

Nikatoa ile tiketi na kuikagua kwa umakini, nikaja kugundua kuwa tiketi ilitolewa toka saa nne asubuhi na mimi nilifika pale saa kumi na moja jioni.

Nilichogundua wakati wa kutoka ukiwapa ile tiketi pale mlangoni wanairudisha tena kwa mwingine atakayeingia. Hivyo, tiketi moja inaweza kuuzwa kwa watu hata kumi kwa siku. Huu ni wizi mwingine unaofanywa na wale wakatisha tiketi.

Baada ya mgeni wangu kufika nikampokea na kutoka naye nje. Nilipofika mlangoni jamaa akataka nimpe tiketi yangu nikamuonesha tu na kumkatalia kuwa inanipasa nibaki nayo kama ushahidi kuwa hiyo siku niliingia ubungo stendi. Nikaondoka na tiketi yangu.

Niwape hongera Kilimanjaro Express na Dar Lux kwa kuwa na terminal zao. Natamani mabasi yote yangekuwa na terminal zao kutupunguzia huu wizi unaofanywa pamoja na huduma mbovu za Ubungo Bus Terminal.
 
Kwa utaratibu ule wa pale Ubungo huwa nawaza kutafuta mbinu ya kukwepa kulipa tu.

Ila si niliskia kuna mpango wa stand ya mabasi ile kuhamishwa iende Mbezi sijui au Tegeta.
 
Kuna mpuuzi mmoja pale UBT alitaka kunichelewesha kisa Shilingi 300 kidogo tuzichape, isingekuwa safari kingenuka asee
 
Vyoo vichafu vimejaa maji, nako kila uingiapo lazima ulipe kutokana na huduma inayokuingiza humo, sijui kwa nini walau hiyo 300 isingetumika kuwalipa wa msalani.
 
Kuna mdau mmoja aliwahi kuniambia kuwa yeye huwa anaondoka kama na laki au laki mbili Kwa siku.
 
Vyoo vichafu vimejaa maji, nako kila uingiapo lazima ulipe kutokana na huduma inayokuingiza humo, sijui kwa nini walau hiyo 300 isingetumika kuwalipa wa msalani.

Ni upuuzi mtupu, getini ulipie na huduma za ndani ulipie... afadhali hata kungekuwa na huduma nzuri basi.
 
Stendi kubwa vilee vyoo vya kubip tu ,in usenge tu .tunafanyiana pale
 
Back
Top Bottom